Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 45
Waandishi Wetu
Daily News; Monday,August 25, 2008 @00:02
Kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, kupinga uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwekeza fedha inayotokana na malipo ya Akaunti ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika kuinua kilimo, imeshutumiwa na baadhi ya wananchi.
Wananchi hao wamesema hatua hiyo ni ya kushangaza na kuhoji siasa za baadhi ya viongozi wa upinzani nchini akiwamo Dk. Slaa. Katika mahojiano na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mohammed Abdul alisema kauli ya Slaa inathibitisha jinsi wapinzani wasivyoelewa siasa za nchi, maslahi ya wananchi na matakwa ya walio wengi.
Hii ni nchi ya wakulima na wafanyakazi, sasa kuna ubaya gani kutoa fedha kuwasaidia wakulima ambao tunasema uti wa mgongo wa nchi yetu unaotegemea kilimo? Slaa aseme jingine, lakini si hili, alisema Abdul jana akiwa katika maandamano ya wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Kauli ya Slaa ni matusi kwa mamilioni ya wakulima wa nchi hii wanaohitaji kila aina ya msaada kuhimili dhiki zao. Na kwa maoni yangu, ni viongozi kama Rais Kikwete na hatua zake wanaoweza kuwasaidia wakulima kuondokana na hali zao za sasa, alisema mwananchi huyo.
Naye Mussa Ibrahim ambaye anaishi Temeke, alisema bila ya shaka baadhi ya viongozi wa siasa nchini wanachanganya mambo na hawaonyeshi uchungu na wananchi kama wanavyodai. Bila kilimo, Tanzania haiwezi kwenda. Hatuwezi kupiga hatua katika uchumi kama mkulima wetu ataendelea kuwa wa hali ya chini.
Sasa Rais Kikwete anachukua hatua, watu wanaanza kumpinga. Hivi kweli wana uchungu na wananchi wetu wakiwamo wakulima. Huu si ndio ukombozi wao, alisema. Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mary Alphonce, alisema kauli ya Dk. Slaa ni kielelezo kuwa baadhi ya wanasiasa nchini wametosheka, kwa kuwa tu wanazo fedha za kutosha, hivyo wanatoa kauli ambazo zinaonyesha wakulima kwao si kitu chochote.
Hawa si ndiyo wanaokaa bungeni na kudai maisha ya Watanzania yamekuwa magumu sasa Rais anatenga fedha kuwasaidia wakulima, wao wanasema anagawa fedha. Hivi afanye nini? Sasa ni aina gani ya uongozi ambao viongozi wanataka kuendelea kushiba na kuneemeka wakati wananchi waliowaweka madarakani tunaendelea kuwa masikini zaidi, alisema.
Naye Moses Elias wa Tabata, alimpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa busara kuiingiza fedha za EPA katika kilimo na ruzuku ya mbolea. Hizi fedha ambazo Rais ameziingiza katika kilimo, zitakuwa na manufaa zaidi kwa nchi hii hasa katika uzalishaji. Tuache kauli za siasa.
Ruzuku ya mbolea ni kwa Watanzania wote. Pengine Slaa hana shida kwa sababu ana uhakika wa posho ya bungeni, alisema Elias. Katika hotuba yake bungeni Alhamisi iliyopita mjini Dodoma, Rais Kikwete licha ya kueleza mafanikio ya serikali yake tangu iingie madarakani Desemba 2005, alielezea kwa undani hatua alizozichukua kuhusu suala la EPA.
Hatua hizo ni pamoja na kuamua kuwa fedha zote zitakazolipwa na wadaiwa, ziingie katika mifuko miwili maalumu, mmoja ukiwa ni kuongeza ruzuku ya mbolea kwa wakulima na ya pili ni kutumia sehemu ya fedha hizo kuongeza mtaji wa fedha za kukopesha wakulima katika Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Wananchi mbalimbali wameunga mkono hatua hizo, wakiwamo wakulima wa Songea waliokaririwa na gazeti hili jana pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walioandamana sehemu mbalimbali nchini kupongeza hatua hiyo ambayo kwa Slaa, anaiona haifai.