Wana CHADEMA bado tunayo kazi ya kuwaelimisha watanzania haki zao na wajibu wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CHADEMA bado tunayo kazi ya kuwaelimisha watanzania haki zao na wajibu wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, Oct 1, 2012.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanachama , wapenzi na mashabiki wa CHADEMA salamu,

  Ndugu zangu popote pale ulipo kama mtanzania, mwanachama wa CDM hasa wale ambao wale Mungu ametupa nafasi ya kupata kaelimu bado tunayo kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania wenzetu na kuwatoa kwenye usingizi mzito waliolala.Nimesema waliopata nafasi ya kwenda shule hata kama ni darasa la saba angalau kidogo unaweza haki zako kama raia wa Tanzania. Nasema bado tuna kazi ya kuwakomboa watanzania kwa kuwaelimisha na kuwaeleza kweli ya hali inayoendelea katika nchi yetu.

  Ndugu nawaomba sana tuache kupoteza muda wetu na nguvu katika kujibu na kuchangia hoja dhaifu za magamba na ndugu zao.Hivi kwa mfano mtu kama Mtatiro na wanachama wake walipigwa mawe huko A town wiki hii halafu anasema wafuasi wa CDM wamewapiga mawe,hivi kweli huyu ni msomi wa UDSM chuo kinasifika kwa kuzalisha wataalam wanaofikiri na "kuargue" critically? Na hapa kuna maswali ya msingi ya kujiuliza hivi watu waliowapiga mawe walikuwa na alama yoyote iliyowatambulisha kuwa ni wanachama wa CDM?Na je huko Arusha kuna chama cha CDM peke yake? Au ndo ndoa yao na CCM kwa hiyo hawawezi kuwarushia mawe.Ngoja na mimi nisingie kwenye mkumbo wa kujadili hoja dhaifu.

  Ndugu zangu kuna watu wanaleta hoja za ajabu na dhaifu humu watu kama akina ritz, zomba na wenzao.Tusipoteze muda na nguvu kujadili hoja za watu kama hawa,tutumie muda na nguvu kutoa ushauri kwa viongozi wetu,ikiwezekana tumtafute Tumaini Makene kama inawezekana atupe email address ambayo tutaweza kutuma ushauri na criticism kwa viongozi jambo ambalo litasaidia katika kukuza chama.

  Ndugu zangu tuwe tunazipotezea hoja dhaifu labda pale tunaona inatulazimu kuchangia na kujibu hoja zao.
   
Loading...