Wana jamii hivi ukisema unataka upinzani imara unamaanisha nn? Upinzani ufanye nn ili ww uuone imara.

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Unaongelea upinzani imara, na kusema hakuna upinzani imara.. Well, upinzani imara una instincts zipi? Upinzani imara unapaswa kufanya lipi ambalo lina thibitisha uimara huo? Unasema 'hakuna upinzani imara' kwani lipi lenye kupaswa kufanywa na 'upinzani' dhidi ya chama dola na upinzani haufanyi?

Wapinzani wameibua hoja nyingi sana (naweza kutaja), wapinzani wameikosoa serikali, wapinzani wametoa dira na mipango mbadala ya maendeleo, wapinzani wametoa randama ya bajeti mbadala dhidi ya bajeti kuu ya serikali, wapinzani hawa ambao unasema sio imara, wameiwajibisha serikali mara kadhaa na Tanzania nzima ikashuhudia..

Well.. Unasema hakuna upinzani imara.. Unafikiri kwanini CCM sasa wameamua kuwa 'chama dola?' yaani wamefungamanisha siasa zao sasa na utawala? Hoja za wapinzani sasa zinajibiwa na dola na vyombo vyake na sio CCM (chama kilichopewa ridhaa), hakuna ulingo wenye uwiano kufanya siasa, hofu ya watawala dhidi ya upinzani ni kubwa.. Hauoni hilo?

Unasema hakuna upinzani imara wakati upinzani 'unavunjwa kwa hila na fedha za hongo na rushwa ya hadharani?' hauoni hayo? Unasema hakuna upinzani imara wakati wanasiasa Wa upinzani leo wanauwawa hadharani na kutekwa na kupigwa risasi kwa sababu tu ya hojaji zao dhidi ya mfumo wa utawala na watawala.. Ah hayo pia hauyaoni?

Unasema hakuna upinzani lakini' wakati huo' wanasiasa wa upinzani wanafukuzwa bungeni, wanafungiwa kutohudhuria vikao mwaka mzima.. Kama hakuna upinzani, hii tuite 'fear of unknown?' ok! Unasema hakuna upinzani, lakini MWENYEKITI WA CCM kwenye mwamvuli wake wa urais, anapiga marufuku shughuli za kisiasa, hii ni hofu ya nini kama upinzani imara haupo? Nashindwa kuendelea kuandika...

Mijadala dhalimu sana hii..

[HASHTAG]#MMM[/HASHTAG]
 
Wanataka waunge juhudi za muheshimiwa raisi ndiyo waonekane kuwa ni wapinzani kama John momose cheyo kwa ccm huyo ndiyo mpinzani.
 
Back
Top Bottom