Wana JF, Hivi kuna tatizo gani kuoa mwanamke aliyekwisha zaa

Wakuu naomba nifahamisheni mazuri na mabaya ya kuoa mwanamke aliyezaa, kuna mwanamke naona tunaendana kila kitu sema yeye tayari ana uzao

Mkuu kama ungeuliza kuoa mwanamke aliyekwisha olewa hapo ningekuwa na ushauri negative...! Unajua ndoa ikiwa mpya ile kitu mtu anaitimba kishenzi.....ingekuwa Big G ingekuwa hoi tepe tepe...!
 
ewaa mrs apo ndo penyewe...kisa na mkasa ...ndo kusema kwamba kama walitengana kwa sababu nje ya uwezo wao kuna hatari wakakumbushiana ili mtoto asifananie upande mmoja tu lol

jingine ikitokea kuwa mi niliyekuoa tukakorofishana kidogo basi si itakuwa rahisi kwenda kwa 'baba mtoto' ! kupoza machungu! na mi niliyeoa nikijua kabisa possibility iyo ipo
!

hivi nitaendaje tena kwa huyo baba mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine hakutaka/hakupenda kunioa bali kunizalisha tu?...ukute baba mtoto kashaoa, mie nimekorofishana na wewe niende kupooza kwake kha! kwa mwanamke anaejitambua hatoweza kufanya hilo katu....btw kwanini unifikirie mkeo kwamba nina akili ya "kupooza machungu"? waaminini wake zenu jamani sio kila mke ana akili ya kipoozeo.
 
hiyo ni tatizo ambalo nalitegemea, lakini mkuu haiwezekani wazazi wawili uhusiano ukafa kabisa?mapenzi yasiwepo wakaangalia ulezi wa wanao tu?
Ule urafiki wa wazi wazi unakuwa umekufa, ila ukisikia anakwenda kwao, na njiani wakakutana, jamaa akigusia tu, binti sio rahisi kukataa kwa sababu waliishavuliana nguo.

Na siku mkikorofishana jambo ambalo ni kawaida, anaanza kumkumbuka huyo jamaa yake, akikwambia naenda kwetu kupumzika, ujue anaenda kwa huyo jamaa.
 
Jamani wala hata haihusu eti kwa vile wamezaa pamoja ndo mapenzi hayaishi! Thubutu nkitu umekubore to the maximum na huwenda ukawa umekutesa sipati kukwambia halafu unieleze eti mapenzi bado yapo kwa vile umezaa naye mtoto? No way
 
Ndoa ni taasisi complicated sana tangu enzi za kale,kuna watu wanajuta kwa nini walioa/olewa na mtu mwenye watoto tayari na kinyume chake. Pili haimaanishi kwamba ukioa/olewa na mwenza fresh mambo yatakuwa shwari.

Hata kama asali haina makombo,ridhiko la moyo ni muhimu zaidi.
 
Mkuu kama ungeuliza kuoa mwanamke aliyekwisha olewa hapo ningekuwa na ushauri negative...! Unajua ndoa ikiwa mpya ile kitu mtu anaitimba kishenzi.....ingekuwa Big G ingekuwa hoi tepe tepe...!

Mh kazi ipo jamani kuna wengine huwa wanafall kwenye wrong hands sasa kama mwanamke ameolewa na mtu ambaye kwa kweli hawakuwezana kisha akaamua kuachana naye then unawezaniambia akimpenda asimuoe kisa aliwahi kuolewa? chunguza kwanza alichopelekea kutoka/achika kwenye nda yake then judge with your own heard na si kumjudge kwa nje!!

Mbona wanaume walioacha wake zao wanaoa tu?!
 
Inategemea na uhusiano alionao na baba wa binti wake na vile vile umri wa binti huyo. Kwa vyovyote vile itabidi ujitayarishe katika miaka ya baadae ku deal na baba, mashangazi, wajomba na ndugu zake huyo binti ..wakati mwingine inakuwa ngumu sana.

Vinginevyo kama umependa ww chukua mzigo atleast anazaa!!
 
Ule urafiki wa wazi wazi unakuwa umekufa, ila ukisikia anakwenda kwao, na njiani wakakutana, jamaa akigusia tu, binti sio rahisi kukataa kwa sababu waliishavuliana nguo.

Na siku mkikorofishana jambo ambalo ni kawaida, anaanza kumkumbuka huyo jamaa yake, akikwambia naenda kwetu kupumzika, ujue anaenda kwa huyo jamaa.

jamani jamani, du! huwezi amini kama mtu mzima anaweza fikiria hilo!
 
Mh kazi ipo jamani kuna wengine huwa wanafall kwenye wrong hands sasa kama mwanamke ameolewa na mtu ambaye kwa kweli hawakuwezana kisha akaamua kuachana naye then unawezaniambia akimpenda asimuoe kisa aliwahi kuolewa?

Hiyo ipo mkuu............wengi tu waliachika wameolewa tena....ni part ya life! Ila duh hako ka-ukweli......cha kutimbwa timbwa kindoa-ndoa kanaumisa roho ati....!
 
Kaka kaka nakushauri huyo aliyezaa achana naye kabisa ndugu yangu utafulia. Kulea mtoto wa mtu mwingine ni usumbufu mkubwa. Siku nyingine huyo baba yake atakuja kwako eti anakuja kumwona mwanae. Na mtoto akikua akikujua kwa babake haishi kiguu na njia kwenda huko kusimulia yako. Ukimrudi kakukosea, atasema kwa kuwa si babake. Likimtokea lolote baya atasema ningekuwa naishi na babangu isingekuwa hivi, shauri ya baba wa kambo. Na hata ukimfanyia mema vipi akafanikiwa, bado atarudi kumuenzi baba mzazi wakati wewe ndiye uliyelea.

Na ikiwa mtoto huyo kabaki kwa babake nawe ukachukua mke, hiyo ni balaa zaidi. Mke ni kila mara kiguu na njia kwa mzazi mwenzie kumwona mwanae. Na nakwambia watazaliwa wengine hapo home kwako na huyo bwana!

Kwa nini ujiingize kwenye usumbufu wote huo na wakati wasichana fresh kabisa wapo hawajazaa, wamejitunza kwa adabu na heshima wanasubiri mume? Huoni kuoa hiyo nung'aembe ni kama promotion kuwa hata wao wanafaa kuolewa kumbe hawafai?

Labda kama na wewe una mtoto bila ndoa, basi oa huyo mtaendana, na kila mtu atamvumilia mtoto wa mwenzie. Lakini kama na wewe hujazaa, usijiharibie heshima yako, achana na hilo nung'aembe.
 
mr linawezekana kabisa, nina mifano hai ya ma frnd zangu wa karibu, tena hata salamu hawapeani na hao baba watoto zao, inategemea kisa na mkasa mpaka wakatengana......

Nyamayao, Naomba nifafanulie ni visa gani hivyo ambavyo vitasababisha watengane kabisa na visa gani vitasababisha warudiane nikiwa naye, na kama kuna uwezekano nieleweshe ni njia gani nitatumia ku-block mahusiano yao yasiendelee upande wa mapenzi,ila kwenye suala la kumlea mwanao nafahamu siwezi zuia, ila nitashukuru kama ukinipa njia nzuri ya kuendeleza zoezi hilo, thanxs
 
Kaka nikuambie wazi, hakuna namna unayoweza ku-block uhusiano wa mtu na mzazi mwenzie unless uzao huo ulipatikana kwa ubakaji. Lakini kama yalikuwa maelewano, mwanamke hana uwezo wa kujitenga na mwanaume aliyemzalisha kwa hiari.
 
Kwa nini ujiingize kwenye usumbufu wote huo na wakati wasichana fresh kabisa wapo hawajazaa, wamejitunza kwa adabu na heshima wanasubiri mume? Huoni kuoa hiyo nung'aembe ni kama promotion kuwa hata wao wanafaa kuolewa kumbe hawafai?

Lakini kama na wewe hujazaa, usijiharibie heshima yako, achana na hilo nung'aembe.

Mkuu maneno mazito haya........! Huu sio ushauri....naona umemkaripia..! duh watu wabaya.....!
 
Kaka kaka nakushauri huyo aliyezaa achana naye kabisa ndugu yangu utafulia. Kulea mtoto wa mtu mwingine ni usumbufu mkubwa. Siku nyingine huyo baba yake atakuja kwako eti anakuja kumwona mwanae. Na mtoto akikua akikujua kwa babake haishi kiguu na njia kwenda huko kusimulia yako. Ukimrudi kakukosea, atasema kwa kuwa si babake. Likimtokea lolote baya atasema ningekuwa naishi na babangu isingekuwa hivi, shauri ya baba wa kambo. Na hata ukimfanyia mema vipi akafanikiwa, bado atarudi kumuenzi baba mzazi wakati wewe ndiye uliyelea.

Na ikiwa mtoto huyo kabaki kwa babake nawe ukachukua mke, hiyo ni balaa zaidi. Mke ni kila mara kiguu na njia kwa mzazi mwenzie kumwona mwanae. Na nakwambia watazaliwa wengine hapo home kwako na huyo bwana!

Kwa nini ujiingize kwenye usumbufu wote huo na wakati wasichana fresh kabisa wapo hawajazaa, wamejitunza kwa adabu na heshima wanasubiri mume? Huoni kuoa hiyo nung'aembe ni kama promotion kuwa hata wao wanafaa kuolewa kumbe hawafai?

Labda kama na wewe una mtoto bila ndoa, basi oa huyo mtaendana, na kila mtu atamvumilia mtoto wa mwenzie. Lakini kama na wewe hujazaa, usijiharibie heshima yako, achana na hilo nung'aembe.

Mkuu hapo kwenye wanawake fresh,niliona bado mbona kuna tatizo,ndoa nyingi zinafungwa za wanawake fresh ila pia ndo zinaongoza kwa matatizo,nadhani ukiangalia upande wa ndoa yenye tatizo naweza sema hata hao wasichana fresh huto-oa,cha muhimu zaidi ufahamu changamoto zitakazokukuta na jinsi gani utaweza zikabili,mtu mwenye busara akimbii matatizo bali utafutia majibu sahihi ya hayo matatizo,ndo maana nimeliwakilisha suala hili kwa great thinkers,nina mtoto wa nje ya ndoa,nakua muwazi kwenye kulijadili hili nipate jibu sahihi
 
Kaka kaka nakushauri huyo aliyezaa achana naye kabisa ndugu yangu utafulia. Kulea mtoto wa mtu mwingine ni usumbufu mkubwa. Siku nyingine huyo baba yake atakuja kwako eti anakuja kumwona mwanae. Na mtoto akikua akikujua kwa babake haishi kiguu na njia kwenda huko kusimulia yako. Ukimrudi kakukosea, atasema kwa kuwa si babake. Likimtokea lolote baya atasema ningekuwa naishi na babangu isingekuwa hivi, shauri ya baba wa kambo. Na hata ukimfanyia mema vipi akafanikiwa, bado atarudi kumuenzi baba mzazi wakati wewe ndiye uliyelea.

Na ikiwa mtoto huyo kabaki kwa babake nawe ukachukua mke, hiyo ni balaa zaidi. Mke ni kila mara kiguu na njia kwa mzazi mwenzie kumwona mwanae. Na nakwambia watazaliwa wengine hapo home kwako na huyo bwana!

Kwa nini ujiingize kwenye usumbufu wote huo na wakati wasichana fresh kabisa wapo hawajazaa, wamejitunza kwa adabu na heshima wanasubiri mume? Huoni kuoa hiyo nung'aembe ni kama promotion kuwa hata wao wanafaa kuolewa kumbe hawafai?

Labda kama na wewe una mtoto bila ndoa, basi oa huyo mtaendana, na kila mtu atamvumilia mtoto wa mwenzie. Lakini kama na wewe hujazaa, usijiharibie heshima yako, achana na hilo nung'aembe.

khaa mabinti fresh wapo kona gani?..na ukumbuke kuna abortion pia, sasa cjui coz wamefanya abortion ndio wapo fresh....halafu kuoa/kuolewa haiangalii tu u fresh/sura/umbo nk...kuna zaidi ya hayo....huyu unamwita nungaembe wewe wa kwako una hakika yupo fresh kama unavyodhani/fikiri?....utakuwa bado wewe ungejua binadamu kuitwa mama/baba ilivyo na utamu wake ucngemuongelea huyu dada kwa kumwita nungaembe....
 
hivi nitaendaje tena kwa huyo baba mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine hakutaka/hakupenda kunioa bali kunizalisha tu?...ukute baba mtoto kashaoa, mie nimekorofishana na wewe niende kupooza kwake kha! kwa mwanamke anaejitambua hatoweza kufanya hilo katu....btw kwanini unifikirie mkeo kwamba nina akili ya "kupooza machungu"? waaminini wake zenu jamani sio kila mke ana akili ya kipoozeo.

Mrs, wapo, tunaongeea uzoefu, au nikutajie list ya wanaonitongoza kwa kisa cha kutafuta mapozeo? LOL akili hizo wanazo sana tu Mrs
 
..huyu unamwita nungaembe wewe wa kwako una hakika yupo fresh kama unavyodhani/fikiri?....utakuwa bado wewe ungejua binadamu kuitwa mama/baba ilivyo na utamu wake ucngemuongelea huyu dada kwa kumwita nungaembe....

Mkuu punguzeni jazba....! Tujaribu kutoa ushauri zaidi.....tusibishane kupitiliza..!
 
Kaka nikuambie wazi, hakuna namna unayoweza ku-block uhusiano wa mtu na mzazi mwenzie unless uzao huo ulipatikana kwa ubakaji. Lakini kama yalikuwa maelewano, mwanamke hana uwezo wa kujitenga na mwanaume aliyemzalisha kwa hiari.

KIFARU amekwambia ilikuwa ni hiari?
 
Mkuu punguzeni jazba....! Tujaribu kutoa ushauri zaidi.....tusibishane kupitiliza..!

kaka umenisoma vibaya.....cbishani kabisa bali tunaeleweshana, na maneno aliyo2mia huyo kumwita huyu mama nungayembe sio ya kistaarabu kabisa.
 
Back
Top Bottom