Wana Jf Tuzipate Forms Za Mafisadi Toka Tume Ya Maadili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana Jf Tuzipate Forms Za Mafisadi Toka Tume Ya Maadili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Apr 22, 2008.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Tume ya maadili imekataa kutoa forms za maadili za viongozi mbalimbali ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi nchini.

  Mimi nashauri JF tuingie kazini na kuzitafuta hizo forms hata kama itakuwa na maana kuzinunua.

  Hizi sheria wanazotunga ili kuwakingia kifua wasiumbuke, njia ya kuziua ni kutafuta njia ya kuzikiuka.

  Mtu kama anaandika uwongo akijua hautajulikana basi tutumie JF kuwaumbua.

  Ninaamini inawezekana kabisa kuzipata hizo forms hata kama zinalindwa na RO.

  Wazee wa kazi hima hima tuelekee kazini.

  Ningetaka kujua fisadi Mkapa aliandika anamiliki nini.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sikutegemea kama hawa waficha mafisadi wakubali kuzitoa form hizo.
  ila ilikuwa move nzuri kwa upinzani kwenda kudai ili tu wapate wakatae tujue kwa uwazi msimamo wao.
  kupatikana kwa form hizo ni ngumu, ila wanaweza kushinikizwa kufanya hivyo kwa maandamano na kupigiwa kelele kila kona.
  tukianza na bungeni, kwenye vyombo vya habari na kwa wananchi mmoja mmoja kulalamika
   
 3. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mkuu wazo lako limenisismua sana, umeongea jambo la muhimu sana, wana JF kama tupata nyaraka nyingine muhimu sidhani kama hii itatushinda, tuingie kazini mwenye uwezo atusaidie, Invisible fanya kweli
   
 4. Mpangwa Asilia

  Mpangwa Asilia Member

  #4
  Apr 22, 2008
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wala si fisadi bali ni LIJIFISADI la nguvu. Haiwezekani watu wake wakafisadi yeye akatulia.
  Ni jambo jema sana kuzipata hizo form na ndo zitakazotupa mwanga wa jinsi gani mgonjwa huyu "TANZANIA" ni mahututi. Hima tuliokoe taifa letu tukufu.
   
 5. Gigo

  Gigo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2008
  Joined: Aug 6, 2006
  Messages: 455
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Hakuna fomu yeyote!!...hakuna kitu kama hicho..labda waziandike upya!!

  Kama hela...kama Mali zina kufanya uwe Mpumbavu basi utakua mpumbavu hata kwenye mambo mengine!!

  hiyo Sheria iliwekwa na wajinga!!CCM...na hivyo vyama vingine hakuna kitu...mavi matupu!!
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Gigo,

  Ndio maana ni muhimu kuzipata hizo forms maana tunajua wamedanganya.

  Kama mtu ana mali na hajaweka kwenye hizo forms ina maana ni mali za wizi.

  Wananchi taratibu wataanza kuelewa kinachoendelea. Mtu uliye na mali halali, huwezi kuficha kuiandika unapotakiwa na sheria.
   
 7. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  NA HATA KAMA HAKUNA FORMS TUNATAKA HABARI YA UHAKIKA KABISA TOKA NDANI KUWA HAKUNA FORMS ILI TUJUE MOJA NA NI WAPI PAKUANZIA ILI WATAJE NA KIELEWEKE
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Swali ni kwanini wanaficha, majibu yameanza kujulikana, sasa zikitolewa hizo nyaraka wengi wataumbuka!
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Wazo ni zuri sana,ila Sheria ya Maadili ya uongozi wa umma ni ngumu sana,na sidhani kama ni rahisi kuzipata,na wakati mwingine huwa nafikiria kama sheria iko hivi ni bora hapa hii tume ifutwe.
   
 10. n

  nat867 Member

  #10
  Apr 22, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nina wasiwasi kwamba tume ya maadili inaweza kubadilisha fomu za mafisadi na kuongeza mali ambazo tunazilalamikia kama ilivyokuwa faili la richmond pale BRELA. Mhh! Ila nimefurahi move ya wapinzani jana!
   
 11. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Mtakuta kwenye form zao wameandika ana Ngombe watatu wa maziwa kuku 50 wa mayai gari la ubunge lina mkopo nyumba aliyeuziwa na serikali!
   
 12. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kuna haja ya kuomba hii tume ifutwe. Haina maana zaidi ya kula pesa. Ni wangapi wamefikishwa kwenye tume hii?

  Imekaa mno kisiasa inaonekana kuwa kichaka cha kulindia maovu.
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mtanzania Mkapa alipoingia madarakani alitangaza "mali zake"....na aliahidi kufanya hvyo siku siku atakapoondoka madarakani.........mpaka leo sijawahi kusikia wapi alitangaza mali zake baada ya kumaliza kipindi chake.......
   
 14. K

  Kinto Senior Member

  #14
  Apr 22, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haiwezekani hao hao mafisadi wa sasa ambao walikuwa wabunge wa wakati huo wajitungie sheria ya kuwabana,halafu iwe valid mpaka leo. Sheria hii ipitiwe tena inaonekana ina mapungufu mengi kama alivyokiri JK
   
 15. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kwani zinaenda kuombwa au zichukuliwe kimtindo?
   
 16. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii ni next assignment ya JF.
  Wao wanakozificha huko ndiko wengine tunanawa nyuso.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Naam zikiwekwa hapa ukumbini itasaidia kupambana na hatimaye kuishinikiza ili hii sheria ya kipumbavu ambayo inawalinda mafisadi iondolewe.
   
Loading...