Wana JF muogopeni Mungu.

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Mko msibani wakati wakutoa jeneza, marehemu alikuwa rafiki yako, hivyo unalazimika kuwa mstari wa mbele katika kubeba jeneza. Lakini kwa jinsi usivyomstaarabu huku-mute wala kuzima simu yako. Ile mnatoka tu mlangoni simu inaanza kuita tena sauti kubwa (simu ya kichina) ''kimasomaso, mwanangu usimuone'' x5
Kutaka kupokea unataka, kuizima unataka ila umebeba jeneza huwezi kuachia. Watu wameshikwa butwaa wanakushangaa. Wana Jf, sipendi watu wanaoacha simu zao on kwenye misiba au sehemu za kuabudia. Hebu tajeni mambo mengine msiyoyapendelea ili iwe fundisho kwa wenye tabia hizo na wamejisahau.
Nawatakia weekend njema.
 
Ile mnatoka tu mlangoni simu inaanza kuita tena sauti kubwa (simu ya kichina) ''kimasomaso, mwanangu usimuone'' x5
Kutaka kupokea unataka, kuizima unataka ila umebeba jeneza huwezi kuachia. Watu wameshikwa butwaa wanakushangaa
i see, you've made my day! well noted!
 
Hili ni dongo kwa nani?
Juzijuzi paka jimmy alifiwa na mpendwa wake,
je jambo hili lilitokea kwenye huo msiba?
Si useme bayana tumseme mkosaji ili ajirekebisha?
Be straight
 
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa nini hakuzima simu.Sometimes watu wanajisahau au wanakuwa wamechanganyikiwa na mawazo mengi
jifunze kuvumilia watu wa kila aina na tabia
 
Hapana Kiranja Mkuu,
Nimeonelea tusifanye mambo yanayowachukiza wenzetu kwani kwa kufanya hivyo tunamchukiza na Mungu pia. Ni hilo tu si mlengi mtu ila nawashirikisha wana JF wote katika tabia njema.
 
Mko msibani wakati wakutoa jeneza, marehemu alikuwa rafiki yako, hivyo unalazimika kuwa mstari wa mbele katika kubeba jeneza. Lakini kwa jinsi usivyomstaarabu huku-mute wala kuzima simu yako. Ile mnatoka tu mlangoni simu inaanza kuita tena sauti kubwa (simu ya kichina) ''kimasomaso, mwanangu usimuone'' x5
Kutaka kupokea unataka, kuizima unataka ila umebeba jeneza huwezi kuachia. Watu wameshikwa butwaa wanakushangaa. Wana Jf, sipendi watu wanaoacha simu zao on kwenye misiba au sehemu za kuabudia. Hebu tajeni mambo mengine msiyoyapendelea ili iwe fundisho kwa wenye tabia hizo na wamejisahau.
Nawatakia weekend njema.

Ni bahti mbaya tu ktuokana na kupitiwa au kuwa na matukio mengi kichwani..hutokeaga. Baada ya tukio hilo mhusika atakua kajifunza kama mimi msomaji ninavyojifunza kwa kusoma.
 
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa nini hakuzima simu.Sometimes watu wanajisahau au wanakuwa wamechanganyikiwa na mawazo mengi
jifunze kuvumilia watu wa kila aina na tabia
Charity,
Nimetoa maelezo tu na sikumhukumu mtu, au nitajie hukumu niliyoitoa hapo kwenye maelezo yangu. Au hujui kutofautisha Hoja, Shitaka na Hukumu?
 
Ni bahti mbaya tu ktuokana na kupitiwa au kuwa na matukio mengi kichwani..hutokeaga. Baada ya tukio hilo mhusika atakua kajifunza kama mimi msomaji ninavyojifunza kwa kusoma.
Abdu,
Haya ndio majadiliano, asante sana kwa mchango wako, kwamba kuna kupitiwa lakini bado si jambo jema, ndio maana nimetoa changamoto ili tujisahihishe na tuwe wepesi kukumbuka.
 
Kweli inabidi tuwe makini, maana uzembe kama huu wakati mwingine unaeza kuku-cost vitu vingi sana au kusababisha distress, kutegemea na social laws za mahali husika..
 
Mie nilifikiri kuna jambo wana JF wamefanya la ajabu!!!
Mchili,
Ndio maana ikaitwa hoja, uelewa wa hoja unatofautiana kutokana na elimu, umri, utashi au mazingira ndio maana wewe umefikiri hivyo.
 
Kweli inabidi tuwe makini, maana uzembe kama huu wakati mwingine unaeza kuku-cost vitu vingi sana au kusababisha distress, kutegemea na social laws za mahali husika..
Abdu,
I like your wisdom, stay blessed.
 
Charity,
Nimetoa maelezo tu na sikumhukumu mtu, au nitajie hukumu niliyoitoa hapo kwenye maelezo yangu. Au hujui kutofautisha Hoja, Shitaka na Hukumu?
Usijali.sijakutaja wewe kama wewe kakuruvi.Ila to whom may be concerned.Mara nyingi huwa linapotokea tatizo sisi viumbe ni wepesi sana wa kuhukumu na kulaumu wengine.Utamuona hafai na vitu vingine kama hivyo bila kujua chanzo cha hayo.lakini jambo lile cku unafanya wewe utatafuta sababu ya kujitetea.Mfano mdogo ni nyumbani,hausigeli anaweza kuvunja glasi na akafokewa sana au hata kukatwa mshahara.Na ikitokea mama mwenye nyumba akavunja glasi huwa haionekani kama ni uzembe ila bahati mbaya.
Ckuwa na maana ya kukukwaza.nisamehe kama umekwazika.
 
''kimasomaso, mwanangu usimuone'' x5

Nadhani na ringtones nazo tuwe tunachagua vizuri. Kuna ringtone zingine ukizisikia na kumtizama mwenye simu, yaani mpaka unashangaa! Najaribu kuimagine kama ingekuwa ringtone nyingine hapo kwa mfano ya kumtukuza Mungu hivi, pengine mambo yasingekuwa mabaya kihivyo. But yes I agree tukiwa misibani tujitahidi kubehave vizuri!
 
Safi nimekupata Mkuu, Charity begins from ourselves.
 
Nadhani na ringtones nazo tuwe tunachagua vizuri. Kuna ringtone zingine ukizisikia na kumtizama mwenye simu, yaani mpaka unashangaa! Najaribu kuimagine kama ingekuwa ringtone nyingine hapo kwa mfano ya kumtukuza Mungu hivi, pengine mambo yasingekuwa mabaya kihivyo. But yes I agree tukiwa misibani tujitahidi kubehave vizuri!
Umenielewa nashukuru Mkuu.
 
Ni pale mtu anapoweka Ring tone ya matusi,

e.g. kuna ring tone moja almaarufu sana kwa hawa vijana wetu wa siku hizi inaongea hivi kwamba:-
WEWE **MA**KO POKEA SIMU x 20++
itaita hilo tusi hadi mtu apokee, ilitokea siku moja kwenye daladala, watu tuliona aibu kwa jinsi mliowasimu wa matusi ulipokuwa unalia halafu kwa muda mrefu, huku mhusika wa simu akiwa ni mtu mzina usiyemzania
 
watu wanapitiwa jamani maisha yanatuchanganya sana unaweza kuta huyo jamaa alikuwa na mawazo kibao mfukoni hakuwa hata senti ,..lakini pia ni funzo kwa wote
 
ilitokea siku moja kwenye daladala, watu tuliona aibu kwa jinsi mliowasimu wa matusi ulipokuwa unalia halafu kwa muda mrefu, huku mhusika wa simu akiwa ni mtu mzina usiyemzania
Ndio hayo tunayosema masikini Mzee wa watu labda alichukua simu ya mwanae akaoshe nayo bila kujua ringtone ni matusi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom