Wana JF Tumeiangusha CHADEMA, tumewaangusha watanzania, tumemsaliti Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF Tumeiangusha CHADEMA, tumewaangusha watanzania, tumemsaliti Dr Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Reyes, Nov 7, 2010.

 1. R

  Reyes Senior Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tathmini yangu fupi ya mwenendo wa uchaguzi inaonesha kuwa kila sehemu ambayo Chadema iliweka mgombea makini, msomi, Kijana na mpiganaji wa ukweli katika Ngazi za Ubunge na Udiwani Chadema iliongoza kwa kura.

  Dr Slaa alipata kura kiduchu sana maeneo ambayo chadema iliweka mgombea dhaifu ngazi ya Ubunge

  Hali ilikuwa mbaya zaidi maeneo ambayo Chadema iliweka wagombea dhaifu wa Ubunge na Udiwani ni kukosa timu sahihi ya kampeni.

  Wagombea Ubunge kama Thomas Nyimbo, Shitambala, Regia nk licha ya uwezo wao lakini katika baadhi ya kata waliangushwa na wagombea wasiouzika na wasiona hoja wa Udiwani.

  Baada ya kutafakari kwa kina nimegundua kuwa sisi wana JF tunahusika kwani wengi wetu tungeweza kujitokeza kwenda kugombea na kuongeza kura kwa Chadema. badala ya kushabikia humu JF

  Ni wakati wa kuamua sasa, Mshawishi na mwenzako tujitokeze. tutengeneze network, tufanye training za stage performance za kutosha, Tuandae wagombea serekali za mitaa na Udiwani kwenye kata zetu ili uchaguzi ujao tuweze kusaidia harakati.

  Suala la kuiangamiza CCM haiwezi kufanya na Mbowe peke yake au Dr Slaa pekee, ni kazi yetu sote hasa vijana

  Hima tuamke, tushikamane, tutambue wajibu wetu kwa Taifa hili

  Mimi nimetangaza nia Isimani Iringa na naanza maandalizi mapemaaaaaa

  2015 peopleeeeeeeezzzzzzzzz
   
 2. m

  mbea Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ili tuungane inabidi Chadema kwanza wajitoe katika sera za udini,ukabila na ujimbo ndio tuanza mapambano ya kweli kuing'oa ccm.
   
 3. R

  Reyes Senior Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ukabila basi chadema chama cha wasukuma maana wamepata wabunge wengi kule na hata myika ni Msukuma

  kama ni Ujimbo Chadema haiwezi kuachana na hiyo sera kwani ndiyo ambayo tunaamini itamkomboa mtanzania

  kama ni Udini sijawahi sikia wala kuona Chadema wakifanya mkutano msikitini au kanisani. Ni bahati mbaya tuu CUF imetawala Zbar na Pwani na kuifanya chadema ishindwe ku penetrate maeneo hayo lakini mkakati kabambe wa kuingia maeneo ya Pwani unaandaliwa

  Acha umbea wewe mtoto
   
 4. m

  mbea Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha wewe bado kinda kimawazo hata kufikiri kidogo washindwa!Kakobe kafunga kanisa siku ya jumapili na aliwaamuru wafuasi wake wakampigie kura Bob Silaa,wakristo wote tanzania tulipewa amri ya kukesha usiku wa kuamkia 31/10/2010 kumuombea bob Silaa aingie Ikulu(inawezekana wewe si miongoni mwetu au huingii kanisani-utatengwa na usharika!,vyama vyote vinavyojiita vya kiraia ambazo nembo zao(logo) zinaherufi ya msalaba + kama Tamwa,TGNP n.k wote walikuwa wakimpigia kapu Bob Silaa,wewe ulikuwa wapi! au ni mmoja wao?

  Unajua jina lako kwetu linamaanisha(Reyes-bushwomen) isije ikawa ni kweli!
   
 5. P

  Pipi New Member

  #5
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi tujipange upya na kwenda vijijini kabisa. Hata hivyo inabidi tujisafishe na ile dhana ya kuonekana tuna chembechembe za udini ambazo CCM inazitumia dhidi ya CUF-Uislamu na CHADEMA-Ukristo.
   
 6. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  No comment jina lako linasadifu unayoongea
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tumeiangusha CHADEMA ni kweli, tumewangusha wa tanzania si kweli


  wayanzania wako juu na wamesimama imara kukataa na kupinga udini na njia yoyote kuwagawa kama chadema kwa kupitia viongozi wake walio wengi wakinadi
   
 8. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kesho nitakuwa kinondoni kuchukua kadi ya CHADEMA. Tutaonana 2015. Damu bado mbichi,
   
 9. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,824
  Trophy Points: 280
  Naanza mikakati ya kugombea udiwani 2015 kata ya Nduli Jimbo la isimani kwa kupitia CHADEMA
   
 10. R

  Reyes Senior Member

  #10
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inabidi tuwasiliane diwani wangu.... asante sana kwa kuitikia wito
   
 11. R

  Reyes Senior Member

  #11
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni muislamu swafiii lakini sijaona chembechembe za udini chadema, nitagombea ubunge isimani iringa ntaona kama chama kitanikataa sababu ya dini yangu.
   
 12. c

  chanai JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi nashangaa sana kusikia hoja za udini na ukabila ndali ya Chadema. Jamani kitu chochote lazima kiwe na mwanzilishi, lazima tukubali hilo. Eti kwa kuwa Chadema kilianzishwa na watu wa kaskazini basi ni chama cha ukabila, nadhani sio sahihi. Kuna wanachama nchi nzima na wengine wameshinda viti vya ubunge na udiwani lakini hawatoki huko. Nafikiri tunahitaji kubadilika na kuachana na mawazo mgando kama haya.

  Nakubaliana na mwanzilishi wa mada hii kuwa tunahitaji kuwa na mikakati ya uhakika katika kujiandaa na changuzi zijazo. Ukisema suala la dini basi tungeweza kusema sisiem ndo ina udini. Angalia kuanzia Z'bar na hata bara raisi na makamu wake wote ni waislamu. Je, tuseme sisiem ina udini? La hasha!! Ninachoamini ni kuwa kiongozi yeyote kuwa na dini yake haimaanishi yeye ni mdini. Hata mimi nina dini yangu, kwa hiyo nikishika uongozi sitegemei kuacha dini yangu. Nafikiri tunahitaji kuwa makini tunapotaka kuzungumzia udini.

  Mimi naanza kutangaza nia kabisa sasa hivi kugombea ubunge Mbinga Magharibi kupitia Chadema. Nitafurahi kushiriki katika mikakati mbali mbali ya kujiandaa ili kuweza kutimiza hazima hiyo.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 13. Y

  YALILA CHIEF Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hvi unajua maana ya udini,ukabila na ujimbo?naamini fikra zako mgango,unaamini usichokiona wala kukijua!tafakari upya,soma mada na hoja mbalimbali ujifunze,mwonesha njia daima amepitia,hao waliokueleza udini,ukabila na ujimbo sio wanachadema,waulize vizuri na urudi upya!
   
 14. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pia kuongezea ni kurudisha akili kwa wale wote ambao wameoshwa akili(brain washed)kwamba pasipo ccm nchi haitakuwa na amani n.k. na hii ifanyike katika ngazi ya vijijini mashuleni na popote pale inapowezekana kwa kukemea maovu ya u ccm.

  Huyo bwana mbea amekuwa sasa biashara ya kuleta mambo ya udini ukabila n.k matokeo ya ubunge yanakuumbua pia kama ni hivyo kesho tutakusikia ukicema nccr ni cha waha, cuf wapemba etc

  Kama jina la mbea halikutoshi ungezea na jina la Mdini (mbaguzi)
   
 15. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kilicho iangusha CHADEMA sio wana JF au wagombea wake wala itikadi za mwelekeo wa chama:nono:

  ila ni nec ya wachakachuaji

  thats it!!!
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  CCM nao wajitoe kwenye sera za ufamilia, uislam, na kutumia watanganyika masikini kupata kura kwani huu uchaguzi umeonesha ccm wanapata kura maeneo ya watu wasio na uelewa tu.
   
 17. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods wa JF naomba watu kama mbea wanaoleta hoja za kipumbavu wafungiwe wanajaza nafasi tu hapa.
   
 18. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mtaji wa ccm umbumbumbu wa watanzania, na
  ndo maana kutoa kwao elemu kunakuwa na mkwamo mkwamo

  ili hali kwa watanzania iendele kuwa hivi:deadhorse:
   
 19. w

  wakushanga JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanatufanya si mapunda
   
 20. C

  CCM Member

  #20
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi mnayo
   
Loading...