Wana JamiiForums wote ' tuliokwazika ' na Bondia Hassan Mwakinyo ' tumsamehe ' kwani hatimaye amemuomba Radhi ' Legend ' Rashid Matumlla

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,385
108,455
Nikiwa kama Mmoja wa Watu niliochukizwa kama siyo kukasirishwa na Kitendo Bondia Mwakinyo cha Kumdhihaki Bondia mwenye Historia iliyotukuka hapa Tanzania Rashid Matumla hadi GENTAMYCINE nikaanzisha Uzi wa Kumsema ambao uliibua Hasira Kali za Watanzania zilizosambaa sehemu mbalimbali hatimaye leo hii kupita Azam Tv Bondia Mwakinyo amemuomba Radhi Matumla na Watanzania wote kwa ujumla tukiwemo Mimi na Wewe.

Hivyo nasi hatuna budi Kiungwana kabisa Kumsamehe na Kuanzia sasa tuweke Silaha zetu chini na tumsaidie akue Kimchezo.

Kwa wale wenye Kumiliki Visimbusi / Vingamuzi vya Azam Tv leo Saa 3 na Nusu msikae mbali na Runinga zenu kwani kutakuwa na marudio yote ya tukio zima ambapo Bondia Mwakinyo alionyesha Heshima ya juu kwa ' The Legend 'Rashid Matumla huku Rashid Matumla nae akionyesha kuwa kweli Yeye ni Mkongwe na amekomaa katika Tasnia hiyo ya Ndondi nchini ambapo nae hakuonyesha ' Kinyongo ' na muda wote alikuwa akimkumbatia Kiupendo na Kumtia Moyo Bondia Mwakinyo hali ambayo inaonyesha kuwa Bondia Mwakinyo amejutia lakini pia amejifunza Kitu na sasa atabadilika.

Kwa wale ambao mlikuwa mnaudharau huu Mtandao wa JamiiForums fikirieni upya kwani kama hamjui na kwa taarifa yenu tu ni kwamba hakuna Mtandao wa Kijamii nchini Tanzania ambao unaibua mambo mengi na una ' Influence ' kubwa ndani ya Jamii ya Watanzania kama huu. Ni Maudhui na Maoni ya huu Mtandao hasa juu ya Uzi niliouanzisha na ambao wengi wenu mlichangia ndiyo umeweza Kuamsha ari kwa Watanzania wengi hadi Kupelekea na Waandishi wa Habari za Michezo nao Kufuata mtiririko na Uzi mzima hadi leo Mwakinyo ameamua Kusalimu Amri na Kuomba Radhi.

Katika hili kila mwana JamiiForums ni Mshindi hivyo unapokuwa hapa jione kuwa Wewe ni sehemu Kuu ya Mabadiliko Kijamii.
 
Kaomba radhi kwakuwa kalazimishwa aidha na wanaomsimamia au chombo cha habari cha Azam au wakongwe waliomwambia usipofanya hivyo basi pambano la juzi ndio litakuwa pambano ulilofanikiwa zaidi ktk ulimwengu wako wa masumbwi vinginevyo bado kibri anacho.
 
Kuomba msamaha ni uungwana, binafsi nimemsamehe kwa moyo mkunjufu kabisa.

Lakini pia Asante sana Popoma, kwa kusaidia kumrudisha dogo kwenye msitari kutokana na thread yako uliyoleta hapa JF.
 
FB_IMG_1575389092129.jpg

huyu mjinga Mwakinyo angekuwa na mikanda kama hii sijui angetukana wangapi , nimemdharau sana .
 
Mimi nilikua nascreenshort hapa comments nammwagia kwenye DM yake kule insta ajue moto kwa watu waelewa ulivo waka
 
Nikushukuru kwa kulianzishia maada lile suala maana limekua na impact kubwa sana kwetu na tukiamini dogo bado kijana mdogo sana kuanza kuonyesha dharau kwa watu wazima kama matumla
 
ebu tuonyeshe hiyo thread yako na utuelezee kinaga ubaga ni matusi gani aliyatoa hassan mwakinyo kwa matumla?

sio unabwabwaja kujimwagia sifa tuu as if na wewe una chuki zako binafsi.
 
Mimi nilikua nascreenshort hapa comments nammwagia kwenye DM yake kule insta ajue moto kwa watu waelewa ulivo waka

Hongera / Kongole sana na mno kwa hilo Mkuu. Na nina Uhakika ni nguvu ya wana JamiiForums ndiyo iliweza Kuamsha Hisia zile Kali hadi nchi nzima nayo ikalipuka na Bondia Mwakinyo Kushambuliwa hadi akajiona Mpumbavu na Kujirudi Kwetu hivi.
 
Mwakinyo achunge domo lake. He has to control his temper. I think he lacks some decorum.... He is uncouthed.... Bado ushamba unamsumbua
 
ebu tuonyeshe hiyo thread yako na utuelezee kinaga ubaga ni matusi gani aliyatoa hassan mwakinyo kwa matumla?

sio unabwabwaja kujimwagia sifa tuu as if na wewe una chuki zako binafsi.

Hiyo ya Kuutafuta huo Uzi ulipo siyo Kazi yangu Mimi bali ni Kazi yako Wewe Mpumbavu Mmoja kuifanya kwani ungekuwa na Akili Timamu tu huo Uzi upo katika Jukwaa la Michezo ( Sports ) leo Siku ya Tatu na bado Wadau wanaendelea Kuuchangia sasa nakushangaa unavyotaka Kubisha kuwa haupo au sikuuanzisha.

Na kukuonyesha kuwa GENTAMYCINE ni habari na kwamba ' Threads ' zangu mbalimbali hapa JamiiForums huwa zina ' Influence ' na ' Impact ' kubwa Kijamii na hadi huko Mamlakani ( Serikalini ) nilishaanzisha Uzi hapa kuhusu Ujenzi wa Daraja la Mto Wami na haikupita hata Miezi Mitatu Ujenzi wake ulianza. Na kama haitoshi miezi michache iliyopita tu hapa hapa nilianzisha Uzi wa Kumtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Afande Jenerali Mabeyo azuie mara moja Mnada ambao ulikuwa umetengewa eneo pale Kawe jirani na Ofisi za Dawasco na Posta huku ukitazamana na eneo la Mafunzo ya Jeshi kwa sababu za Kiusalama ambazo nilimpa na kweli ndani ya Siku mbili Kibao Kikubwa kikawekwa pale kuwa HAKUNA TENA MNADA HAPA na hadi leo kipo nenda ukakione.

Huyo ndiyo GENTAMYCINE ' Purely Talented, Charimatic Fella, Game Changer and Entartainer "
 
Aombe radhi wiki nzima kama tulivyomlazimisha kuomba msamaha wiki nzima kukulia Pwani isiwe tabu ya kujimwambafy na maneno bila break
 
Back
Top Bottom