Wana JamiiForums, muoneeni huruma 'Mzee wa Upako'!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Jana 'nilibahatika' kusikiliza mahubiri ya Mzee wa Upako kupitia Channel Ten!
Kwa kweli katika kuhitimisha mahubiri yake, mzee wa upako alionesha kuumizwa sana na maneno yanayoandikwa juu yake hapa JF na akasema amewakosea nini? Yani kufundisha maneno ya Mungu ndio imekuwa kosa.

Kwa kweli alionekana inside he is a broken man hadi nikamuonea huruma. Sasa kwa heshima na taadhima, ninawaomba wana JF tumpumzishe mzee wa upako angalau tusije kusika kajitia kitanzi kutokana na maneno na michango yetu juu yake...

Tumpumzishe kama tulivyompumzisha PM Majaliwa, maana naye alivyokuja speed na swala la Faru John likamtoa nduki mpaka sasa katulia tulii kama maji mtungini...
 
10809540_267354180055551_1574502767_n.jpg
 
Jana 'nilibahatika' kusikiliza mahubiri ya Mzee wa Upako kupitia Channel Ten!
Kwa kweli katika kuhitimisha mahubiri yake, mzee wa upako alionesha kuumizwa sana na maneno yanayoandikwa juu yake hapa JF na akasema amewakosea nini? Yani kufundisha maneno ya Mungu ndio imekuwa kosa.
Kwa kweli alionekana inside he is a broken man hadi nikamuonea huruma.
Sasa kwa heshima na taadhima, ninawaomba wana JF tumpumzishe mzee wa upako angalau tusije kusika kajitia kitanzi kutokana na maneno na michango yetu juu yake...
Tumpumzishe kama tulivyompumzisha PM Majaliwa, maana naye alivyokuja speed na swala la Faru John likamtoa nduki mpaka sasa katulia tulii kama maji mtungini...
Ni kweli ila tumpumzishe
Fumba macho...........apite
 
Huyu hata akijinyonga ni sawa tu maana anatuharibia na kutuchafua wakristo!
 
ZABURI 75

Itapendeza Sana Akijikita Kwenye Mambo Ya Kuchunga Kondoo Tu,Siasa Akiwa Kama Mkweli Asimame Kwenye Mstari Kukemea Lolote Baya Bila Kuweka Mahaba


Ukichanganya Siasa Na Dini Hasa Ukawa Mfano Una Kadi Ya Chama Fulani Ndiyo Unapanda Madhabahuni Kwaajili Ya Kuponda Chama Kingine Huku Ukijisahau Waumini Wako Wote Hawawezi Kuwa Chama Kimoja
 
Mungu hamfichi mnafiki, viongozi wengi huharibu wafuasi wao kwa kuwaaminisha kwamba wao walishakuwa safi. Kutamka maneno ya kwamba nikikuombea usipopona au kufanikiwa nitaacha kuhubiri na kwenda kuuza bangi, ni majivuno na majitukuzo makuu. MUNGU hapendi yeye alewe tu, aache tu kufika huku jf
 
mbona na yeye anatoaga mfano kanisani kwake kuhusu waumini aliokutana nao na maisha yao

wacha na sie tu'mfano'e sasa

[HASHTAG]#mzeewaKITWANG[/HASHTAG](A)IO
 
Kama hayafanyi yanayojadiliwa humu imemuuma nn? Aache maneno na jirani zake atupige sara tuu!!akiyafuata ya humu kondoo wote watamtoroka Mubashara mchana kweupeee!!
 
Kwa hiyo sasa hivi anaomba poo....Vipi ule msemo wake maarufu.."watashindanaaaaaa" umefua dafu ehhh..
 
Hajui tu, magazeti ndo yanamsema, hebu soma hii.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Dar es Salaam, Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako, amekamatwa na polisi akituhumiwa kumfanyia fujo na kutishia kumuua jirani yake.

xab.jpg.pagespeed.ic.Kghj235SlH.jpg


Tukio hilo lilitokea juzi maeneo ya Kawe wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa tatu alipochukuliwa na polisi wa Kituo cha Kawe.

Taarifa za mchungaji huyo kufanya vurugu, zilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, huku video aliyorekodiwa eneo la tukio, ikimuonyesha akiongea huku akionekana kama aliyelewa chakari.

Wakati wa tukio hilo, Mchungaji Lusekelo alikuwa ameegesha gari lake barabarani kiasi cha kusababisha usumbufu na foleni ya magari mengine.

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa ni kulipiza kisasi kwa jirani zake hao wanaoishi katika nyumba namba KAW/MZN/1348, ambao alidai wamekuwa wakimkebehi kuwa hafai kuwa mchungaji kwa sababu ya ulevi.

Licha ya baadhi ya watu kumsihi aondoke eneo hilo kutokana na hadhi yake, mchungaji huyo alikaidi, huku akiendelea kuongea kwa sauti iliyofanana na mtu mwenye kilevi. Baadhi ya maneno yaliyosikika kwenye video hiyo tumeshindwa kuyaandika kutokana na maadili ya taaluma kwa kuwa si ya kawaida.

“Mjinga wewe, mimi ni zaidi ya askari na wewe ni mgambo, na si mgambo wewe ni raia tu.

“Umenitukana sana wewe mpaka leo nimeamua kuloana na mvua, usitoe gari hapo mshenzi sana wewe, na nikikuona mahali popote…, mshenzi kabisa, muangalie sana huyo,” alisikika Mchungaji Lusekelo akiongea kwa sauti.

Baada ya kuongea maneno hayo, ilisikika sauti ya mwanamke kutoka ndani ya uzio wa nyumba hiyo ikimjibu mchungaji huyo: “Huwezi, aniangalie kitu gani.”

Hata hivyo, hata watu mbalimbali walipomsihi aache kutoa lugha hizo za kejeli na aondoe gari lake lililokuwa limesababisha foleni, alikataa akisema hataliondoa hadi atakapokuja Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.

Baada ya purukushani hizo, polisi kutoka katika Kituo cha Kawe walifika eneo hilo saa tatu asubuhi, wakamchukua mchungaji huyo na kumpeleka kituoni. Inadaiwa baada ya kufikishwa kituoni hapo, mchungaji huyo alipimwa kiwango cha ulevi na kukutwa 131, ambacho kinaelezwa kuwa ni kikubwa ulevi wa kupindukia.

Ilipofika saa tano asubuhi, mchungaji huyo alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central), ambako huko nako inadaiwa alipimwa kilevi na kuonekana kushuka hadi kufikia 121.

Gazeti la Mtanzania lilipomtafuta Kamishna Sirro ili kuzungumzia sakata la mchungaji huyo, alisema atalizungumzia leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Juni 5, mwaka huu, Rais Magufuli alikwenda kusali katika kanisa la Mchungaji Lusekelo na kuahidi kumjengea barabara inayoingia kanisani hapo.

CHANZO:MTANZANIA
 
Back
Top Bottom