kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Mko msibani wakati wakutoa jeneza, marehemu alikuwa rafiki yako, hivyo unalazimika kuwa mstari wa mbele katika kubeba jeneza. Lakini kwa jinsi usivyomstaarabu huku-mute wala kuzima simu yako. Ile mnatoka tu mlangoni simu inaanza kuita tena sauti kubwa (simu ya kichina) ''kimasomaso, mwanangu usimuone'' x5
Kutaka kupokea unataka, kuizima unataka ila umebeba jeneza huwezi kuachia. Watu wameshikwa butwaa wanakushangaa. Wana Jf, sipendi watu wanaoacha simu zao on kwenye misiba au sehemu za kuabudia. Hebu tajeni mambo mengine msiyoyapendelea ili iwe fundisho kwa wenye tabia hizo na wamejisahau.
Nawatakia weekend njema.