Wana JF, nakufa na kipaji changu tafadhali nisaidieni......! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF, nakufa na kipaji changu tafadhali nisaidieni......!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by KAMBOTA, May 31, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe mkoani morogoro niko mwaka wa kwanza nachukua shahada ya production and operation management niliwahi kusoma seminari ya Mtakatifu Maria Visiga kwa O-level na baadaye Ilboru special school kwa A-level , sasa marehemu mama yangu alikuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi za watoto na mimi nikazaliwa na kipaji cha uandishi , nikageuka mtunzi wa vitabu, mashairi n.k , mpaka gazeti la Dira wakanikubali na kwasasa naandikia kwenye gazeti hilo kama mchambuzi upande wa makala za kisiasa na kihistoria. Sasa kinachonichanganya akili ni kuwa licha ya watu kukiri kuwa nina uwezo wa kuandika na kutunga ila bado hawako tayari kunisaidia, huku wakijua gharama za uchapaji ni kubwa mno sitoweza ku-afford, katika purukushani zangu nimefanikiwa kusajili kampuni yangu iitwayo Vijana Intellectual Company mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa tano ila sina pesa za kuchapa vitabu , wengi wa watu wanaojifanya wanasaidia ni wagumu mno na ni matapeli wa mjini, kwasasa nina umri wa miaka 21 ni kijana wa kiume na ni mtanzania pure kabisa . Huwa nafikiria kusubiri labda baadae nitakapokuwa na fedha za kutosha kuchapa lakini hofu yangu ni kuwa kwasasa ndiyo kijana mbichi na nguvu na akili yangu inachemka sana hivyo ni heri nikachakarika kutunga sasa kabla uzee haujaninyemelea, hivyo lengo hasa la kuja hapa jamvini ni kuwa natafuta mtu aliyetayari kunifadhili au kusimamia kazi zangu ili zichapwe na kusambazwa awe mtu mwenye uzoefu na aliyetayari kukuza vipaji vya vijana, awe na maono na mtazamo wa kimaendeleo mimi niko tayari hata kuingia mkataba naye ila cha msingi awe serious na kazi sitaki longolongo au blah blah, kifupi sipendi porojo za kupotezeana muda,naweza kuandika kwa lugha mbili yaani kiingereza na kiswahili kwa ufasaha kabisa bila matatizo yoyote, hivyo tafadhali aliyetayari tuwasiliane tuanze kazi haraka, sipendi kufa na kipaji changu nataka kuacha urithi kwa taifa letu na ulimwengu mzima...ASANTENI SANA
  Contacts zangu ni 0717-709618 au
  novakambota@gmail.com
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dogo, Ninamshukuru Mungu kwa kipaji alichokupa. Neema ya Mungu iwe nawe siku zote na akupe maisha marefu ili ulitumikie taifa lako. Dogo mie ninaushauri mdogo tu kulingana na historia uliyotoa. Nilipitia maisha kama yako ila sijapata kumshutumu mtu yeyote zaidi ya kuweka malengo yangu na kumtegemea Mungu na hivi ninamaliza degree yangu ya tatu (Ph.D in Civil Engineering). Hivyo nakushauri umalize shule kwanza, soma kwa bidii ufaulu masomo yako vyema upate first class distinction (Ikiwezekana uwe na GPA ya 5) alafu utaona watoa msaada watakavyokutafuta na hautawatafuta wewe. Usimbilie maisha haraka hivyo na kujiona unakipaji, Acha kipaji kikue na kijioneshe chenyewe na hapo utakula mema ya nchi. Una mwanzo mzuri ila unataka kutafuta mwisho mbaya!!
   
 3. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ni bahati nzuri kwamba umeweza kutambua kipaji chako, faida za kufanyia kazi kitu unachokipenda ni kwamba unakuwa na uwezo mkubwa wa kuvumilia hata kama mafanikio hayaji mara moja, kuna tatizo kubwa la vijana wengi wa kitanzania kutotambua vipaji vyao (hata wenye kiwango kama chako cha elimu) jambo ambalo linachangia sana kuwakwamisha maendeleo yao.

  Mshukuru mungu kwa kukuwezesha kutambua kipaji chako mapema, tunza kazi zako zitakulipa lazima (it's just a matter of time). Usikate tamaa kamwe katika maisha yako.
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Endelea kuandika,ila weka msisitizo sana kwenye masomo yako ya chuo uhakikishe unafanya vizuri....nina hakika kwa confidence uliyonayo kuhusu uwezo wako na hatua kama hii ya kuzungumza na kuwa tayari,Mungu atafungua mlango kwa wakati wake,uzuri hujakaa tu na kusubiri muujiza,unafanya uwezalo kupata sponsors,na utawapata....priority number one iwe mafanikio katika masomo ya chuo kwa sasa. Hutakufa na kipaji chako,hilo ni hakika,kuwa mvumilivu kidogo na zidi kujieleza kwa watu,huwezi jua wapi mlango utafunguliwa.....goodluck!!
   
 5. A

  Albimany JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mkuu atamaliza vipi masoma yake na unajua masomo ya juu sio bure?

  mini bado nasema kama mfadhili yuko ajitokeze kumsaidia kijana kama alivyojielezea,hiyo itamsaidia kijana kuweza kuendelea na masomo wakati huo akikikuza kipaji pia.
  e
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  ukijitambua utajikomboa,
  wakati ni huu kijana tumia kipaji chako kujikomboa.
  dunia ya sasa watu wanaangalia whom you know and not what you know or have..make contacts through your work na sio lazma kipaji chako kikunufaishe leo, ila kitumie kujuana na watu ambao watakuwa msaada kwako.
   
 7. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye RED naomba sana mkuu ukiweza soma RICH DAD POOR DAD!
   
 8. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,891
  Likes Received: 1,644
  Trophy Points: 280
  Ikiwa una amin unaweza pesa itakufuwata ila sio kuifuwata. Angalia matajir wakubwa sana wamefanikiwa kwakujitegemea nasii kutegemea. Amin u have a capital and u wl do! What ever u wish.
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Jaribu kuchukua mkopo Benki, manake siku hizi ukienda na wazo lenye mwelekeo mzuri hawatasita kukupatia kiasi cha Pesa utakachohitaji..
  Cha muhimu usiwe na Papara, mambo mazuri hayataki haraka..
  Good luck..
   
 10. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  You are right Michelle, tatizo ni kwamba elimu yetu haitufundishi kuwa na three C's yaani COMPETENCE, CONFIDENCE NA COMMITMENT
   
 11. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  "sasa marehemu mama yangu alikuwa mwandishi wa vitabu vya hadithi za watoto na mimi nikazaliwa na kipaji cha uandishi , nikageuka mtunzi wa vitabu, mashairi n.k , mpaka gazeti la Dira wakanikubali na kwasasa naandikia kwenye gazeti hilo kama mchambuzi upande wa makala za kisiasa na kihistoria."

  Unayakumbuka Haya maneno aliyosema?? au hukusoma??,

  Mi nashauri kwa pesa ndogo anayopata aiweke kwenye Elimu hata kama ikiwa ndogo kiasi gani, Mimi nilikua nalipwa buku 5 kwenye Kazi yangu ya Kuendesha tex Mbezi mWisho pale, Nikasoma MOA, kwa Sasa Nagonga mlango wa Degree ya pili.

  Sali Sana, Heshimu kazi yako, Usiache kuandika, Vitabu haviandikwagi ndani ya miezi au mwaka, ni miaka.

  Elimu Kwanza Mr!
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  pole,na hongera kwa kipaji. ni kawaida kwa kijana kuwa na haraka ya kutimiza ndoto zake haraka. kama ulivyoshauriwa,vuta pumzi.endelea kuandika na hifadhi scripts zako. ukifika wakati,utakutana na the right pple na utapata muelekeo. mbuyu unaoona leo ulianza kama mchicha. kila la kheri, uandike hii kwenye dibaji ili siku nikisoma vitabu vyako nikukumbuke na kuona fahari juu yako.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ok mi nakushauri jifunze kuandika proposal then tafuta NGO kama DFID ,USAID, NORAD, DANIDA au british council na ofisi za balozi nyingi tu na nyingine nyingi. Hata UDSM au hata wizara ya utamaduni.

  Ukiandia proosal yako vizuri huweiz kukosa wa kukufadhili hata 100% kama kweli unayoandika yana manufaa na ni ya muhimu kwenye jamii ya kitanzania.

  je unaweza kutoa japo summary ya kazi yako moja au mbili nzuri kuliko zote yaani amabyo katika zote uipata mfadhili ndo utataka muanze nayo?
   
 14. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  nina wasiwasi kama wewe ni mwandishi mzuri,, maana unaandika post halafu inakuwa haina paragraph - i.e. unaandika paragraph ndefu mno.. jaribu kufanya paragraph fupi fupi....
   
Loading...