Wana JF, Naomba Tumjibu Mhariri wa HabariLEO, Kwani Anauliza; KWA VITISHO HIVI...

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Ifuatayo ni tahariri yake ya 8/10/07:

Kwa vitisho hivi tunaipeleka wapi nchi yetu?

Mhariri
HabariLeo;
Monday,October 08, 2007

KATIKA siku za karibuni nchi imegubikwa na mjadala wa madai ya ufisadi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa serikalini, utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi na hasa kauli mbiu iliyoiweka serikali ya sasa madarakani ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania.

Mjadala huu unaelekea kuchukua sura tofauti kila siku ziendavyo mbele na sasa umefikia hatua ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kutishia mgomo wa nchi nzima kama njia mojawapo ya kuishinikiza serikali kuharakisha uchunguzi wa tuhuma hizo walizozianzisha wao wenyewe.

Hoja inayotolewa hapa ni kwamba mgomo huo hauepukiki hadi hapo rais atakapounda Tume huru ya kuchunguza madai ya ufisadi kuhusiana na mkataba wa uchimbaji dhahabu wa Buzwagi na kwamba kampuni kadhaa hewa ziliundwa na kupewa fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambazo zilitumika kufadhili uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa kuwa kumeibuka madai mapya na mazito na kuna tishio la kuitisha mgomo wa nchi nzima hatudhani kama itakuwa busara kukaa kimya na kujifanya hatuoni linaloendelea.

Ikumbukwe kwamba mgomo wa nchi nzima si suala la mzaha au porojo za jukwaani kama ambavyo inaelekea kufanywa na wanasiasa waliozungumza jana. Mgomo wa nchi nzima maana yake ni kuweka rehani usalama na maisha ya watu wote waishio humo. Imetokea sehemu nyingine migomo ya aina hiyo huishia kwa vurugu nchi nzima, umwagaji damu na hata kusababisha kutangazwa kwa hali ya hatari.

Hatudhani hayo ndiyo waandaaji wa mgomo huo ndiyo wanayotutakia. Kama sivyo wafute haraka tishio lao na wachukue mkondo unaostahili katika kuwasilisha madai yao.

Na kwa kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala bora inayotumika kwingineko duniani, maadamu waandaaji wa mgomo huo wanadai wana ushahidi wa tuhuma kadhaa walizozitoa, ni vyema wakazipeleka Polisi au Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na baadaye Mahakamani ili haki itendeke.

Hivi kama kwa kila tuhuma utaitishwa mgomo wa nchi nzima nchi yetu itasonga mbele au itarudi nyuma? Jibu la swali hilo ni bayana.

Tunatambua kwamba kiu ya wengi wetu ni kutekelezeka kwa kasi ya ajabu kwa ahadi ya Maisha Bora kwa Watanzania wote na hakuna shaka tumeshuhudia jitihada za kutuwezesha kutimiza ndoto hiyo kama zilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka huu japo baadhi wanajifanya hawazioni wala kuzisikia.

Hata hivyo hiyo si sababu ya kuitumbukiza nchi katika dimbwi la maisha hatari kwa wote kwa njia ya mgomo.


Source: HabariLEO.

MAJIBU YANGU KATIKA VIPENGELE KADHAA HAPO JUU:

Ikumbukwe kwamba mgomo wa nchi nzima si suala la mzaha au porojo za jukwaani kama ambavyo inaelekea kufanywa na wanasiasa waliozungumza jana. Mgomo wa nchi nzima maana yake ni kuweka rehani usalama na maisha ya watu wote waishio humo. Imetokea sehemu nyingine migomo ya aina hiyo huishia kwa vurugu nchi nzima, umwagaji damu na hata kusababisha kutangazwa kwa hali ya hatari.
Maisha ya wananchi Tanzania yamewekwa rehani kwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru; kila mwaka kuna ahadi za hili na lile katika vikao vya bajeti na makongamano mengineyo ya siasa na kiuchumi lakini hakuna lililotendeka la kusema maisha ya Watanzania yako huru kutoka katika utegemezi wa misaada na ufisadi wa wachache ambao pamoja na ushahidi wote wanapopatikana kuwa na hatia hawawajibishwi.

wachukue mkondo unaostahili katika kuwasilisha madai yao.
Mkondo upi huo?...wapinzani wakati wako bungeni kuongelea Buzwagi wengine wameitwa waongo hata kufikia kufungiwa kushiriki vikao vya bunge. Katika kutoa hoja, CCM ambayo ndiyo chama tawala na yenye wabunge wengi zaidi, wabunge wake wameishia kuunga mkono hoja ya kumzuia Mh. Zitto kushiriki vikao vya bunge, bila kujali hili wala lile bali ushabiki wa kisiasa na kivyama tu, hapa bunge kama mkondo wa kuwasilisha madai ulipuuziwa na majority ya CCM MPs.

Na kwa kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala bora inayotumika kwingineko duniani.
Hapa ningependa kukubaliana nawe,lakini nakupinga kwani sehemu nyingine nyingi ambazo kuna utawala bora, shutuma kama hizo za Buzwagi au BoT zinapotokea, mawaziri au viongozi husika hujiuzuru mara moja, au kukaa pembeni wakati uchunguzi unaendelea. Lakini katika nchi yetu huu utawala bora umekaa kivyake vyake tu, Mh. Balali bado analipwa na anaendelea kuwa Gavana wakati serikali imekubali kuwa kuna hitilafu na mapungufu katika hizo account na hivyo imealika kampuni za kigeni kufanya uchunguzi. Kuhusu Mh. Karamagi, naye pia ili kuonyesha utawala bora angelitakiwa ajiuzulu mara moja; Ndg. Mhariri, hebu angalia utawala bora katika nchi unazotaka ziwe mfano; sema Japani hivi... umesikia jinsi watu wanvyojiuzulu?!.... huo si ndiyo utawala bora?...au unamaanisha nini haswa? Kwangu miye, utawala bora ni kuwajibika na kukubali kuwajibishwa.
Hivi kama kwa kila tuhuma utaitishwa mgomo wa nchi nzima nchi yetu itasonga mbele au itarudi nyuma? Jibu la swali hilo ni bayana.
Hivi sasa mimi naona ni vitisho vyako. Na jibu la swali lako ni bayana kuwa viongozi wabadhirifu na mafisadi wakijua kuwa wanaweza kuwajibishwa pale tuhuma zinapotokea na kuwa na vithibitisho bayana kuwa wameshiriki, migomo kama hiyo inayokusudiwa haitakuwepo tena kwani wasipowajibishwa na serikali na vyombo vyake vya sheria kama ilivyo sasa basi Watanzania watagoma! Your question is hypothetical ain't it?! The answer to that is BAYANA.

Hata hivyo hiyo si sababu ya kuitumbukiza nchi katika dimbwi la maisha hatari kwa wote kwa njia ya mgomo.
You seem so content with your current lifestyle, well, my mom ain't, my cousins ain't, my brothers and sisters ain't, and you know what? WATANZANIA WALIO WENGI ain't either! Budget support almost 50% - how long for? Upcountry journeys -Tanzanians are forced to travel through Kenya to reach lake zones... and so forth, how long for? Maisha ya walio wengi katika nchi yetu tayari yako katika hatari. Wananchi wanakufa wanyonge katika roho zao, wananchi wako kimya kutokana na unyonge wa unfulfilled promises, etc. Lakini ninaposoma kauli yako hii ninacho ona ni kuwa wewe umeridhika na hutaki wenzako wawe hivyo, as long as kuna amani inayotokana na maisha duni basi unataka a sticky status quo to the detriment of Tanzanians at large!


SteveD.
 
SteveD
That is good observertion. Article kama hizi nimekuwa nazitegemea sana kwenye kipindi hiki ambapo serikali inabanwa. Serikali ikiboronga huwa kunakuwa na media campaign ya kuwa-brainwash watu kuonesha kuwa mass action ni hasara. Anavyosema kuwa nchi itaingia kwenye matatizo, ina maana kuwa haoni nchi iko kwenye matatizo, na hayo ni mawazo finyu sana kwa mwandishi wa habari. Unless asiwe mtanzania anayejua hali halisi ya Tanzania na watanzania, au awe ni mmoja ya wanaopokea bahasha za laki tatu halafu anatarajiwa kulipa fadhila. Sio jambo la ajabu kuona waandishi wa habari walionunuliwa.
 
SteveD
That is good observertion. Article kama hizi nimekuwa nazitegemea sana kwenye kipindi hiki ambapo serikali inabanwa. Serikali ikiboronga huwa kunakuwa na media campaign ya kuwa-brainwash watu kuonesha kuwa mass action ni hasara. Anavyosema kuwa nchi itaingia kwenye matatizo, ina maana kuwa haoni nchi iko kwenye matatizo, na hayo ni mawazo finyu sana kwa mwandishi wa habari. Unless asiwe mtanzania anayejua hali halisi ya Tanzania na watanzania, au awe ni mmoja ya wanaopokea bahasha za laki tatu halafu anatarajiwa kulipa fadhila. Sio jambo la ajabu kuona waandishi wa habari walionunuliwa.

Bongolander, Haswaa..
Tanzania yetu inahitaji kubadilika na cha kutia moyo mabadiliko haya (haswa ya kifikra) yanaanza kuonekana (angalau kiduchu), through medium kama hizi. Inakera tu kuona Mwanataaluma katika uandishi kama huyu mhariri anaandika kitu kama hicho, angekuwa balanced kidogo nisingempinga sana, ila anaulekeo mmoja tu, nao ni kuweka vitisho indirectly kwa wasomaji.

Sasa watu kama mimi na wewe ambawo taaluma zetu siyo uandishi tunapoweza kuona yale anayo dhamiria, je wanataaluma wenzake wataona yapi?! These guys need to appreciate the fact that Tanzanians are now awakening and becoming reactive to scandalous and disgraceful acts that have engulfed our society far too long.

SteveD.
 
NI kweli tatizo kubwa ni kwamba tunasahau kuwa waandishi wa habari ndio wanatakiwa kuwa kama kioo chetu, lakini siku hizo mambo yanakwenda sana ovyo. Ukiangalia magazeti ya Mwananchi, majira (except for this day and other few) utaona ni upuuzi tu. Nadhani rushwa sio kina Karamagi tu au kina Balali tu. Waandishi wa habari tuliokuwa tunawaita waandamizi kama kina Salva wameprove kuwa useless kabisa, nadhani nao wanatakiwa kushikiwa mabango wafanye kazi yao vizuri, wasitulishe upuuzi.
 
yote ni sehemu ya mapambano ya kifikra.. wao bado wanaamini wakiwatishia wananchi kuwa wapinzani wanataka kuleta umwagaji damu na machafuko nchini basi hoja zao zitakuwa na nguvu zaidi!!
 
MAHAKAMA, POLISI, PCCB, BUNGE NANI ANA IMANI NAVYO, huyu jamaa haoni watu wanachukua sheria mkononi kuangamiza waharifu. suala lililobaki ni wananchi kuwahukumu viongozi wao kama wanavyofanya kwa wezi.
 
Na kwa kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala bora inayotumika kwingineko duniani

Hivi ndio visingizio vinavyotuletea matatizo, hawa viongozi wanatumia haya maneno ya utawala bora, amani na utulivu katika kuhujumu taifa letu. Utasemaje utawala bora wakati kama kiongozi unagawa mali za nchi bure? Huu ndio utawala bora?
 
ni zile zile mbinu wanazoendelea kutumia wakati wa kampeni, ati ukiwafata wapinzani kutakuwa na vita na umwagaji damu, wakitoa mifano ya rwanda na burundi.

hapa anaetishwa ni mtanzania wa kijijini, ambae anaiamini serikali kama chombo cha kumlinda, na amekuwa akiambiwa mara kadha wa kadha kuwa upinzani ni hatari.

mtanzania huyu hajui kuwa upinzani ni moja ya sehemu ya taifa la tanzania, ambao unakubalika kikatiba, ambao upo kwa ajili ya kutetea haki yake.
 
tusimsahaumkurugenzi wa habari wa ikulu bwn Salva alinyojikanganya leo asubuhi akihojiwa na viky mtetema wa bbc kuhusu kashfa za ufisadi.Akidai kuwa nchi inaendeshwa na sheria nzuri na hizo ni shutuma ni uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu nayeye ana imani kuwa wananchi wanaipenda na wataendelea kuipenda CCM ndio maana kikwete aliibuka na 80% I felt like laughing and crying at the same time.
 
Mwaka 1995 vyombo kadhaa vya habari vilitumika kuhadaa wananchi kwa kutumia picha za matukio ya Rwanda 1994 kama silaha ya CCM dhidi ya kukabiliana na mabadiliko na kuwafanya waamini ya kuwa yaliyotokea Rwanda yatatokea hapa ikiwa CCM itaondolewa madarakani.Uzushi wa hali ya juu. HAWATAWEZA TENA.

Watanzania wa sasa sio wale wa miaka ile,propaganda za kijinga hakuna atakaye azikubali tena. Kama nchi itaingia katika machafuko wa kulaumiwa ni Viongozi walioko madarakani kwani wao ndio wasiotaka SULUHU na wananchi waliowaweka madarakani.

Hawa vibaraka nao wanaotumia vyombo vyao vya habari kupotosha ukweli sababu ya 'vibahasha'hukumu yao yaja,hawana tofauti yeyote na mafisadi wenyewe,maana wanawabeba kwa kalamu zao kwa gharama ya damu ya walala hoi walio wengi.
 
inawezekana hawa waandishi wa habari wana elimu yakutosha. ila ninadhani haitoshi kwa uandishi wa habari.

ukiangalia articles zao zinatisha. sio za kina. ni za umbea na usuda.

ni wale wale waliosadikiwa kupokea book kumi kumi hapo mbeya na katibu wa wasira ili wasiandike kilichojiri. bila sisi kupiga kelele yawezekana wasingejaribu. hata yale waliyoyaandika tunaona yalikuwa shallow sana kulingana na hari halisi ilivyokuwan na kutoweka hata picha yoyote.

ni wale wale walioshtumiwa na bunge tukufu kuwa elimu yao haitoshi, hivyo waende wakasome zaidi.

samahani kama kuna waandishi wa habari niliowaudhi, ila samaki mmoja akioza, wote wameoza, mnaonaje tukiungana na bunge kuwataka wakasome tena, mana wanadharirisha profession zao.
 
Mwenye Njaa Hana Miiko,mwenye Shibe Hamtambui Mwenye Njaa, Ogopa Sana Mtu Aliyekata Tamaa Ya Maisha!!!!

Hawa Jamaa Nawaita Wajinga Kwani Wanafikiri Mtz Wa 1995 Ni Yule Wa 2010. Km Walimchagua Jk Kwa 80% Wategemee Anaendelea Kupendwa Wanajidanganya. Mimi Mwenyewe Nilimpigia, Mungu Anisamehe Kwa Kuuweka Huu Utawala Mbovu Madarakani.

Jk Endelea Kuwavuta Maswahiba Wako Ikulu Siku Moja Watakutokea Puani.

Angalia Dhamana Uliyopewa Na Watz 35m, Sio Kikundi Kidogo Cha Mtandao. Mtandao Wako Umesababisha Mpasuko Ndani Ya Sisiem Na Sasa Mpasuko Unahamia Kwenye Nchi. Lakini Ndo Bado Unawasogeza Wanamtandao Wako Kwenye Nyumba Nyeupe. Please Bro, Take Action To Save The Nation And Its People.

Vitu Ambavyo Havikuwezekana Hata Mwaka Mmoja Uliopita,sasa Vinafanyika. Ulitegemea Mwananchi Angechoma Kituo Cha Polisi Au Kumtimua Dc Wako Na Mawe. Hakuna Imani. Baadae Watakugeukia Wewe.

Salva, Chunga Kauli Zako Na Uelewe Siku Moja Utakuja Kujibu Mbele Ya Hivyo Vyombo Vya Dola Ambavyo Hatuna Imani Navyo Sasa.
 
Salva, Chunga Kauli Zako Na Uelewe Siku Moja Utakuja Kujibu Mbele Ya Hivyo Vyombo Vya Dola Ambavyo Hatuna Imani Navyo Sasa.

Eti si kuna wakati nilisikia kuwa huyu ni mwandishi makini sana na ataleta mabadiliko Ikulu?
 
Waogopeni Sana Watu Wapole, Ndio Watz Ni Wapole, Wavumilivu Na Wenye Subira. Uvumilivu Unakwisha, Subira Inatoweka Na Sasa Wanakuwa Wakali Kwani Wamegeuzwa Kuwa Madaraja Ya Wajanja Wachache Huku Wakibaki Maskini.

Huwa Naogopa Sana Nikiona Vijana Mitaani Wakiwa Hawana Kazi Za Kufanya. Kundi La Watotowalio Shule Za Msingi Na Sec. Tutawaweka Wapi Hawa? Rasilimali Zinatoweka Na Zingine Kuwa Mikoni Mwa Wachahe. Siku Moja Bomu Litalipuka, Nyie Endeleeni Tu Kupuuza Madai Ya Wananchi Na Kudai Wapinzani Hawana Sera.

Amani Ya Nchi Hii Iko Rehani, Kwani Hakuna Amani Penye Njaa. Njaa Huondoa Subira, Uvumilivu Na Upole.

Mmekalia Siasa Tu Badala Ya Kuchapa Kazi, Mnahatari Ninyi!!

Anyway Tukisema Mnasema Hawa Ni Wapinzani, Mi Napinga Nikiwa Ndani Ya Sisiem, Kimeoza.

Sisiem Sio Baba Wala Mama Na Wala Haina Haki Ya Kutawala Nchi Hii Milele.
 
Mwandishi Makini Kabla Hajageukia Kwenye Mtandao, Baadae Alipoingia Kwenye Mtandao Rai, Mtz Yote Kwisha. Na Sasa Kaenda Nyumba Nyeupe Kumalizia Kazi. There Is A Syndicate Here, Lets Wake Up Guys To Protect Our Country, Resources And People.
 
Huyu Mhariri lazima aitetee serikali maana ndio mwajiri wake. Lakini anasahau kwamba sasa Watanzania tumechoshwa na hawa Plat Form Policy makers. Mgomo ni njia muaafaka ya kuwabana watawala hamna njia nyingine, ikibibidi few should die for the sake of the Nation. Hamna anayeogopa risasi mpaka kieleweke!!!!!
 
I am not suprised! what else could we expect from mhariri wa habari leo? he is just like them, he is one of them, but he is forgetting that wa TZ washaamka zamani.fISADI LAZIMA AWATETEE MAFISADI WENZIE JAPO kuna uwezekano jamaa ni maskini kama most of Tanzania lakini karidhika na hali yake na ana enjoy vibuku ten anavyopewa ili aendelee kutetea ujinga. Si kosa lake, his mind is polluted already.
 
Hamna anyeogopa risasi mpaka kieleweke !!!!...
Sentensi kama hizi mimi zinaniogopesha sana na sasa zimeenea midomoni mwa watu kuliko wakati mwingine wowote labda kwenye vita ya Majimaji. Sasa mbona hawa wakubwa hawashtuki wakati wao na familia zao ndio watakuwa kwenye target?Usingizi gani huo?
 
Sentensi kama hizi mimi zinaniogopesha sana na sasa zimeenea midomoni mwa watu kuliko wakati mwingine wowote labda kwenye vita ya Majimaji. Sasa mbona hawa wakubwa hawashtuki wakati wao na familia zao ndio watakuwa kwenye target?Usingizi gani huo?

Wataogopa wapi wakati kwa wao ni easy kuondoa familia zao right away kuzipeleka nje kwa pesa walizokwisha kutuibia? I hate them.
 
Kosa lingine,

Kitendo cha gazeti la serikali kukurupukia hoja hii kinaonyesha kuwa ni wazi wanaogopa sana uwezekano wa mgomo huo lakini vilevile kinatoa mwanya kwa watanzania kufikiria zaidi umuhimu na uwekano wa kutekelezwa mgomo huo. Zaidi kunawaambia waandishi waandike na kuichambua zaidi hoja hiyo hivyo kuipa umaarufu.

Kazi kwelikweli..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom