Hili La Mwaka Huu Halipiti Bure Mpaka Ccm Imetoka Kwenye Hatam
Ccm imeimarika zaidi ya mnavyodhani. UKAWA ni ukabila/CHADEMA & udini/CUF
bila shaka kabisa na hawana lolote usione wazee wetu wa ccm wametulia ukadhaniwanaogopa ila wanasuka mipango ccm oyeeee
Nawaomba kwa dhati wanachama wa CCM tushikamane kwa nguvu zote kipindi hiki kuelekea uchaguzi yatasemwa mengi sana kuhusu chama chetu na viongozi wetu tusiwape nafasi wabaya wetu wanaopanga kutuangamiza kwa maneno ya UONGO. Wale MAFISADI waacheni waende kwenye vyama dhaifu (vyama vya UKABILA na UDINI). CCM ndo chama dola na itaendelea kushika dola milele na milele

Wana CCM tusijione wanyonge kwa ule umati wa pale Jangwani siku watani wetu wa jadi wanazindua kampeni zile zote ni hila za mafisadi katika kututisha. Sisi tumejipanga na tuna timu makini ikiwemo WASANII MAARUFU hasa Dada Wema na Mcekeshaji Steve Nyerere wao watapita kila nyumba kuhakikisha tunapata kura za kutosha. Ondoeni hofu ushindi kwetu ni lazima. Mgombea wetu anauzika sana. Asanteni.
Wanaondoka CCM wameondoka kwa uroho wa madaraka baada ya kutemwa na vikao halali vya chama wanahaha na kukimbilia chama dhaifu CHADEMA huu ni uroho wa madaraka tofauti na malengo na kanuni za CCM
Kwani kuna CCM tena?
Nawaomba kwa dhati wanachama wa CCM tushikamane kwa nguvu zote kipindi hiki kuelekea uchaguzi yatasemwa mengi sana kuhusu chama chetu na viongozi wetu tusiwape nafasi wabaya wetu wanaopanga kutuangamiza kwa maneno ya UONGO. Wale MAFISADI waacheni waende kwenye vyama dhaifu (vyama vya UKABILA na UDINI). CCM ndo chama dola na itaendelea kushika dola milele na milele
Kwa style hii kweli tutaupata mshikamano?
Naishauri CCM isome alama za nyakati. Katika matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa viti maalum kupitia VIJANA yaani UVCCM inaonesha kuwa watoto wa wananchi wa kawaida hawana nafasi ya kupata fursa za uongozi kupitia UVCCM.
Kati ya majina 6 ya walioshinda nafasi hizo wote ni watoto wa viongozi wa CCM, Je hii ni coincidence kwamba watoto wa viongozi pekee ndio wenye uwezo?
Mimi nilikuwa nafuatilia kwa karibu mchakato mzima wa uchaguzi huu na ninachoweza kusema ni kwamba CCM imelewa na madaraka na wakati sasa umebadilika, CCM isiendelee kuendesha mambo yake kwa mazoea sasa ni mwaka 2015 mambo yanabadilika wananchi sasa wana upeo kulinganisha na zamani.
UKAWA inawekeza katika vijana ambao hawana ajira na hawana fursa za kufanikiwa ndani ya CCM kwa sababu CCM inapendelea watoto wa vigogo.
Kuna vijana wengi ambao waliingia katika mchakato huu wa kupitia UVCCM na wana uwezo wa uongozi lakini hawawezi kufanikiwa ndani ya chama kwa sababu ya kuna wengine wanabebwa kutokana na majina ya wazazi wao. Hebu angalia majina ya walioshinda uchaguzi huo na uhusiano na viongozi wa CCM.
Washindi wa ubunge viti maalumu UVCCM - Bara, 2015.
1.HALIMA BULEMBO - Mtoto wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo.
2.ZAINAB KATIMBA - Mtoto wa Kada wa CCM, Bi Maimuna Tarishi pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mbalimbali nchini.
3.JULIANA MASABURI - Mtoto wa Kada maarufu wa CCM na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi
4.MARIUM DITOPILE - Mtoto wa Merehemu Ditopile Mzuzuri aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM Wilaya za Sengerema, Mwanza, Tabora na Mbunge wa Ilala, DSM.
5.MARIA KANGOLE - Mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Arusha Bw. Onesmo Kangole.
6.SOPHIA KIZIGO - Mtoto wa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Taifa) Bw. Mfaume Kizigo.
7.JACQUELINE MZINDAKAYA - Mtoto wa Kada Maarufu wa CCM Dkt. Chrisant Mzindakaya ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kwela na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Simiyu.
CCM ijiulize, Je watoto wa viongozi wa CCM wanawakilsha asilimia ngapi ya vijana wa nchi hii?.
Cha ajabu watoto hawa walianza kuzunguka mikoani na kuanza kampeni kwa wajumbe wa ngazi ya Taifa kabla ya mchujo wa ngazi mkoa haujafanyika.
Je, walipata wapi uhakika kwamba watapita ngazi za mikoa mpaka wakaanza kutoa rushwa ngazi ya Taifa bila ya kuwa na uhakika wa kubebwa?