Wana JF Tuungane na Member SAJENTI...Ana Wakati Mgumu

Mungu akubariki kwa kujitoa kwako. Na mimi hofu yangu ni majina yetu itakuwaje, atakuwa mwaminifu kuficha majina yetu, manake kwenye Mpesa tumesajiri majina yetu halisi. Kwako PJ plz naomba ufafanuzi juu ya hili kabla sijatuma
1. Kama unaona hatari sana jina lako kuwa revealed, basi mpe namba hii AGENT wa Mpesa aitume kwa SAJENTI mbele yako.

2.Sidhani kama interest ya SAJENTI kwa sasa itakuwa ni kunakili majina na IDs za watu...

Naamini ana mambo muhimu mno ya kusimamia baada ya kadhia aliyoipata!...Atakremu majina ya members wangapi?..kwaajili ya kufanyia nini?

Ahsante kwa kuonyesha moyo wa Upendo!
 
Mungu akubariki kwa kujitoa kwako. Na mimi hofu yangu ni majina yetu itakuwaje, atakuwa mwaminifu kuficha majina yetu, manake kwenye Mpesa tumesajiri majina yetu halisi. Kwako PJ plz naomba ufafanuzi juu ya hili kabla sijatuma

ninavyoona hakuna haja ya kujua Ram ndio Abdallah ambalo ndio jina halisi kinachotakiwa ni mchango
 
Mimetupia mchango hapo,,,,, E29KR... Imethibitishwa Tshs 3,000 imetumwa kwa Abd..... tarehe 11/1/12.

Mwambie adelete msg zetu tusije kuvunja kanuni za JF kwa kutoa siri za majina ya members.

Naamini kwa buku tatu yng ukijimlisha na za memba wengine 1000 kati ya wote 59,000 wa JF jamaa atakuwa na pa kuazia kusolve problems. Pia tutamsaidia counselling akihitaji.
Kiongozi,
Mungu akubariki sana!
Kiasi chochote ulichomtolea huyu ndugu yetu kitamfaa sana, maana nia si kumtajirisha, bali kumsaidia kidogo tu aweze kupata hata vocha, au kuandaa mboga ya wanawe, wakati huu ambapo yuko kwenye stress!
Aksante tena!
 
Weka picha za msibani maana siku hizi watu wengi wajasiliamali:

Kwa wanaotokea ubungo kupitia chuo kikuu panda dalax2 za changanyikeni teremkia kituo cha bondeni ( chuo cha takwimu) then ulizia kitongoji cha kizota. Hata wenye usafiri binafsi utaratibu ni huo huo. Tunafanya hitma ya marehemu leo saa 10 alasiri karibuni tujumuike sote. Namba yangu ni 0765 068886.
 
Jamaniii... Pole zake na wanae aisee!
PJ asante kwa initiative mkubwa wangu!
 
hata mimi nimetuma lakini atajuaje kuwa crashwise ndiyo ******** hata kama atayaanika....
Hana jinsi yoyote ya kujua, unless kama mtumaji anaunganisha na text fulani yenye kureveal ID na Jina kwa hiari yake mwenyewe... hizi hofu zingine zinakuwa Above Sea Level!
Mkuu CRASHWISE, Mungu amekuona, na kama ni baraka tayari hapo ulipo unatembea nazo!
 
acheni wasiwasi kwani ukituma huna haja kuandika jina lako unalotumia jf na sidhani kama ana haja ya kufahamu ww ni nani
hata hivo sisi wanajf tuna mutual agreement ya kulindana ingawa haijaandikwa lakini ndio hivo labda kama wapo TISS wana ajenda zao lkn
tunayoandika ni sahihi kabisa.SAJENT mungu azidi kukupa nguvu.
 
Mkuu pakaj nami natuma buku ten muda huu. kufarijiana ni jambo muhumu sana mkuu.
Tayari nimetuma mkuu.
Mamndenyi,
Heshima nyingi kwako!
Faraja ya maneno yafaa sana, lakini wewe umeamua kufanya kwa vitendo, ambavyo vitamgusa mfiwa kwa namna ya pekee!
Nina uhakika 100% kuwa kwa muda huu ameshajihakikishia kuwa hayuko peke yake!...tuko naye!:tea:
 
Hana jinsi yoyote ya kujua, unless kama mtumaji anaunganisha na text fulani yenye kureveal ID na Jina kwa hiari yake mwenyewe... hizi hofu zingine zinakuwa Above Sea Level!
Mkuu CRASHWISE, Mungu amekuona, na kama ni baraka tayari hapo ulipo unatembea nazo!
Ameniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....
 
Ndugu yangu Sajenti
Pole kwa yaliyokusibu.
Tunamwombea sana shemeji yetu apumzike saLAMA.

11th October 2010 11:06

icon1.png
Tarehe 10.10.2010 - Thank you my lovely wife Jackline....
Siku ya jana tarehe 10.10. 2010 mimi na my wife wangu kipenzi Jack tulikuwa tunatimiza miaka 3 ya ndoa yetu.Pamoja na mawimbi ya hapa na pale mungu ametufikisha hapa. What a wonderful wife and mother you are Jack??? Kwa kupitia JF napenda kumwambia mke wangu kwa kweli nakupenda sana wewe na mwanetu Nancy " Kadadaa"..Najua my wife huwa anapita pita humu..

https://www.jamiiforums.com/members/sajenti.html
https://www.jamiiforums.com/members/sajenti.html
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom