chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 11,960
- 20,532
Miaka kadhaa hapo nyuma,uchaguzi ukikaribia,wagombea wa Ccm walikuwa wanajipanga kwa hoja,na walikuwa wanajiandaa kuzifafanua kwa wapiga kura.
Katika kujipanga kisera, mgombea alipata kundi la wapambe waliomwelewa na kumuunga mkono,na aliwapa jukumu la kushawishi wanachama na wapiga kura,kupitia utaratibu huu, mgombea "aliwezesha" makada ili wasambaze ajenda za mgombea, kwa kweli kwa utaratibu huu watu tulifaidika na wengine tulijenga tuvibanda mjini.
Kipindi kabla ya uchaguzi,na magazeti yalikuwa na kambi,kwa waandishi ilikuwa kipindi cha mavuno.
Sasa hali tofauti,japo wana Ccm tunashangilia jamaa zetu wanavyopita bila kupingwa, sasa tujiandae, tutakosa tisheti ambazo zilikuwa zinatusitiri,tutakosa vihela vilivyokuwa vinapitapita, wagombea hawatatuthamini sisi wanachama,watathamini polisi na wakurugenzi na watawajali ili watangaze matokea au kuwaambia wajifiche wasipokee fomu za ugombea za wapinzani.
Chama kitabaki kwa wagombea na maafisa uchaguzi tu! Mgombea akiwa vizuri kwenye chama na kwa Afisa uchaguzi, mambo yamekwisha, mshindi anatangazwa kwa nguvu na nadhani hata polisi wataajiriwa kwa wingi.
Wapambe na makada,sasa tutafute shughuli ingine,shughuli ya kuitaftia Ccm kura itafanywa na polisi na wakurugenzi