Wana JF Kuhusu Swala la Marketing hatuwezi anza hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF Kuhusu Swala la Marketing hatuwezi anza hivi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Dec 17, 2011.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Swala la Marketinghatuwezi anza hivi?

  - Si uongo kwa sasa kuna ushindani mkubwa sana wa kibiashara kwa sasa duniani kotejambo ambalo hufanya watu kuja na njia mbadala za kutafuta soko

  - Wakuu nimekuwa ni kijiuliza kwa nini Wahindiwanafanikiwa sana katika biashara hapa Tanzania? Nasasa hata wachina na Wazungu.?

  - UKIJARIBU KUTAFITI NI KWAMBA.

  0. Wahindi hawana wivu wao kwa wao.

  1. Wahindiwafanya Biashara wana umoja mkubwa sana
  2. Wanamtandao wao unao waunganisha nchi nzima
  3. Nawameweka na sheria za kuwalinda wao kwa wao
  4. Katikahuo umoja wao wanahakikisha wanainuana wao kwa wao kwanza. Kivipi?

  - WAHINDI HUFANYA BIASHARA WAO KWA WAO PAMOJA NA KWAMBACC WABONGO NDO WATEJA WAO WAKUU.

  - MHINDI AKIHITAJI BIDHAA ATAENDA KWENYE DUKA LA MHINDIMWENZAKE AKIKOSA ATAENDA JINGINE MPAKA APATE, HAWEZI ENDA KUNUNUA KWA MBONGOWAKATI HICHO KIFAA KIKO KWENYE DUKA LA MHINDI MWENZAKE

  - VILE VITU AMBAVYO HAVIUZWI NA WAHINDI WENZAO NDO HAPOHUWA WANAENDA KWA MADUKA YA WABONGO

  - WAKO RADHI WASAFIRI HATA KUTOKA ARUSHA KWENDA MOSHIKUNUNUA KIFAA KWENYE DUKA LA WAHINDI WENZAO HATA KAMA HICHO KITU KIPO ARUSHAKWA MADUKA YA WABONGO

  - KIKIKOSEKANA KAMA NIKIFAA KIKUBWA SANA KITAAGIZWA HATA DAR KWA WENZAO, HATAKAMA KIKO WANAPO ISHI ILA KINAUZWA NA WABONGO

  - KWENYE UJENZI WAHINDI HUTAFUTA MAKONTRACTA WAKIHINDINDO HUWA WANAWAJENGEA JARIBU KUFUATILIA UONE.

  - WANAFANYA BIASHARA WAO KWA WAO
  1. Kwanini wao waweze?
  2. Wanatumiambinu gain?

  Kuhusu Swala la Marketing Hatuwezi anza kama Wahindi?

  - Najua humu JF kuna makundi ya wafanya Biashara wafuatao

  - WAFANYA BIASHARA WA IT NA KOMPUTA REPAIR

  - WAUZAJI WA KOMPUTA

  - WAUZAJI WA SIMU

  - WAMILIKI WA MIGAHAWA YA CHAKULA/Hotel au restraurant

  - WAMILIKI WA MADUKA YA NGUO/VIATU

  - WAMILIKI WA HOTEL/ GUEST HOUSE

  - WAUZAJI WA NAFAKA/ MAZAO MBALIMBALI YATOKANAYO NA KILIMO NA MIFUGO

  - WAFUGAJI WA KUKU WA NYAMA

  - WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA NA NYAMA

  - WAFUGAJI WA KUKU WA MAYAI

  - WAMILIKI WA MIN SUPER MARKET

  - WAMILIKI WA MADUKA YA REJAREJA

  - WAMILIKI WA GEREJI ZA KUTENGENEZA MAGARI

  - WAUZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO

  - WAKULIMA WA MAZAO MBALIMBALI

  - WAMILIKI WA KAMPUNI ZA KUSAFIRISHA MIZIGO

  - WAMILIKI WA KAMPUNI ZA DESAINING

  - WAMILIKI WA KAMPUNI ZA PRINTING MATANGAZO NA KAZIMBALAMBALI

  - WAMILIKI WA SARUNI ZA WANAUME KWA WANAWAKE

  - WAMILIKI WA KAMPUNI ZA UWAKILI/ SHERIA

  - WASHAURI WA BIASHARA

  - WAMILIKI WA KAMPUNI ZA UJENZI NA KUCHORA RAMANI

  - WAMILIKI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO NA VYA KATI

  - WAMILIKI WA CAR HIRE, TAX NA KAZALIKA

  HIZO NI CHACHE WAKUU INGAWA NAJUAWAKO HUMU WANA MILIKI BUSINESS ZA AINA TOFAUTI TOFAUTI

  1 Je wakuu sisi hatuwezi kutengeneza market network tukaanzakuuziana sisi kwa sisi?

  2. Hatuwezi fanya Biashara sisi kwa sisi?

  3. Kama ni ndio tufanyeje ili na sisi tuwe kamawafanya biashara wa kiasia wanao pigana tafu wao kwa wao?

  4. Kama haiwezekani tatizoni nini?

  5. KWA NINI WAHINDI WANAWEZA NA CC TUSHINDWE? NA KWA SASA HATA WAUNGU WALIOKO TZ NI HIVYO HIVYO

  KWA SASA KUNA USHINDANI MKUBWA SANA WA KIBIASHARA KIASIKWAMBA BILA KUTENGENEZ NETWORK HATUTAFIKA MBALI, TUAZE NA SISI TUJARIBUKUTENGENEZA DIRRCTORY YETU WAFANYA BIASHARA MIKOA YOTE NA AINA YA BIASHARAAMBAYO MEMBERS ANAFANYA ILI UKIHITAJI HUDUMA FULANI UNAMCONSALT KWANZA MEMBERS NAKAMA MEMBERS HAWANA BASI NDO TUENDE KWA HAO WAHINDI NA WENGINE.


   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wazo lako ndiyo haswaa mwalobaini wa ajira zisizo rasmi na masoko ya bidhaa za ndani. Ila nasikitika JF ni pahala pa kupiga soga za kisiasa zaidi kuliko kujadili uchumi.
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Yapu good aidia,
  tatizo sisi watanzania tunaoneana wivu sisi kwa sisi, mtanzania anaona akienda kununu kitu kwa fulani atakuwa anamnufaisha sana, so anaona bora akawachangie hao wahindi na wengineo.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280

  Ya ni jambo ambalo likiwekwa katika practical linaeza saidia wafanya biashara wadogo humu. kwa sasa competition ni kubwa sana na wanao umia na hiyo stiff competition ni wafanya biashara wa dogo na wakati, make wao hawana mitaji mikubwa kushindana na makampuni makubwa
  - nikupitia njia hii tunaqweza shindana na makampuni mengine katika kuuza.
   
 5. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,128
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja kwa asilimia mia.
   
 6. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Tatizo letu ufanisi unakuwa very slow. Unamwambia mtu nifanyie kazi hii munakubaliana kazi itafanyika kuanizia kesho , jamaa nakuja na excuse kibao leo siwezi aanza kuna vifaa fulani kumbe havipo, mara ooh nimepata tatizo la kifamilia mtoto wa mjomba wake mke wangu kafiwa na mdogo wa mume wake . hapo tukibadilika yote yatawezekana
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Tunaweza baada ya muda mrefu kidogo. Nitatoa mchango kidogo.

  Nilikuwa nanunua saruji kwa jamaa yangu mmoja mifuko mingi, baadae jamaa akaanza kuniuzia saruji iliyochakachuliwa. Sasa mimi nikawa nagombana na mafundi kila siku, kumbe ni jamaa yangu. Nilituma gari siku moja bila fundi kwenda, jamaa kapakia mifuko ya ajabu. Ili nipate amani ilibidi nihamie kwa Mhindi/Mpakistan pale Sokota, sababu ya kwanza hiyo inayoleta ugumu.

  Njoo ktk bei, kwa jamaa hapa Buguruni bei ni mbaya kuliko Mbagala kwa mgeni, halafu kwa huyu mgeni wapakiaji analipa yy na sio wezi, kwa huyu jamaa yangu vibaka kibao. Chukulia mfano wa wale Warusi pale Tabata na bei zao zilivyo za haki, nenda pale pale kwa Mswahili mwenzako uone cha moto, sababu ya pili hiyo.

  Wabongo tunauza mafeki huku tukijua ni mafeki, sasa nina sababu gani ya kuja dukani kwako nikishajua ww unauza feki? Sasa hivi tunachakachua kila kitu, hadi mizani tumechakachua.

  Kwa ufupi tunakomoana wenyewe. Tubadilike.

  Ngoja na wengine wachangie.
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  MKUU UNACHO SEMA NI SAHIHI KABISA, BUT KUMBUKA HATA WAHINDI NI MABINGWA WA KUCHAKACHUA.

  OK PAMOJA NA KWAMBA KUNA MATATIZO MENGI SANA KAMA VILE UAMINIFU NA USANII KINACHOTAKIWA NI NJIA YA KUWEZA KUWEZESHA HILI.

  - MKUU KWA USHINDANI WA SASA BILA MBINU MBADALA NI VIGUMU KUSHINDANA NA MAKAMPUNI MAKUBWA KABISA HAPA TANZANIA. NA IT WILL TAKE A TIME KUSHINDANA NAO KIKAMILIFU KWENYE SOKO

  - MIMI NA ZANI SOLUTION SI KUANZA KUPONDEA KWAMBA HAKUNA UAMINIFU, KWA SABABU HATA SISI TUNAO PONDEA UNAWEZA KUTA KUNA USANII HUWA TUNAFANYA KATIKA BUSINESS.

  - INAWEZA TENGENEZWA CLUB FULANI HIVI NA IKAWA NA MEMBERS AMBAO WANAJISHUGHULISHA NA BUSINESS ZA AINA TOFAUTI THENI IKATENGENEZWA UTARATIBU AMBAO UTAWEZESHA MEMBERS KUFANYA BIASHARA WAO KWA WAO PAMOJA NA KWAMBA WATAKUWA WANAWAUZIA NA WATU WA NJE.
  - MFANO.
  1. KUNAWEZA KAKAWA NA WAZALISHAJI WA MAYAI PAMOJA NA KUKU WANYAMA
  2. NA KUNA WAMILIKI WA MADUKA YA JUMLA NA REJAREJA/MIN SUPERMARKET
  KWA NINI HAWA WA MATAI NA KUKU NYAMA WASIWAUZIE HAWA MEMBERS?
  KWA NINI HAWA WAMILIKI WA HIZI SUPER MARKET WASINUNUE KWA HAWA MEMBERS AMBAO WANAZALISHA MAYAI?

  HUO NI MFANO TU BUT KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA HILI JAMBO KUFANYIKA NA KUFANIKIWA.

  TATIZO LA SISI WA TANZANIA TUNASHINDWA KABLA YA KUANZA YAANI KABLA YA KUANZA KUPLACTICE TIYLAI MTU KASHINDWA.

  1. Tukuiendelea na huu mfumo tutapata shida sana tutabaki kuwa fanyia kazi wahindi.
  2. Ni kivipi mmiliki wa kiwanda kidogo sana cha kusaga nafaka ataweza kuteka soko na kushindana na wakina AZAM, MOHAMED ENTREPRISES, AZANI, PEMBE NA KAZALIKA?

  NJIA PEKEE NI KUTENGENEZA MTANADAO NA ITAWEKWA VIGEZO NA SHERIA ZA KULINDA MNUNUZI NA MUUZAJI NA SI KWAMBA WATU WATU WATUMIE NJIA HIYO KUUZA LOWA QUALITY GOODS AND SERVICES.

   
 9. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Ni wazo zuri sana ila hilo ni ngumu kufanikiwa kutokana hatuna UZALENDO, HESHIMA, HAKI baina yetu watanzania na hilo ndio linatuangusha kuanzia ngazi ya viongozi wetu hadi walalahoi.

  Mtanzania anaweza kuwa ananunua bidhaa kwa meku kwa wingi sana na meku akaanza kumbambikizia bidhaa mteja wake au kupandisha bei ovyo kisa tu amemzoea,au huyu mteja anaanza kutolipia bidhaa zake kwa muda husika atakuja na story kibao anasahau kuwa meku atashindwa kuendesha biashara.

  Pia kuna suala la UZALENDO hili ni kubwa sana aisee yaani mtu akiona bidhaa ya TZ tu anaanza kudharau au akienda dukani kwa mmatumbi anaona kama kila kitu fake au kuona kila kitu kinachouzwa na ngozi nyeupe ni bora zaidi atakama wanaibiwa.
  Ukija uswahilini huku unataka kumuajiri kijana akusaidia kazi yeye anataka mshahara mkubwa kuliko msomi wa ofisini, kazi ya 10,000 yeye atataka 30,000 na zaidi kisa anakuona kama unazo.

  Tukiweza haya mambo matatu itasaidia sana uchumi wetu mpaka uongozi .......UZALENDO, HESHIMA, HAKI baina yetu waTZ
   
 10. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Idea ni nzuri mkuu, labda kwa kuongeza yaliyochangiwa, Watanzania na Waafrika kwa jumla ni watu very selfish, yaani tuna ule tunaita mtimanyongo tunapoona mwenzetu anafanikiwa, sijui nalo tutakabiliana nalo vipi.
  Alaf inabidi tufaham huu ushindani wa kibiashara unatokana na bei zetu.
  Mass production/sales ndiyo siri ya biashara yoyote, kwasababu jinsi unavyo uza kwa wingi ndiyo overheads/fixed cost zinavyopungua, hivyo ukiuza bei ya chini kidogo, profit margin inakua ile ile na unapata wateja wengi zaidi. Lakini tatizo letu tunataka utajiri wa haraka kwa ku hike prices kitu ambacho kinafukuza wateja.
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Si vigumu kufanya, najaribu kuuonyesha umma matatizo tuliyo nayo ambayo ni ya kizembe zaidi. Haya tunaweza kuyaondoa bila kulipa ada chuoni. Kwa njia ya kuambizana wazi hali inaweza kubadilika. Habari za customer care ni issue nyingine muhimu.

  Kama tunaweza kuweka matatizo ya kizembe yanayotukabili wazi na kuyapa majibu yake, tutakuwa tumepiga hatua moja mbele.
   
 12. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Good points wakuu...TUBADILIKE WAJAMENI..
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wamebadirisha biashara zao bila gharama kubwa, mzee mmoja ana nyumba ya wageni pale mkoani. Huyu mzee asubuhi huwa anawahi kuleta chai yy mwenyewe na kuwajulia hali wateja wake. Anawauliza nini kimewasumbua au wapi amekosea.

  Asubuhi anakupa mlinzi akupeleke Stand ya bus ili usafiri salama, hii ni huduma kwa mteja. Sisi tumegeuka ni matangazo ya biashara yake, hakuna siku chumba kinalala bila mtu.Usafi,ulinzi, lugha vyote safi. Mimi na wafanya b/ness wenzangu ni lazima tufikie kwake. Huyu tayari ana net work.

  Ninachokisema hapa, ni lazima sisi wajasiriamali tuwe sehemu ya biashara zetu kama huyu mzee. Sio unaajiri kijana na wewe unapiga mluzi na maji ya mende kwa mbali, ni lini utajua kijana kaharibu kazi?
   
 14. SUPERUSER

  SUPERUSER JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  I agree with u kwamba patriotism ina matter kwa success ya business ata uchumi wa taifa...ila nadhani wahindi wananunuzana wao kwa wao coz they are minority...ata mbongo ukiwa nchi za wenzetu ukikutana na mbongo mwenzio lazima muestablish connection
   
 15. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mhh! Hapa nilipo kuna mbongo ana duka lake la vyakula toka bongo na vingine vya hapa. Sasa huyu bwana anafungua duka muda anaotaka yeye na kufunga anapotaka yeye. Je kwa mwendo huu utaweza kweli ku depend kupata bidhaa toka kwake? Yaani ule utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuwa serious kwenye kazi hatuna kabisa!!!
   
 16. DullyM

  DullyM Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Na sisi wabongo tuna tatizo flani extra!! ukizitengeneza kidogo tu lazima ubadilishe life style!! wahindi anaweza kuchakachua mpaka vi extra billioni lakini ukikutana nae bado anazungumzia biashara kwa heshima!! sisi kuna wale wa mtindo flani akizidaka kwanza kiswahili anasahau hayo yanayofuata usiulize.. sasa lini tutafika?!?!!?
   
 17. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Wakuu tatizo si kuangalia kimefanyika nini ila kinachotakiwa ni kuona tunafanyaje.
  - Najua kuna tatizo kubwa sana la elimu ya biashara kwa watanzania walio wengi sana, na hilo lina sababishwa na mambo mengi sana, kama vile
  1. Uelewa mdogo wa elimu ya Biashara
  2. Kutumia ndugu katika biashara mtu akiamni anabana matumizi
  3. Kushindwa kuwekeza katika utafiti, hapa katika utafiti ni kwamba ni watanzania walio wengi wanao fanya business asilimia 100% hawatengi kiasi fulani cha mapato yao kwa ajili
  1. Tafiti za bidhaaa mpya/ new product and services
  2. Marketing
  3. Kusomesha wafanya kazi wake/kuwaendeleza kielimu
  - Wafanya biashara wengi wanaona kuwaendeleza kielimu wafanya kazi wake ni hasara na na mtu anaishia kuajili ndugu zake wasio kuwa na elimu yoyote ile.

  - WAKUU MIMI NICHO ZUNGUMUZIA NI KWAMBA MEMBERS WA JF NA SI WOTE NDO TUTENGENEZE HIYO NET WORK, MIMI SI MANISHI WATANZANIA WOTE, NAZANI HATA KULE INDIA WAHINDI HAWAFANYI KAMA WANAVYO FANYA HUKU, ILA HUKU WAMEAMUA KUFANYA HIVYO KWA SBABU NI WACHACHE NA ILI WAWEZE KUSHINDANA VYEMA.

  - SI RAHISI HII KITU IWAHUSISHE WATANZANIA WOTE WANAO FANYA BIASHARA. ILA NI GROUP FULANI AMBALO LINAWEZA TENGENEZWA
  - KILICHOPO TUJADILI INAWEZA KUWA VIPI NA SI KUPONDEA KWAMBA WATANZANIA WANAFUNGUA MDA WANO TAKA NA WANAFUNGA MDA WANAO TAKA.

  WAKUU KWA HILI LA WAHINDI NAZANI WANA SHERIA ZINAZO WA GUIDE SI KWAMBA WANAJIENDESHEA TU KIHOLELA
   
 18. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  MKUU MIMI SIJAMANIISHA HII KITU IJUMUISHE WATANZANIA WOTE,

  -
  HII KITU NI KWA SMALL ENTREPRENEURS AMBAO WANAANZ NA HII ITASAIDIA KUWA BUST ILI WAWEZE KUSHINDANA BAADAE NA WATU KAMA AKINA MOHAMED ENTREPRISES.

  -
  Ukisema iwajumuishe wafanya biashara nchi nzima haitakuwa na maana tena, na unacho sema kwa wahindi ni sahihi kwa sababu wako wachache, ila na wao hii inawasaidia kushindana na watanzania.

  Hii network ninayo zungumzia inakuwa ni kama clabu fulani ambayo itakuwa na members ambao ni wafanya biashara mbalimbali hapa Tanzania.

  1.
  Hii networl au club inaweza kuwa na sheria zake za kuwalinda wanunuzi na wauzaji

  2. Na tunaweza kuwa tunakutana kila mwaka mara mbili kupena up dates na changamoto za biashara

  3. Kutakuwa na muda maalumu wa mwanachama kuwepo kwenye club it means hii club itatumika kuwalea wafanya biashara wadogo na wanapo fikia umri fulani basi wanaachwa washindane wenyewe huko nje.

  4. Hii ya muda maalumu itamfanya members achacharike zaidi kwa sababu anajua ana miaka my be 4 ya kupata hii service

  - Mfano mimi naweza anzisha kampuni ya IT nitapata sapoti ya kuwafanyia kazi members na hapo hapo nafanya na kazi zisizo kuwa za members na baada ya muda fulani nitakuwa ni mekomaa kuweza kushindana na makampuni makubwa ya IT hapa Tanzania na nje ya nchi

  - Hii wakuu inaweza wasaidia wale ambao wanaanza Biashara na wanakumbana na ushindani wa kufa mtu, hivyo wanapo kuwa na sehemu ya kuwasaidia kupanda juu inakuwa vizuri zaidi.
  - Na hii tunaweza kuwa na website yetu na members wote wakawa na akaunti zao mle kwa ajili ya kupasha na news yza biashara.

  INAWEZEKANA TUACHE MANENO NA TUACHE KUSHINDWA HATA KABLA YA KUJARIBU, NDO TATIZO LETU WATANZANIA
   
 19. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  - True mkuu,
  Ni lazima tuheshimu Business zetu, Tunako elekea watanzania wengi watakuja shindwa biashara kwa sababu ya Mambo kama hayo.
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Mawazo yako mazuri sana lakini jf wengi hawapendi kujulikana kazi zao. Ni wachache sana wanaojitangaza. Nashindwa kuelewa wengi wameajiriwa au wana biashara ila washaridhika na wateja wanaopata.
   
Loading...