Wana CCM waliovamia chama msiba wao ni mkubwa zaidi. Vyeo walivyoahidiwa vimeyeyuka

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi, Wana CCM wa kuja au wavamizi wanaompinga Mama Samia Suluhu hawakutegemea mabadiliko ya ghafla ya kuondoa sera kandamizi.

Mimi ni mwana CCM. Kati ya mwaka 2017 mpaka 2020 Chama kilivamiwa na watu toka upinzani wakisema "Wanaunga juhudi za mwenyekiti wa CCM za kuleta Maendeleo".

Hawa wavamizi ndani ya CCM walimfuata mwenyekiti wa CCM tu bali hawakufuata itikadi na sera. Sasa Mwenyekiti hayupo.

Kundi la pili lilikuwa CCM maslahi au watafuta vyeo hawa kazi yao ilikuwa kusifu na kumpamba mwenyekiti wa CCM kwa kauli za "Aongezewe muda amefanya mambo makubwa toka tupate uhuru"

Hawa watu walijiona hii nchi ni ya kwao na hakuna mtu zaidi ya wao, Walitishia watu kwa mgongo wa mwenyekiti,

Hawa wavamizi waliamua kujitoa ufahamu na kupanga safu zao za uongozi ndani ya chama wakitegemea ataongezewa muda wa kutawala Mwenyekiti.

Unakumbuka kauli kama"Unaijua viete wewe?. Kama hamtaki kufuata sera zaCCM hameni nchi.

Makundi haya ndani ya CCM yameachwa yatima na wapweke sana, Sasa wamekaa kupinga sera za Mama Samia

Kila dakika wana CCM wavamizi wanahubiri Mama awabane wafanyabiashara, Mama aendeleze sera za chuki na kuligawa Taifa. Kitu ambacho kwa dini ya Mama Samia sio haki na hairuhusiwi.
 
Inaonekana watu wengi sana walikuchukizwa na utawala wa JPM na kumlilia Mungu wao ambaye amesikiliza sala yao. Bygone alikosea sana kunyang'anyana sifa na Mwenyezi Mungu! Kwa hatua ambayo wafuasi wake walifikia, mara kumfananisha na Yesu Kristo, mara wanamtaka Mungu ashuke kumshuru Bygone na yeye kuridhika tu bila kukemea ilikuwa ni self suicide.

Wapenda HAKI tutamtetea rais SSH kwa nguvu zote.
 
"Kundi la pili lilikuwa ccm maslahi au watafuta vyeo hawa kazi yao ilikuwa kusifu na kumpamba mwenyekiti wa ccm kwa kauli za "Aongezewe muda amefanya mambo makubwa toka tupate uhuru"

Hii imenichekesha sana!🤣🤣🤣
 
Gussie hujawahi kuwa mwana CCM na Hata posts zako humu za nyuma zinaonesha hivyo. Kati ya watu ambao Mama anatakiwa kuwahepuka ni ninyi. Msimpotoshe. CCM ni ya kila mtu ilimradi anakubaliana na Ser, itikadi na misingi yake.

Wale mnaofikiria kama Nape na Makamba eti kwakuwa baba zao walikuwa CCM tangu "zamani" basi ndio wana haki zaidi, mmepitwa na wakati!
 
Gussie hujawahi kuwa mwana CCM na Hata posts zako humu za nyuma zinaonesha hivyo. Kati ya watu ambao Mama anatakiwa kuwahepuka ni ninyi. Msimpotoshe. CCM ni ya kila mtu ilimradi anakubaliana na Ser, itikadi na misingi yake. Wale mnaofikiria kama Nape na Makamba eti kwakuwa baba zao walikuwa CCM tangu "zamani" basi ndio wana haki zaidi, mmepitwa na wakati!
Sawa kabisa mkuu

Tatizo ni pale tuliposhuhudia wapinzani wengi waki "Jump ship" kuunga mkono Sera za Mwenyekiti. Note hapo zile barua za kuhama vyama na kurudia chaguzi kama vile muandishi alikua mmoja. Hakuna sehemu waliongelea Sera nzuri za CCM wala itikadi ya CCM(Walifurahishwa na uchapakazi wa JPM)

Sasa hao ndo wako mguu nje mguu ndani
 
Gussie hujawahi kuwa mwana CCM na Hata posts zako humu za nyuma zinaonesha hivyo. Kati ya watu ambao Mama anatakiwa kuwahepuka ni ninyi. Msimpotoshe. CCM ni ya kila mtu ilimradi anakubaliana na Ser, itikadi na misingi yake. Wale mnaofikiria kama Nape na Makamba eti kwakuwa baba zao walikuwa CCM tangu "zamani" basi ndio wana haki zaidi, mmepitwa na wakati!
Hao unaowataja hawana haki kuliko watanzania wengine. Lakini kati yao mwenye nafuu ni makamba.

Nape Hana tofauti sana na mwigulu hawafai.
 
Sawa kabisa mkuu

Tatizo ni pale tuliposhuhudia wapinzani wengi waki "Jump ship" kuunga mkono Sera za Mwenyekiti. Note hapo zile barua za kuhama vyama na kurudia chaguzi kama vile muandishi alikua mmoja. Hakuna sehemu waliongelea Sera nzuri za CCM wala itikadi ya CCM(Walifurahishwa na uchapakazi wa JPM)....
Kama nani kwa mfano? Ngoja nikutajie wachache; Waitara bado Mbunge na Naibu Waziri. Katambi, Gekul na Silinde hivyo hivyo. Prof. Kitila ni Waziri Kamili. Hapo bado sijamtaja Dk. Slaa.

Unafikiri kati yao nani sio mwana CCM? Unamzidi Mama akili aliyewaacha kwenye nafasi zao na wengine kuwabadilishia nafasi ili waendelee kutekeleza Ilani ya CCM?
 
Back
Top Bottom