Wana jf nisaidieni elimu ya tanzania imeingia kirusi gani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana jf nisaidieni elimu ya tanzania imeingia kirusi gani!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kibajaj, May 30, 2011.

 1. k

  kibajaj Senior Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaama dakika ishirini zilizopita nilikuwa naendesha usahili kwa vijana ambao wamemeliza vyuo vikuu amini usiamini kati ya vijana hao kumi walishindwa kabisa kufanya conversation ya kingereza japo kwa dakika mbili.

  Baba yangu ameishia la nne lakini anaongea kingereza standard na kinachoeleweka ila vijana hawa wana utasikia its likee..... its like..... yani ...... i mean......what am trying to say is?

  Ika yaani anababaika mpaka anatia huruma, ni kwamba siku hizi hawafundishwi kingereza shuleni au ndo mkakati wa kufanya kiswahili lugha ya kimataifa umeanza?

  Au basi elimu wanaiacha darasani wanatoka na vyeti?

  Tatizo liko wapi jamani?

  Au wizara ndo imekosa sera kiasi hiki?
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Unadhani wachina wanaweza kuzungumza kingereza.wewe badala ya kuangalia weledi unaangalia lugha.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  elimu ya Tanzania au elimu ya watu uliowahoji? Mkuu nipe nafasi ya kazi uone wengine tulivyo fit. Tatizo ni kazi za kupeana,Tangaza kazi kihalali uone vichwa vilivyo mtaani. Cha ajabu hata ukiuliza hao unaowafanyia usahili kazi zimetangazwa lini na wapi waweza kukosa jibu!
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  mlichokuwa mnaangalia ni uelewa wa hao uliowainterview wa kazi wanayoiombea au ni kiingereza chao na je kiingereza kilikuwa ni moja ya qualification za kuomba kazi katika kampuni yako na je wanaenda kufanya kazi ya kuongea kiingerez aau taaluma yao
   
 5. T

  The Priest JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inategemea na nafasi wanayoomba,huwezi kuajiri position zngne bila kuangalia uwezo wa mtu kwny lugha,na pia uwezo wa mtu kujieleza na kujiamini ni kipimo kizuri cha ueledi wa mtu..
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jibu hoja za kipindupindu, Gsana na Mr. rocky ili nione upeo wako kuhusu issues.
   
 7. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hio ndio hali halisi ya vijana wanaomaliza vyuo wengi wao wanaangalia mechi za Barcelona, Tv soaps za ITV, Bongoflava kwa sana na Leo tena ya Clouds. Unadhani kweli wataeza ku communicate kwa kiingereza? English mpaka uijue inahitaji self initiatives usome sana vitabu,magazeti na literature mbalimbali ndio utaijua vizuri lugha.

  Tukubali tukatae Kiingereza graduaates wetu wengi kinawapiga chenga. Niliwahi kuhudhuria interview moja hapa Country Office ya WOrld Bank aliingia kijana ana Post graduate ya Finance lakini kujieleza kiingereza alichemka mbaya na ilimfanya akakosa kazi .

  Vijana jitahidini kusoma vitabu na magazeti mbalimbali ili muongeze ufahamu wa kujua english.

  Hii inadhihirika hata kwenye mashindano kama Zain Inter- Universities Africa Challenge.

  Tanzania tulikuwa hatufiki mbali kwani hatuna utamaduni wa kujisomea makala mbalimbali na European History.
   
 8. k

  kibajaj Senior Member

  #8
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu kazi imetangazwa sana tu na siyo kama nimekurupuka,ivyo we ulitaka turicruit project manager ambaye hata kujieleza hawezi? acha kulea ujinga. ila sishangai kwa kauli zako manake suala la kingereza lishaletaga ugomvi bungeni.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe may be tungejua ni position gani anazungumzia tungeweza kumwelewesha zaidi au tuone mapngufu ya hao vijana sio kuwahukumu moja kwa moja
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mi silei ujinga wala sijakuambia ukamuajiri mtu ambaye hana uelewa wa lugha kuwa Project Manager wenu. Suala nililolizungumzia hapo ni ile ufahamu wa lugha wa jumla maana kila kazi inategemea zaidi uzoefu wa mtu na kama haihitaji matumizi ya lugha sana tthe way unavyotaka wewe watu wakuelewe.
   
 11. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,897
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Hapo sijakupata......ulikuwa unawapima uelewa wa lugha au uwezo wa kufanya kazi kitaaluma??????.......Du initisha maana kama mtu kujua kitu lazima akiongee kwa kiingereza.......basi ukienda uingereza na ukakutana na mtoto wa miaka saba anaongea kiingereza unaweza ukampa ajira kwa sababu tu anajua kiingereza vizuri.........
  Mkulu kiingereza ni lugha tu na si taaluma......kama ni hivyo basi Mourinho asingepata kazi ya ukocha Uingereza.....au wachina wasingeendelea mpaka pale walipo sasa........mkulu try to wash out colonial mentality.....
   
 12. k

  kibajaj Senior Member

  #12
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu weledi ambao mtu hawezi kujieleza? Alaf kakudnganya nani wachina hawajui kingereza? ebu nenda star times apo tbc then ufike beidjin uone.
   
 13. k

  kibajaj Senior Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivyo ata kama kazi niya uelewa maelezo yakitolewa kingereza ataelewa nini sasa?
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280

  Mkuu kwa uelewa wa jamaa kujua kuongeaa kiingereza vizuri ni kipimo tosha cha kupata kazi bila hata kuangalia uelewa au uzoefu wa kazi wa wahusika na sijui kama hiyo kazi ya Project Manager atakuwa anafanya na wazungu pekee ambapo hatawasiliana na watu wa kawaida wa vijijini ambako hata hiyo lugha hataitumia kwa wale watu wa kawaida wa kijijini ambao hata kiswahili ni ndoto.
   
 15. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mkuu umesema kwel kaz za sku hizi full kujuana ndo sabab vilaz wanapachikwa kwenye nafas muhim and then wanashindwa kutimiza wajib coz up stares hamna kitu kisa baba ni katib mkuu bas anapachikwa serikalini....mtaani wamejaa watu fit sana tatzo ni watoto wa wakulima ndo sabab hutawaona kwenye hzo interview za kupeana.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  So kipimo chako cha kujua huyu mtu anajua au anaiweza kazi yake ni flow ya english na sio utendaji wake wa kazi . So kama mimi nikija naflow english na nina vyeti vyangu viko vizuri ila kichwani sina utaalamu wowote wala uzoefu wa kazi mtanikubali
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Unashagaa hilo mkuu . Mie nimeona watu kadhaa wana defend PhD zao ni uharo kabisa na aibu lakini nawaona siku hizi ndiyo wa kwanza kuandika na kutaka waitwe Drs .Wako pia wengi wana degree moja wengi tu hawawezi kutengeneza CV yao wenyewe .Ndiyo shida hii kaka elimu zao hizi sijui inakuwaje
   
 18. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #18
  May 30, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo, unaona bora babayako aliyeishia darasa la 4 kuliko kijana aliyehitimu chuo kikuu sasa?
   
 19. J

  Juma. W Senior Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna njia mbili tu za kuweza kujua kama mtu anaweza fanya kazi fulani; 1. Kumuuliza aeleze ataifanya vipi na 2. Kumpa kazi aifanye. Mara nyingi kwenye usaili tunatumia njia ya kwanza yaani "mtu ajieleze/auze skills zake". Mara zote kwa wahitimu wa elimu ya juu kiingereza hutumika kama lugha ya usaili. Kuna sababu mbalimbali zilizochangia kutumika kwa hii lugha katika usaili.

  Kwa kweli ni kama mtu hawezi kujieleza inakuwa ngumu kufanhamu anajua kiasi gani. Bila kujieleza utajuaje kuwa mtu anajua anachokiomba? Mtu amaomba kazi ya ualimu, uhasibu, uhakimu, n.k lazima aeleze kwa maneno jinzi atakavyofanya kazi. Tukumbuke pia kuwa hawa watu wataongea na watu tena toka sehemu mbalimbali duniani. Je akishapata ajira itakuweje? Itakuwa kama yule jamaa yetu moja ambae kamaliza shule na kupata ajira lakini akiona mzungu anakuja ofisini anaaga.

  Hii ni "changamoto". Binafsi sioni sababu za kukataa ukweli.Tukubali; kuukubali udhaifu ni kitu muhimu sana katika kutatua tatizo. Tukishaukubali udhaifu wetu tujadili/tuamue tubadilike vipi? Vinginevyo tuendelee kutegemea kazi za deiwaka.
   
 20. k

  kibajaj Senior Member

  #20
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haswaaa manake na darasa lake la nne anaweza kujieleza na pia anaweza kukuandiakia kwa kingereza fasaha fasaha actiona plan na strategic plan zake siyo hawa unaowatetea.
   
Loading...