mchakachuaji192
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 366
- 68
ndugu za kuna rafiki yangu mmoja (binti) amebahatika kupata mchumba kwa sasahivi binti anasoma chuo kikuu ndio anaingia mwaka wa tatu sasahivi, mchumba wa huyu rafiki yangu sasahivi anataka kwenda nyumbani kwa binti kujitambulisha, ila tatizo linaanzia hapa huyu binti baada ya kuwajulisha wazazi wake wamemwambia binti kuwa ni mapema mno sasahivi kuona binti yao anaolewa maana wao wamedai kuwa wanataka asome akiwa na master (ambayo wazazi wake wanajiandaa kumsomesha akimaliza chuo) na akimaliza ndio aanze kufikiria suala la yeye kuolewa sasa huyu binti yuko njia panda afanyaje ili kulinda uhusiano wake na mpenzi wake na pia kuwaridhisha wazazi pia, ameniomba ushauri mie nimeona nililete hapa jukwaani ili tujadiliane kwa pamoja. Naomba kuwasilisha.