Wana JF Hebu Niambieni Hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana JF Hebu Niambieni Hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kwetumbali, Oct 11, 2010.

 1. k

  kwetumbali New Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi nini hasa nchi hii inahitaji?Msije kuniambia siasa na uongozi maana woooooooooooooote wezi!
  Nimeuliza hili swali watu wengi sana ila sijapata jibu zaidi ya kuzunguka zunguka.Nimekuja hapa nisikie mnasemaje kwa hili.I mean alllllllllllllllllllllllll are not clean.Am confused!!
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,061
  Likes Received: 24,064
  Trophy Points: 280
  Nchi inahitaji umpigie kura yako Dr. Wilbroad Slaa kwa maendeleo ya Taifa! Usisahau hilo, kamwambie na mkeo, nduguzo, majirani na wengine wote!
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Anasema alllllll are nor clean akimaanisha kuwa hata Dr Slaa naye hayuko clean.
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  nchi namhitaji slaa awe rais
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nchi inakuhitaji wewe kama allllllllllllllll are not clean!
   
 6. dazenp

  dazenp Senior Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  that includes you kuwa your not clean as well.............the fact remains that tunataka Maendeleo Usafi wa mtu ni muhimu hatukatai ni jambo la msingi ila je do you need Usafi bila maendeleo?...............jiulize ukipata jibu......Jibu tarehe 31 October 2010
   
 7. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Nafikiri tunahitaji vita kidogo ili tutiane akili......otherwise tukipata rais mjeshi msomi asiye na stori nyingi...kidogo itakuwa much better.....nasema haya sababu sioni hata mmoja mpaka sasa ambaye ni kweli anaweza akaleta mabadiliko yeyote zaidi ya unafiki na njaa....yaani hakuna lazima tukubaliane sababu kwa jinsi mfumo wa maisha ulivyo ukishaingia ikulu tu taratibu zote zinabadilika....
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....sasa unataka wanaJF wakuambie nini wakati umesha-conclude................sana sana tutakuambia wewe ndio unahitaji kubadilika na hiyo attitude..................hivi unategemea utakutana na mwanadamu aliye perfect?...................hivi unaelewa maana ya mfumo wa Uongozi/Utawala wa Sheria.................
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa as a fifth Prezdaa
   
 10. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "Associate yourself with men of good quality if you esteem your own reputation. It is better be alone than in bad company."
   
 11. P

  PWAGU Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  chagua slaa kwa maendeleo ya makanisa
   
 12. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135


  chagua kikwete kwa maendeleo ya familia yake........
   
 13. R

  RMA JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :bolt::wink2:Nchi hii kwa sasa inamhitaji Dr Slaa! :wink2::bolt:

  Dr Slaa Yes We can!

  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.:loco:


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!:loco:


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..:spider::A S 465:


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? :director:


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious! :rain::alien:


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?:music::rain:


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :hat::rain::director:


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.


  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. :spider:


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..:rain::bolt:
  [FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]
   
 14. THE BRAIN

  THE BRAIN Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sasa hapo tena aseme amezungushwa! hilo ni jibu tosha kabisa "Let us vote for CHADEMA and select DR.SLAA" THE SECOND TANZANIAN AFTER NYERERE "YES WE CAN"
   
 15. J

  Jafar JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nchi hii inahitaji kumpigia kura Dr. Slaa
   
 16. A

  African Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Water cannot rise above its source . A community will get the leadership it deserves. Watu wabaya hawawezi kupata kiongozi mzuri na watu wazuri hawawezi kupata kiongozi mbaya-
   
 17. m

  magee Senior Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  we need liberty and emporwerment i.e empowering the weak with proper info. ........watu waelewe nini cha hitajika kupata Tanzania bora,maana tulivyo leo ni matokeo ya jana.Elimu ya uraia na liberty is all we need tukiwa na haya watu wataju nani wa kumpigia kura .
   
 18. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  hewalaaaa!!:loco::loco:
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  Wizi wa CCM tunaufahamu lakini wa upinzani hatuujui hivyo tuwape nafasi ya kuongoza ili nao tuwapime.
   
Loading...