Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,270
Ifuatayo ni tahariri yake ya 8/10/07:
Kwa vitisho hivi tunaipeleka wapi nchi yetu?
Mhariri
HabariLeo;
Monday,October 08, 2007
KATIKA siku za karibuni nchi imegubikwa na mjadala wa madai ya ufisadi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa serikalini, utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi na hasa kauli mbiu iliyoiweka serikali ya sasa madarakani ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania.
Mjadala huu unaelekea kuchukua sura tofauti kila siku ziendavyo mbele na sasa umefikia hatua ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kutishia mgomo wa nchi nzima kama njia mojawapo ya kuishinikiza serikali kuharakisha uchunguzi wa tuhuma hizo walizozianzisha wao wenyewe.
Hoja inayotolewa hapa ni kwamba mgomo huo hauepukiki hadi hapo rais atakapounda Tume huru ya kuchunguza madai ya ufisadi kuhusiana na mkataba wa uchimbaji dhahabu wa Buzwagi na kwamba kampuni kadhaa hewa ziliundwa na kupewa fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambazo zilitumika kufadhili uchaguzi mkuu uliopita.
Kwa kuwa kumeibuka madai mapya na mazito na kuna tishio la kuitisha mgomo wa nchi nzima hatudhani kama itakuwa busara kukaa kimya na kujifanya hatuoni linaloendelea.
Ikumbukwe kwamba mgomo wa nchi nzima si suala la mzaha au porojo za jukwaani kama ambavyo inaelekea kufanywa na wanasiasa waliozungumza jana. Mgomo wa nchi nzima maana yake ni kuweka rehani usalama na maisha ya watu wote waishio humo. Imetokea sehemu nyingine migomo ya aina hiyo huishia kwa vurugu nchi nzima, umwagaji damu na hata kusababisha kutangazwa kwa hali ya hatari.
Hatudhani hayo ndiyo waandaaji wa mgomo huo ndiyo wanayotutakia. Kama sivyo wafute haraka tishio lao na wachukue mkondo unaostahili katika kuwasilisha madai yao.
Na kwa kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala bora inayotumika kwingineko duniani, maadamu waandaaji wa mgomo huo wanadai wana ushahidi wa tuhuma kadhaa walizozitoa, ni vyema wakazipeleka Polisi au Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na baadaye Mahakamani ili haki itendeke.
Hivi kama kwa kila tuhuma utaitishwa mgomo wa nchi nzima nchi yetu itasonga mbele au itarudi nyuma? Jibu la swali hilo ni bayana.
Tunatambua kwamba kiu ya wengi wetu ni kutekelezeka kwa kasi ya ajabu kwa ahadi ya Maisha Bora kwa Watanzania wote na hakuna shaka tumeshuhudia jitihada za kutuwezesha kutimiza ndoto hiyo kama zilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka huu japo baadhi wanajifanya hawazioni wala kuzisikia.
Hata hivyo hiyo si sababu ya kuitumbukiza nchi katika dimbwi la maisha hatari kwa wote kwa njia ya mgomo.
Source: HabariLEO.
MAJIBU YANGU KATIKA VIPENGELE KADHAA HAPO JUU:
SteveD.

Maisha ya wananchi Tanzania yamewekwa rehani kwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru; kila mwaka kuna ahadi za hili na lile katika vikao vya bajeti na makongamano mengineyo ya siasa na kiuchumi lakini hakuna lililotendeka la kusema maisha ya Watanzania yako huru kutoka katika utegemezi wa misaada na ufisadi wa wachache ambao pamoja na ushahidi wote wanapopatikana kuwa na hatia hawawajibishwi.Ikumbukwe kwamba mgomo wa nchi nzima si suala la mzaha au porojo za jukwaani kama ambavyo inaelekea kufanywa na wanasiasa waliozungumza jana. Mgomo wa nchi nzima maana yake ni kuweka rehani usalama na maisha ya watu wote waishio humo. Imetokea sehemu nyingine migomo ya aina hiyo huishia kwa vurugu nchi nzima, umwagaji damu na hata kusababisha kutangazwa kwa hali ya hatari.
Mkondo upi huo?...wapinzani wakati wako bungeni kuongelea Buzwagi wengine wameitwa waongo hata kufikia kufungiwa kushiriki vikao vya bunge. Katika kutoa hoja, CCM ambayo ndiyo chama tawala na yenye wabunge wengi zaidi, wabunge wake wameishia kuunga mkono hoja ya kumzuia Mh. Zitto kushiriki vikao vya bunge, bila kujali hili wala lile bali ushabiki wa kisiasa na kivyama tu, hapa bunge kama mkondo wa kuwasilisha madai ulipuuziwa na majority ya CCM MPs.wachukue mkondo unaostahili katika kuwasilisha madai yao.
Hapa ningependa kukubaliana nawe,lakini nakupinga kwani sehemu nyingine nyingi ambazo kuna utawala bora, shutuma kama hizo za Buzwagi au BoT zinapotokea, mawaziri au viongozi husika hujiuzuru mara moja, au kukaa pembeni wakati uchunguzi unaendelea. Lakini katika nchi yetu huu utawala bora umekaa kivyake vyake tu, Mh. Balali bado analipwa na anaendelea kuwa Gavana wakati serikali imekubali kuwa kuna hitilafu na mapungufu katika hizo account na hivyo imealika kampuni za kigeni kufanya uchunguzi. Kuhusu Mh. Karamagi, naye pia ili kuonyesha utawala bora angelitakiwa ajiuzulu mara moja; Ndg. Mhariri, hebu angalia utawala bora katika nchi unazotaka ziwe mfano; sema Japani hivi... umesikia jinsi watu wanvyojiuzulu?!.... huo si ndiyo utawala bora?...au unamaanisha nini haswa? Kwangu miye, utawala bora ni kuwajibika na kukubali kuwajibishwa.Na kwa kuwa nchi yetu inatawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala bora inayotumika kwingineko duniani.
Hivi sasa mimi naona ni vitisho vyako. Na jibu la swali lako ni bayana kuwa viongozi wabadhirifu na mafisadi wakijua kuwa wanaweza kuwajibishwa pale tuhuma zinapotokea na kuwa na vithibitisho bayana kuwa wameshiriki, migomo kama hiyo inayokusudiwa haitakuwepo tena kwani wasipowajibishwa na serikali na vyombo vyake vya sheria kama ilivyo sasa basi Watanzania watagoma! Your question is hypothetical ain't it?! The answer to that is BAYANA.Hivi kama kwa kila tuhuma utaitishwa mgomo wa nchi nzima nchi yetu itasonga mbele au itarudi nyuma? Jibu la swali hilo ni bayana.
You seem so content with your current lifestyle, well, my mom ain't, my cousins ain't, my brothers and sisters ain't, and you know what? WATANZANIA WALIO WENGI ain't either! Budget support almost 50% - how long for? Upcountry journeys -Tanzanians are forced to travel through Kenya to reach lake zones... and so forth, how long for? Maisha ya walio wengi katika nchi yetu tayari yako katika hatari. Wananchi wanakufa wanyonge katika roho zao, wananchi wako kimya kutokana na unyonge wa unfulfilled promises, etc. Lakini ninaposoma kauli yako hii ninacho ona ni kuwa wewe umeridhika na hutaki wenzako wawe hivyo, as long as kuna amani inayotokana na maisha duni basi unataka a sticky status quo to the detriment of Tanzanians at large!Hata hivyo hiyo si sababu ya kuitumbukiza nchi katika dimbwi la maisha hatari kwa wote kwa njia ya mgomo.
SteveD.