Wana JF naomba msaada wa daktari mzuri wa wajawazito

Mikhail Tal

JF-Expert Member
May 12, 2016
377
672
Mchumba wangu ana ujauzito ndo upo kwenye trimester ya kwanza ila amekuwa analalamika kupatwa na hizi shida
- Tumbo kuwaka moto
- Vichomi
- Mdomo unakuwa mchungu
- Halafu analalamika kichwa pia huwa kinakuwa kinamuuma
- Analalamika pia kwamba kwamba akila chakula anakaa mda mfupi na kutaka kula tena .. yaani ni kama akila chakula kinapotea.

Nimekuja hapa kuomba msaada ki ukweli maana nimeshazunguka vituo vya afya sasa kama vitatu ila bado sijakutana na daktar wa kutoa ushauri na matibabu ya kueleweka. Wengi wanaishia kusema hiyo ni kawaida tu 'unywe maji mengi' na 'mboga mboga' ila sasa naona shida imekuwa ni ile ile tu hamna hata nafuu.

Nitashukuru kama ntapata msaada wenu, mimi nipo Dar es salaam so ningependa kuelekezwa kwa daktari aliyepo pia Dar es salaam.

Ama hata najua kuna members humu ni wataalamu wa afya mawazo yenu pia ntayapokea.

Asante
 
Hizo ni changamoto za mimba miezi ya mwanzon. Hali hiyo itapotea yenyewe akifikisha miez minne hadi mitano. Usihangaike kumpa dawa kwan hakuna tiba ya hiyo hali. Kuitwa mama si mchezo!.
Hakika nashuhudia mkuu.. mwenyewe usingizi hauji kabisa
 
Hizo ni shida nyingi sana kwa trimester ya kwanza, jaribu kufika kwa specialist bila shaka atakua na second opinion
 
Cheki damu, katika kipindi hicho mama anachangia damu na mtoto na matumizi ya kiumbe ni makubwa. Upungufu wa damu husababisha maumivu ya kichwa.
Daktari atawapa ushauri zaidi
 
halafu na tabia za kuwapa mimba wachumba sio ishu, ungeoa kwanza.
Pole, nadhani waliotangulia wameishakusaidia
 
Mchumba wangu ana ujauzito ndo upo kwenye trimester ya kwanza ila amekuwa analalamika kupatwa na hizi shida
- Tumbo kuwaka moto
- Vichomi
- Mdomo unakuwa mchungu
- Halafu analalamika kichwa pia huwa kinakuwa kinamuuma
- Analalamika pia kwamba kwamba akila chakula anakaa mda mfupi na kutaka kula tena .. yaani ni kama akila chakula kinapotea.

Nimekuja hapa kuomba msaada ki ukweli maana nimeshazunguka vituo vya afya sasa kama vitatu ila bado sijakutana na daktar wa kutoa ushauri na matibabu ya kueleweka. Wengi wanaishia kusema hiyo ni kawaida tu 'unywe maji mengi' na 'mboga mboga' ila sasa naona shida imekuwa ni ile ile tu hamna hata nafuu.

Nitashukuru kama ntapata msaada wenu, mimi nipo Dar es salaam so ningependa kuelekezwa kwa daktari aliyepo pia Dar es salaam.

Ama hata najua kuna members humu ni wataalamu wa afya mawazo yenu pia ntayapokea.

Asante
Madaktar wote wamekidhi viwango ndio maana wanautwa madaktari,uzuri unaotk ww upi sasa au wa sura
 
Back
Top Bottom