Wana CCM Orodhesheni Mema na Mazuri ya Upinzani!

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,500
2,000
Kila mara hapa JF watu wanaoonekana kuwa Upande wa CCM ama Serikali hulaumu sana watu wanaoikosoa serikali ama CCM kwa hoja kwamba wanaoikosoa Serikali na CCM huwa hawaoni Mema na Mambo Mazuri yanayofanywa na Serikali au CCM? Wanahoji ni kwa nini kila siku kuna watu kazi yao ni kukosoa tu hata siku moja hawaisifii CCM ama Serikali inayoongozwa na CCM?

Leo ni nafasi ya wana CCM na waunga mkono Serikali nao kuorodhesha Mambo mazuri na ya kimaendeleo pamoja na mema yanayofanywa na upande wa Upinzani Hususani UKAWA!
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,897

UPINZANI UMEJITAHIDI kulifanya jiji la DAR na ARUSHA kuwa safi
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,086
2,000
Hata usafi wa Dar aliouona YEHODAYA wewe huuoni?
Ni kazi ya Comred Paul Makonda yule mnaemwita anaejipendekeza.
Dar Mpya,Dar ya Makonda,Mti wangu Nyumba yangu
Wakati watu wanalazimishwa kufunga biashara na kufanya usafi mlibeza na kupinga humu,kuna mchaga mmoja wa pale stendi ya ubungo alifungua thread humu akimtukana Makonda kwa kumlazimisha afunge duka hadi saa 4,wakati asubuhi ndio muda wa biashara.
Sasa mmeona mafanikio mnayarukia.Hatujawahi kusikia meya wa chadema au kubenea wakipaza sauti kufanya usafi,ni Paul Makonda anaetumia nguvu za kisheria kuwahamasisha watu wafanye usafi
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,500
2,000
Sasa mmeona mafanikio mnayarukia.Hatujawahi kusikia meya wa chadema au kubenea wakipaza sauti kufanya usafi,ni Paul Makonda anaetumia nguvu za kisheria kuwahamasisha watu wafanye usafi
Aliyesema mfanikio ya Upinzani ni Usafi wa Dar siyo mimi ni YEHODAYA kama utaka kumkanusha mkanushe jamaa yako na usishambulie tusiohusika. Kwenye uzi huu sisi wengine ni watazamaji tu. Kwa ivo kwa maoni yako hakuna jambo la maana ambalo upinzani umefanya!?
 
Ngoso

JF-Expert Member
May 26, 2012
528
250
Kila mara hapa JF watu wanaoonekana kuwa Upande wa CCM ama Serikali hulaumu sana watu wanaoikosoa serikali ama CCM kwa hoja kwamba wanaoikosoa Serikali na CCM huwa hawaoni Mema na Mambo Mazuri yanayofanywa na Serikali au CCM? Wanahoji ni kwa nini kila siku kuna watu kazi yao ni kukosoa tu hata siku moja hawaisifii CCM ama Serikali inayoongozwa na CCM?

Leo ni nafasi ya wana CCM na waunga mkono Serikali nao kuorodhesha Mambo mazuri na ya kimaendeleo pamoja na mema yanayofanywa na upande wa Upinzani Hususani UKAWA!
Chama kinapo omba ridhaa ya kuongoza nchi ni sawa na baba kwenye familia.yaani ni wajibu wake kwa mwanae kumtunza,kulea kumpa elimu afya na maisha bora kwahiyo chama au serikali inapoyatimiza hayo kwa wananchi wake hakuna haja ya kusifiwa kwakuwa ndio wajibu wake. kazi ya wapinzani ni kuzungumzia yale mapungufu hata kama ni madogo kiasi gani kwamfano baba kamnunulia mtoto kiatu cha ngozi bila sox wapinzani watalaumu kutonunuliwa sox bila kujali gharama ya kiatu. Tanzania tumefika hapa kutokana na utawala wa ccm. majizi mafisadi matumizi mabaya ya ofisi yamefanywa na CCM na Serikali maana wao ndio wapo madarakani.kwakuwa awamu ya tano inapambana na madudu ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wapinzani kwa awamu zilizo tangulia hatuwezi kusifia kwakuwa amesikia kelele za wapinzani ameamua kuanza kubadilika na kutimiza wajibu wake kwa wananchi.sifa atapata kama atakomesha mikataba inayoendelea kutunyonya kama IPTL,LUGUMI,MADINI,UDA N.K
 
mzalendo15

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
1,367
2,000
Mazuri ya wapinzani hayawezi kuonekana moja kwa moja kwakuwa wao sio watawala was miaka mingi ukilinganisha na CCM.
Mazuri ya wapinzani ya meonekana katika kuibua hoja chanya ambazo zilifungua akili za watanzania ukianza kipindi kile cha EPA,RICHMOND,SAFARI ZA NJE ZISIZO NA TIJA,KULIMBIKIZA MADARAKA,KUBORESHA ELIMU,ULINZI na mambo mengi sana amabayo wapinzani waliyatolea fikra chanya.
Na kwakuwa wao ndio watawala waliyachukua Yale ya upinzani na kuwafanyia kazi.
Chakustaajabisha baada ya kuzifanyia kazi hizi hoja za wapinzani wakazigeuza kuwa wao ndio wameziibua huu ni ubinafsi usiokifani.
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,960
2,000
Serra zake nzuri amazi watawala wanajaribu kuiga na wanashindwa kuzitekeleza ipasavyo!!
 
stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,482
2,000
Zaidi ya matusi na hivi mmemuingiza mtaalam wa matusi mange kunambwe, sijaona lingine la maana toka kwenu!
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,783
2,000
Kila mara hapa JF watu wanaoonekana kuwa Upande wa CCM ama Serikali hulaumu sana watu wanaoikosoa serikali ama CCM kwa hoja kwamba wanaoikosoa Serikali na CCM huwa hawaoni Mema na Mambo Mazuri yanayofanywa na Serikali au CCM? Wanahoji ni kwa nini kila siku kuna watu kazi yao ni kukosoa tu hata siku moja hawaisifii CCM ama Serikali inayoongozwa na CCM?

Leo ni nafasi ya wana CCM na waunga mkono Serikali nao kuorodhesha Mambo mazuri na ya kimaendeleo pamoja na mema yanayofanywa na upande wa Upinzani Hususani UKAWA!
Ebu kwanza orodhesha mambo mazuri matano (5) yaliyofanywa na Serikali nami nisifie matano (5) yaliyofanywa na Ukawa.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,783
2,000
Ni kazi ya Comred Paul Makonda yule mnaemwita anaejipendekeza.
Dar Mpya,Dar ya Makonda,Mti wangu Nyumba yangu
Wakati watu wanalazimishwa kufunga biashara na kufanya usafi mlibeza na kupinga humu,kuna mchaga mmoja wa pale stendi ya ubungo alifungua thread humu akimtukana Makonda kwa kumlazimisha afunge duka hadi saa 4,wakati asubuhi ndio muda wa biashara.
Sasa mmeona mafanikio mnayarukia.Hatujawahi kusikia meya wa chadema au kubenea wakipaza sauti kufanya usafi,ni Paul Makonda anaetumia nguvu za kisheria kuwahamasisha watu wafanye usafi
Baelezee! Wasione vyaelea!
 
Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Elimu bure na kuongezeka kwa bei ya korosho na Pamba ndio maana ya kutiririka pesa kwa wanyonge.

la Nyumbu hawatakaa waelewe hili.

Wako bize kupangusa viatu vya Lowasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom