Wana CCM tunahujumu juhudi za Rais Samia. Tuacheni Unafiki sisi wenye Tunaikwamisha Serikali

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,321
11,386
CCM ina wanachama zaidi ya Mil 8. Chanjo zimeletwa kwa watu Mil 1.

Mwenyekiti wa Chama kasema watu wakachanje naye akaenda chanja kama mfano. Mpaka leo chanjo si zaidi ya 400,000. Hii ni Hujuma. Tena hujuma ya wazi kabisa.

Kwa wanawachama wetu zaidi ya Mil 8 nchi nzima tungekuwa tunagombania kuchanjwa na tunataka Serikali ilete nyingine.

Badala yake nadhani hata zilizopo zitakuwa zime expire maana ni muda sana na zinaishi kutegemeana na mazingira. Hazijaisha na hakuna tena kelele. Hii si sawa. Je hatumwamini Mwenyekiti wetu?

Mnadhani anajisikiaje kuona yeye na kundi dogo tu la watu ndo wamechanja?
 
Hahaha! Hongera kwa kufikirisha akili.

Lakini bado kasema sio LAZIMA kuchanjwa.
 
Hakuna mtanzania mpumbavu wa kuchoma ovyoovyo chanjo za majaribio
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom