Wana CHADEMA tumeshamchoka Lowassa. Hafai na hana thamani tena chamani

Kada wa CHADEMA

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
289
615
Siamini Lowassa huyu ndiye yule tuliyeaminishwa na Mwenyekiti wetu kuwa ana kundi kubwa la wafuasi wanaomuunga mkono.

Siamini kuwa Lowassa huyu ndiye yule ambaye tuliambiwa kuwa pindi tu atakapojiunga na CHADEMA angekuja na wenyeviti wa mikoa na wilaya kibao wa CCM.

Siamini kama Lowassa huyu wa sasa ndiye yule ambaye tuliambiwa kuwa wabunge wa CCM kwa idadi kubwa wataachia chama chao na kujiunga na chama chetu.

Siamini kama Lowassa huyu ndiye yule aliyekuwa anasababisha mafuriko kila alipopita.

Siamini kama Lowassa huyu ndiye yule aliyesimamisha miji kadhaa pindi alipowasili.

Siamini kama Lowassa huyu ndiye yule ambaye alisababisha vijana wengi wadeki barabara ili rais mtarajiwa apite sehemu safi na salama.

Siamini kama Lowassa huyu ndiye yule ambaye kila alipopita watu nyomi. Na tena siamini kama Lowassa huyu ndiye yule aliyepambwa na akina Molemo kuwa atatingisha Jiji la Mwanza pindi atakapowasili Mwanza.

Ninachoamini ni kuwa Lowassa huyu ndiye yule aliyekataliwa na CCM na tuliyemnadi kwa zaidi ya miaka nane kuwa ni fisadi.

Naam, Lowassa ni fisadi na ndo maana viongozi wetu wanashindwa kusimama jukwaani na mabango ya kupinga ufisadi.

Hakika kilichotokea ni kinyume. Wana Mwanza walitulia tulii kabisa na hakuna aliyeshtushwa na ujio wa Lowassa.

Hii imenipa wasiwasi sana kuwa wana CHADEMA kindakindaki tayari tumeshamchoka huyu mzee na tunatamani CHADEMA yetu ya enzi za Dr Slaa irejee.
 
Mliingizwa chaka na mwenzenu akachukua salio lake,chezea mbowe wewe na kwa sasa hamuwezi kkumtoa ng'o hela zake mtafanya nini
 
Wewe thamani yako ipo ccm tu maana kazi yako ni kufanywa ngazi na wapenda kula,kipofu mkubwa wewe
1457761906667.jpg
 
Back
Top Bottom