Elections 2010 Wana CCM Newala Wampongeza Rais Kikwete kwa Ushindi wa Kishindo

shilanona

Member
Oct 31, 2010
55
22
Hivi wanajamii hivi huu ushindi wa kishindo ndiyo upi huo? Je ni wa kishindo kwa sababu alishinda kwa kura 61% au kwa mazingitra ya utata wa matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na NEC?
Nipi hapa Newala na kuna shmrashamra ya kumpongeza Rais Kikwete kwa ushindi huo wa Kishindo.
 
Hao si ndo walimzomea Mkuchika wao mbele ya Pinda mwaka jana kuhusu ukosefu wa maji? Mi nadhani huyo Mkuchika hakushinda ubunge, alifaidika kwa kura za kuchakachuliwa.
 
Nadhani hao ndugu zangu kwanza hawana cha kufanya,alafu kishindo gani hicho kwani asilimia 61 na asilimia 80 za mwaka 2005 kipi kishindo?tuwapeleke darasani wakasome hesabu za sehemu na asilimia.
 
Ushindi wa vishindo una tafsiri nyingi!!! Kwa mazingira tuliyonayo katika uchaguzi wa 31.10.2010 Kikwete alipata ushindi wa vishindo vya wizi na dhuluma kwa wapigakura karibu milioni 20-na kuwafanya waonekane waliopiga kura ni milioni 8.6 tu-ni vishindo vya aibu na fedheha!!!!!!!!!!!
 
Hivi wanajamii hivi huu ushindi wa kishindo ndiyo upi huo? Je ni wa kishindo kwa sababu alishinda kwa kura 61% au kwa mazingitra ya utata wa matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na NEC?
Nipi hapa Newala na kuna shmrashamra ya kumpongeza Rais Kikwete kwa ushindi huo wa Kishindo.

Ni ushindi wa kishindo cha uchakachuaji-wanabadilisha tu maneno, lakini truth remains kuwa ni ushindi wa vishindo vya wizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom