Wana JF wenye ufahamu na Itifaki tusadiane hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF wenye ufahamu na Itifaki tusadiane hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jagermaster, Feb 15, 2011.

 1. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii picha inaonyesha kikao kimojawapo muhimu katika maandalizi ya Bunge huko Dodoma. Katika viongozi waliokaa hapo, anaonekana katibu wa Bunge, Spika, Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar. Nataka kuuliza hivi makamu wa pili wa rais wa Zanzibar hapo kwenye meza kuu ya Bunge la URT anakaa kama nani?. Hivi hawa viongozi wetu wa selikari huwa wanaongozwa na watu wa Itifaki wanapokaa katika vikao kama hivyo au wanajiamulia tu kwamba flani kaa hapa?. Hivi huyo makamu wa pili wa rais wa Zanzibar anaingia Bungeni kama makamu ya rais wa Zanzibar au kama mbunge wa kawaida?. Kama kitendo hicho kinafanyika bila kanuni yoyote, hivi kweli Tanzania tunaongozwa kwa kanuni zozote au viongozi wetu wanaamua katika vikao vyao vya faragha juu ya itifaki wanavyojisikia. Watu waliokuwa ukaribu na tukio hilo watujuze, hii itifaki iliamuliwa na nani maana inaonyesha ilikuwa mbele ya waandishi wa habari.
   

  Attached Files:

 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  huyo makamu wa zanzibar ni mbunge huko kwao...
  but sijui hapo amekaa vipi?
  tusubiri lawyers waje....
   
Loading...