Wana jamvi namleta kwenu kamanda Esther Wasira; naomba tumpe ushirikiano

Esther Wasira,

Natumaini unamfahamu mtu anaitwa Kitila Mkumbo wa UDSM. Huyu mwombe ushauri kila upatapo fursa. Jitahidi pia kupata hekima za wazee kama kina Dr.W.Slaa, Prof. Baregu, Prof Safari na hata Freeman A. Mbowe

Unaoona nimewa-tag ni members wa JF tayari kwa majina yao. Kuna challenges za kutumia majina halisi, lakini tumia busara katika kujibu hoja zetu. Si kila hoja lazima ijibiwe, hata kimya wakati mwingine ni jibu.

Karibu JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kila tatizo unaloliona lina chanzo chake, kikubwa ni kushughulika na chanzo cha Tatizo na sio tatizo lenyewe;kufanya hivyo ni sawa na kulipalilia tatizo. Nikisema nina mkakati nitakuwa nadanganya, lakini naamini Uongozi wa juu wanajua hilo na wanashughulikia kwa level hiyo.

Sasa wangu Ester, inabidi tukafanye kweli Sumbawanga, ni sehemu muhimu sana kwako. Halafu pata muda uwaandikie waraka baraza kuu kuhusu usingizi wa BAWACHA. Kama BAVICHA tumeweza kuivunika UVCCM kwa nini sio BAWACHA kuivunika UWT
 
hiyo imekaa personal zaidi, naomba nisijibu tafadhali...
Kuna tofauti gani kiitikadi kati ya CDM na CCM?
Uonavyo wewe tofauti zipo kiutendaji zaidi au kiitikadi zaidi? ... kiutendaji namaanisha kuanzia sera mpaka ushughulikiaji wa sera.
Unafikiri, CDM ikipewa ridhaa na watanzania, itashughulikiaje matatizo hayo (ya kisera na uytendaji).
 
KARIBU ESTHER, NILIKUKUBALI SANA KT MDAHALO LAST WK, NAOMBA WEWE KM MWANAMKE UTWAMBIE UTAHUSAIDIAJE UMOJA WA WANAWAKE WA CHADEMA aka BAWACHA AMBAO KWA DHATI YANGU NAUONA UMEDOROLA, NA KM JUMUIYA HAUCHANGII PAKUBWA NA HATUPATI MCHANGO WAO KT VUGUVUGU LA MABADILIKO M4C NA HASA UKIZINGATIA WANAWAKE NI MOJA YA WACHANGIA USHIND WA MAGAMBA aka CCM, JIBU PLZ
 
Huyu tusimwite jembe maana naona cdm majembe yamekuwa mengi!! kwa nini huyu tusimwite MPINI!!!
 
Kamanda, nataka kujua kabla ya kujiunga CHADEMA ulikuwa mwanachama wa chama gani? Pia mimi binafsi naona unafaa kuwa mbunge wa kuchaguliwa; je, ungependa kugombea jimbo gani?

Kwanza nashukuru kwa kuniamini.. Sijahamia Chadema, Nimejiunga. Kuhusu Ubunge, huu ni Utumishi na kama jina linavyojielezea, mtumishi hutumwa, hivyo kama nitatumwa nitakwenda nitakapoelekezwa..
 
Mmh yasije yakawa ya Ms Sumari. Vinyonga wengi kwenye hili janvi ukivaa majani makavu wanakupepea, ukivaa majani mabichi wanatapika wakati sungura ni sungura awe mweusi, mweupe au anamadoadoa wote ni sungura.
 
kabla hujafika mbali tupe mpango wako,umeolewa au una jamaa au uko single ili tuanze kulenga au namna gani vipi?
Nakushauri kuwa Um-pm, usijifanye kama mbuzi aliyeingia kundi la ubeberu jana, ambaye kila mbuzi anayekatisha mbele yake anataka ajulikane kuwa amekuwa beberu na kwa ujinga huo yuko tayari kumparamia hata aliyemzaa au hata dada yake.
 
Habari Wana Jamvi,

Awali ya yote niombe radhi kwa kutofika mapema kuchangia thread hii, nilitumwa na mwajiri wangu nje ya eneo la kazi, sikuwa nimeona hii.

Asanteni sana kwa kunikaribisha kwa namna ya kipekee; I am truly humbled. Nimekuwa mfuatiliaji wa pembeni kwa muda mrefu lakini sasa hivi nipo humu miguu yote miwili.

Binafsi huwa nafurahishwa na uhuru wa kuchangia mawazo uliopo humu ndani, na nadhani kama kuna kiongozi anayetaka kujua anatakiwa abadilishe nini na wapi, awe anapita humu na anazingatia yote ya msingi yanayoongelewa na jamii yake. This is "Jamii Forums".

Ninashukuru kwa yote mema na mazuri yaliyosemwa juu yangu, maana yananipa nguvu za kusonga mbele, lakini pia nashukuru sana kwa yale ambayo hayaonekani kuwa mazuri au mema kwangu maana hayo hasa ndio yanayonijenga zaidi.

Thank you..

Karibu sana Kamanda. Vipi ukichukua jukumu la marehemu Rejia? I mean kuwa active member kwa kutupatia updates za matukio ndani ya chama kama alivyokuwa marehemu Rejia? Ni pendekezo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom