Wana JF Tuipe Uzito Habari hii

kaisa079

Member
Nov 16, 2007
20
4
BARUA YA WAZI KWA MKUU WA WILAYA YA TARIME
Ndugu Mhariri,
Sisi ni kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mwera Vision iliyo katika wilaya ya Tarime.
Tunachukua nafasi hii kuipongeza serikali katika juhudi zake za kuhakikisha wasichana hasa kutoka viojijini wanapata elimu.Suala la kustaajabisha ni pale ambapo baadhi ya walimu wasio na maadili mema ya ualimu wanapoamua kutumia nafasi zao ili kukwamisha juhudi za serikali.
Kama ukifuatilia kwa makini kumekuwa na matukia ya mara kwa mara kwa wasichana kupata mimba katika shule yetu hii.Miaka michache iliyopita kilitokea kisa cha mwanafunzi kujifungua chooni ambacho kiliandikwa katika magazeti mengi,
Sisi wasichana wa kike tunaosoma hapa kwa kweli tunaona aibu kwa visa vya aina hii.Ukweli ni kwamba wahusika wakuu wa kuwatia mimba wanafunzi ni walimu wetu.Kama kuna walimu wawili wa kiume(Majina Tunayaifadhi ila wakiendeleza tabia zao tutawataja) wamekuwa wakitusumbua sana sisi wanafunzi wa kike,wanatutongoza mara kwa mara na ukimkatalia ataanza kukupa viadhabu visivyo na msingi na kukuzulia visa vya ajabu ili mradi tu upate shida ya kuishi hapa shule.
Shule hii ni ya binafsi na tulitarajia kuwa kwa kuwa ni shule ya kibiashara maadili ya walimu yangekuwa mazuri ili kuvutia wanafunzi wengi zaidi,lakini imekuwa kinyume.
Mkuu wa wilaya ya Tarime tunakuomba utusaidie kutatua tatizo hili kwani mkuu wa shule amaeonekana kutojali kabisa matatizo haya.
Sisi hapa tumefuata elimu na Ada mwaka huu imepanda sana hivyo hatuko tayari kuharibiwa maisha yetu na walimu wapenda ngono na kupoteza malaki ya ada za wazazi wetu.Tunatarajia kuwa kilio chetu kitasikika.

Ni sisi wanafunzi wa Mwera,Tarime Mara

Habari hii nimeforwadiwa na rafiki yangu mmoja
Kazi kwako mkuu wa wilaya ya Tarime,waokoe hao dada zetu kama malalamiko ya ni ya kweli.Walimu wa aina hii wanatakiwa wafukuzwekazi.
 
nakubaliana nawe mkuu, wanatakiwa wahasiwe na kufukuzwa kazi, wasije peleka ukware wao kwingine! !! teh teh teh
 
Back
Top Bottom