Wana jf huyu mtoto ni malaika anahitaji msaada wetu, na amekataa kwenda loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana jf huyu mtoto ni malaika anahitaji msaada wetu, na amekataa kwenda loliondo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by COMPLICATOR2011, Jul 19, 2011.

 1. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  [h=1]Mtoto huyu haendi Loliondo[/h]

  [​IMG]Mtoto Cecilia Edward (14) (pichani), mkazi wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, ambaye kwa sasa anaishi na mlezi wake, Mbagala jijini Dar es Salaam, bado anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akihudhuria kliniki na hajapata mabadiliko.

  Kwa mujibu wa mlezi huyo, Cecilia anasumbuliwa na ugonjwa huo, hali iliyosababisha tumbo kujaa maji mara kwa mara.

  Imeelezwa na mlezi wake huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwamba tatizo hilo lilimuanza Cecilia baada ya wazazi wake wote kufariki dunia akiwa na umri wa miaka minne.

  Hata hivyo, mlezi wake huyo alisema mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuwa hana niya ya kwenda kutibiwa Loliondo kama ilivyoripotiwa na gazeti hili siku za nyuma.

  “Sina mpango wa kumpeleka mtoto huyu Loliondo na anaendelea na kliniki,” alisema.
  Awali gazeti hili katika toleo namba 687 la Mei 31 liliandika kimakosa kuwa jina lake ni Khadija Ally na kuwa mtoto huyo anaomba msaada wa kwenda kutibiwa Loliondo kwa Babu.
  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wandugu wapenda angalieni kiumbe huyu.....UKIMSAIDIA MMOJA WAPO WA WADOGO HAWA UMEMJUA MUNGU KWELI KWELI.....NA UKIMKATAA MMOJA WAPO WA WADOGO HAWA UMEMKATAA MUNGU KWELI KWELI....
   
 3. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Sasa kinachonishangaza mimi ni huyo mlezi wa mtoto huyo kukataa kutaja jina lake, au ndo chuma ulete wake?
   
 4. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  kwani we jina la mlezi unalihitaji la kazi gani? Toa msaada upokee baraka. Imeandikwa fanya wema usingoje shukrani.
   
 5. d

  dakota Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  mimi naomba contact za huyu mtoto au account number ya bank au je pesa nitakayo tuma tafikaje kwa mlengwa please naomba kama nitaweza kuwasiliana na mzazi wa huyu mtoto
   
Loading...