Wana Iringa mjini, Njooni tujadili maendeleo ya Jimbo letu

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,404
9,234
Habarini wandugu,

Iringa mjini kwa sasa inakua ila kwa kasi ndogo ukifananisha na miji mingine. Hali ya kiuchumi ni sawa tu na mikoa mingine na hii inatokana kubadilibadilika kwa Uchumi wa nchi.

MIUNDOMBINU KWA UJUMLA:

Hali ya barabara zinazounganisha mitaa bado sio nzuri, barabara nyingi ni vumbi tupu na makorongo na isitoshe tupo kipindi cha mvua, hali kadhalika barabara kuu iendayo Dodoma ndio hiyo ipo kwenye matengenezo.

Hali ya maji na umeme sio tatizo sana kwa maeneo yenye idadi kubwa ya watu ila kwa sehemu kama Nduli na vijiji vya kigonzile, na Ugele maji badi ni tatizo sugu.

HALI YA USAFI:

Hapa napingana na Meya wetu anayeuhadaa umma kuwa Iringa Manispaa ni ya pili kwa usafi... Nimetembea maeneo mengi kiukweli maeneo mengi bado ni machafu na taka zimelundikana tu.

Hali ya UKIMWI:

Licha ya kuwa na utitiri wa NGOs zinazishugulika na masuala ya UKIMWI, UKIMWI bado umeendelea kukua kwa kasi hali inayitishia uhai wa jamii.

SIASA:

Hali ya siasa ni ya kawaida kama ilivyo maeneo mengine yenye Demokrasia.

WAFANYABIASHARA NA JAMII:

Wafanyabiashara wakubwa wa hapa bado sijaona umuhimu wao katika kusaidia huduma za kijamii zaidi ya kuwatumikia tu wanasiasa.

Karibuni Jamani
 
Huyo meya ni kikwazo cha maendeleo kwani hana upeo wa kutosha isitoshe anafanya makusudi kwa kuwa mbunge anatoka upinzani.

Inasemekana kuwa yeye kwa kushirikiana na mwenyekiti wa CCM Mkoa wanafanya makusudi kutokutekeleza na kuhamasisha maendeleo ili upinzani uonekane haufai.

Fitina za mwenyekiti wa CCM mkoa, Lukuvi na Pindi Chana ndizo kikwazo cha maendeleo ili kumkwamisha mpambanaji wenu wa CHADEMA. Dawa yao ni ndogo sana, wachagueni CHADEMA kwa wingi 2015 ili kuchochea kasi ya maendeleo.
 
Tumuondoe kwanza mchungaji Msigwa kwenye Ubunge ndio maendeleo yatapatikana
 
Huyo meya ni kikwazo cha maendeleo kwani hana upeo wa kutosha isitoshe anafanya makusudi kwa kuwa mbunge anatoka upinzani.

Inasemekana kuwa yeye kwa kushirikiana na mwenyekiti wa CCM Mkoa wanafanya makusudi kutokutekeleza na kuhamasisha maendeleo ili upinzani uonekane haufai.

Fitina za mwenyekiti wa CCM mkoa, Lukuvi na Pindi Chana ndizo kikwazo cha maendeleo ili kumkwamisha mpambanaji wenu wa CHADEMA. Dawa yao ni ndogo sana, wachagueni CHADEMA kwa wingi 2015 ili kuchochea kasi ya maendeleo.

Kweli mkubwa hilo hata mimi nimeliona hawampi ushirikiano kabisa mbunge.
 
Tumuondoe kwanza mchungaji Msigwa kwenye Ubunge ndio maendeleo yatapatikana

Kamuondoe kwanza Samwel Sitta anamiaka zaidi ya 30 jimbo lake lipo taabani hakuna maendeleo yoyote ukimaliza hapo nenda kwa Kapuya alafu malizia kwa Nkumba ndiyo urudi hapa kutuaminisha ushenzi wako
 
kwa kifupi
iringa imeendelea kwa ujumla wake,
si kama zama zile wakati vyuo havijaanza.
Kama fitna za kisiasa zikiwekwa kando kuna uwezekano wa iringa kupaa zaidi ki-maendeleo.
Mkoa una fursa nyingi ambazo ni bikra kabisa.
 
Na siku wanairinga mkamchagua Pindi au Jesca msimbachaka kwa kisa cha kuliresha jimbo ccm mtavuna ya mama mbega mara dufu. Hao hawana sifa ya kuwa viongozi kwani wanakosa ubunifu. Tamaa zao zitawatia umaskini. Achaneni nao mmrudishe mchungaji msigwa na mmjazie madiwani wa kutosha waishike na kuiongoza manispaa kama iringa haijabadilika kuwa jiji basi. Shida ni akili ndogo kuongoza akili kubwa utatarajia maendeleo?. Mwamwindi ni zigo na mchungeni salim asas kwa jinsi anavyojitengeneza yasije kuwa ya kina abood!.
 
Iringa ingekuwa mbali sana kimaendeleo. Kikwazo CCM ambao wana mawazo mgando.Wanafikiiria maslah yao tu kuliko maslahi mapana ya wananchi na taifa kwa ujumla
 
Kwa kusema ukweli ccm wanatumia sana umaskini wa mtu kumkandamiza zaidi. Hawajali kabisa. Binafsi nimekaa miaka 20 hapo manispaa na kwa bahati mbaya nawafahamu mno viongozi wa ccm wa mkoa na hata manispaa kwenyewe kwa jinsi walivyo na elimu ndogo isiyoweza kumwongoza yeyote katika maendeleo. Leo hii kuna vyuo vingi mjini hapo na vimejaa wasomi wa kila nyanja lakini hao kina Jesca na mwamwindi hawawasogelei ili kuchota taaluma zao katika kuhamasisha maendeleo. Iringa ina raslimali watu wa kutosha kama watatumika ipasavyo maendeleo yangetisha. Ccm wakikabidhiwa huo mji mmekwisha kwani waarabu wataendelea kuwatia umaskini. Ikataeni kwa nguvu zote.
 
Chadema MBONA mnatukana mtu akitoa hoja inayogusa ukweli? cha msingi hapa siyo kutukana ila ni kutoa proof ya hoja yako. Mtu mjinga hujihami kwa matusi na makelele ili kuficha ignorance yake, mwenye hekima husikiliza hata maneno ya kichaa na kuyachambua na pia kuyafanyia kazi.
Leteni hoja iayoonsha meya anakwamisha maendeleo Iringa mjin ili wenye ubongomkubwa wa analyse
 
Napata shida nikiona mji mchafu na pia kuna maeneo ambayo yanaendelezwa barabara hazijapasuliwa, barabara katikati ya mji hasa Kihesa Idunda ni makorongo tu, hakuna calverts hovyo hovyo tu kama hatuna meya wala Mbunge hivi ndio vitu vya kujadili kwa uwazi nani tatizo hapa? kama ni meya fine apigwe chini si diwani tu huyu? kama ni mbunge apigwe chini tumpe kazi mwingine nae ndani ya miaka mitano akishindwa piga chini mpaka tuone maendeleo yetu yako vizuri.

Ila matusi sipendi
 
Back
Top Bottom