wana JF ARUSHA Mliokwisha Kuoa/kuolewa; Ombi Langu la dhati kwenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wana JF ARUSHA Mliokwisha Kuoa/kuolewa; Ombi Langu la dhati kwenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by luvcyna, Aug 10, 2011.

 1. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Habarini wanajamvi wote lakini zaidi waishio Arusha,..
  Leo ninaleta ombi langu la dhati kwenu,. lakini kabla sijawasilisha nieleze kwanza kwa kifupi kilichonisukuma humu leo..
  Katika haya maisha inafika wakati inakulazima mwanaume/mwanaume kuishi na mwenzi wako na kuwaacha wazazi wako, hapo nami ndipo nilipofikia..katika kufikia uamuzi huo ni mengi mtu unaweza kupitia yanaweza kuwa mepesi au hata mazito kama ilivyo kwangu mimi.

  Ni muda umepita tangu nlipopita humu na kuomba ushauri kwenu kuhusiana na swala zima la kuomba ndoa toka kwa jamii ya niliyetaka kumuoa, ushauri niliopewa niliubeba kama ulivyo na kuchanganya na ya kwangu,nashukuru Mwenyez Mungu na wana jf kwa ujumla kwani katika hilo nilifanikiwa. Sasa nimefikia hatua ya kufunga ndoa,taratibu zote nimezifata now its final.
  But something so confusing came up... katika hatua niliyofikia nilihitaji mdhamini, nilimpata mfanyakazi mwenzangu, tukapanga itakavyokuwa kuanzia mavazi na mengine yote ya muhimu, katika hali isiyo ya kawaida,siku za ivi karibuni mkewe kabadilika na kusema hayuko tayari kudhamini ndoa yangu, sababu ni kuwa haoni kama anaendana na mke wangu mtarajiwa kimaumbile akiwa na maana urefu na upana wa mwili wake ni tofauti na wamke wangu mtarajiwa ilihali tulisha lijadili hilo na kuamua lisiwe kikwazo.

  imefika mahali sasa naomba msaada kwenu tena katika hili, kimawazo au hata nikimpata wa kunidhamini kutoka humu itakuwa ni jambo jema kwani muda unaelekea kuniishia sasa..najiona kama nimepatikana katika hili.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Upo katika dhehebu gani! Na je? Nimepita tu!
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Duu, headache kweli. Zaidi ya pole sina msaada hapo, labda atajitokeza -- tusubiri
   
 4. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Check just an imediate solutiƶn to rescure the situation
   
 5. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ongea na kaka PAKA JIMMY nadhani ameoa,lol....sema unatafuta bestman na matron wa mkeo ukisema mdhamini wengine wataingia mitini wakidhani ni mambo ya pesa lol
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  We Bwana mdogo! Lugha ni ngumu ama shida siyo yenyewe? Swali tena! Upo dhehebu gani hapa Arusha?
   
 7. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole sana,
  Kwa jinsi ninavyojua, wasimamizi wa ndoa ni mashahidi wa kwanza kushuhudia ndoa ilifungwa kihalali.
  Lakini zaidi ya hilo ni lazima kuwa muangalifu kuchagua msimamizi wa ndoa.
  Kwani yanapotokea matatizo baadae yakindoa, msimamizi huwa consulted kwa ushauri.
  Nakushauri, ni vizuri kuchagua mtu mzima na muelewa.
  Kutokana na muda mdogo ambao umebakia.
  Ila kama unawajua waumini wenzako vizuri unaweza kumkonsult yoyote akusaidie katika hili.
  Ni wazi ungependa mtu kijana, au unayejuana nae akusaidie hili.
  Lakini kutokana na unyeti wa swala hili si vizuri kuangalia kwa mtazamo huo kwani sio muhimu.
  Ikiwa unahudhuria mafundisho ya ndoa basi, unaweza kuongea na mwalimu wako anaweza kukusaidia.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  duh! Mi nilistuka nikafikiri mambo ya pesa kumbe siyo.
  Ngoja nije arusha nimdhamini.
   
 9. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  cheki na mzee mwanakijiji atakusaidia tu nina imani
   
 10. D

  Derimto JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Nadhani watu wengi wanaogopa gharama zisizo rasmi na ndiyo maana unakuta mtu anachukua mtu wa karibu ili anapoingia gharama inakuwa kama sehemu ya mchango wake na zaidi sana lazima mtu huyo awe pia mshauri wa mambo ya nyumbani na hicho ni kipaji zaidi siyo vya darasani kama MBA kwa maana hiyo basi ukikwama kabisa nipm na unijulishe harusi yako ni lini ili niangalie namna ya kukusaidia
   
 11. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Mimi nilifikiri hivyo. Hivi bestman na matron lazima wawe ni mtu na mkewe? Nilipooa mimi (a bit of ancient times) haikuwa hivyo. Nilitafuta bestman wangu na mke wangu akatafuta matron wake. After all its a one day thing.
   
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nije kushika maua? au ushapata watoto
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyie watu:
  Mmeangalia vizuri kichwa cha habari? Ngoja niwakumbusheni, hiki hapa:

  Wana JF ARUSHA Mliokwisha Kuoa/kuolewa; Ombi Langu la dhati kwenu.

  Sasa kama hujakidhi hivyo vigezo usichangie. Cha ajabu walio mstari wa mbele kuchangia ni wale ambao hawajaoa/kuolewa, tena wengi wenu hampo Arusha. Halafu mnamwambia atafute solution ya haraka, ama! hiyo solution ya haraka ndiyo anayoiomba...msimrudishie tena hicho hicho alichokiomba.

  Ushauri wangu sasa kwa mleta mada:
  Inategemea na dhehebu ulilopo lakini nijuavyo mimi haijalazimishwa kuwa wasimamizi ni lazima wawe mke na mume. Wanaweza kuwa ni watu wenye ndoa lakini si mke na mume....unajua kazi yao wale ni mashahidi tu kuwa ndoa hiyo ilifungwa na waliishuhudia, kwisha.

  "In a worst cenerio" inaruhusiwa kusimamiwa na hata mtu asiye na ndoa ama wa dini tofauti (hata muislamu). Inapendekezwa kuchukua watu wa dini yako na wenye ndoa ili wasiwe wageni wa taratibu za pale kanisani na taratibu za dini yenu kiujumla...vile vile ni rahisi kwao kuwa na ufahamu mkubwa juu ya masuala ya ndoa.
  Faida ya kusimamiwa na mtu na mkewe si zaidi ya hii kuwa endapo mtapata matatizo ya kindoa basi ni rahisi kuomba ushauri kwa wasimamizi wenu ambao mnaweza kuwapata kirahisi kwa pamoja. Yaliyobaki huwa ni "SHOW"
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,631
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha unataka kua flower girl? gauni unajinunulia lakini
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwani Mwanakijiji anapatikana Arusha??
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Jestina, mambo? si umeingia hapa juzi hata wiki mbili tatu bado, Paka Jimy umeshamfahamu? Daaaaah
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Nilidhani mke amekumwaga,kumbe hilo!!Mbona tatizo dogo sana hilo?Ahirisha ndoa tafuta msimamizi mwingine,haya mambo ndo maana huwa siyapendi!
   
 18. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  nashukuru wadau kwa michango ukizingatia na muda ulivyopaa, kama walivyosema wadau wengine woga wa gharama nadhani nami nimeliona hilo kwa wengi, as per mdau aliyeshauri nitafute toka kwa waumini wenzangu, mpaka kufika hivi sasa kila ninayekutana naye ananipa sababu mara mke wangu mzazi,mara nimefunga,na mengine til nimechoka, .. Kifupi tu nitakuwa tayari kugharamia yote ilimradi siku ipite na nifanikiwe katika hili,.nazidi kumwomba tu Mungu labda nitapata msaada, wacha nijaribu na wadau mliowapendekeza.. Nashukuru
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa hapo ulipofikia usiumize kichwa:
  Kama jamaa yupo tayari ila mkewe ndo ndo hayuko tayari basi fanya jitihada za kumtafuta matron mwingine then na huyo jamaa wote kwa pamoja wawasimamie. Kumpata matron jitahidi kumshirikisha zaidi mkeo mtarajiwa, nadhani huenda yeye akampata kirahisi kuliko wewe.
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi nipo dar ila naeza kuja kukusaidia sijaolewa lakini. si umepata wa kiume? nitasimama nae au?
   
Loading...