Wana CCM mpaka sasa JK ametimiza ahadi gani alizohaidi? Au ilikuwa anatania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM mpaka sasa JK ametimiza ahadi gani alizohaidi? Au ilikuwa anatania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Mar 17, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Vip ahadi alizohaidi mwaka 2010 km flying over, mabasi ya kwenda kasi, treni na kuifumua reli yote ya kati, kilimo kwanza, meli maziwa makuu nk

  Na arumeru kawatania atafanyaje vile
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Politics is all about lies and nothing else so do your thing and don't wast your time with those liar.
   
 3. m

  mwikumwiku Senior Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado Anayafanyia fizibiliti study kwanza! Ngoja aende Marekani halafu akirudi ataanza na hizi ahadi za arumeru, (LIFO)! Pole Mtanzania mwenzangu, umezidi upole wa kizezeta!
   
 4. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Maisha bora!kazibiti mfumuko wa bei,ajira kwa vijana wote,mahabara na nyumba za walimu kila shule,balabala juu dsm,n.k
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kasome kwenye uzi wa mazuri ya JK kule juu mengine utayakuta kule.
   
 6. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  anasema mwisho wa utekelezaji wa ahadi zake ni 2015.
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Aliwaahidi umeme wa mgao. Na hiyo ameshaitimiza
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkimkumbusha Jk ahadi zake anaweza kupiga Mwereka
   
 9. M

  Makupa JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Chali wa moshi umechapia kidogo, hata hivyo sio mbaya endelea kujifunza
   
 10. m

  majogajo JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nyingine hizi na mahali alipozitja
  [FONT=&quot]AHADI ZA CCM UCHAGUZI MKUU 2010

  Ninyi watoto wa nyoka acheni kumwaga sumu humu. Mmezewea majungu kama wazazi wenu. Kila kukicha huyu hivi yule vipi. fitna na majungu hamna issue? Haya pelekeni list hii hapa chini kwa hao waliowatuma maana wamejisahau ni nini waliahidi na wajibu wao ni upi.

  1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36.Kulinda haki za walemavu - Makete
  37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha [/FONT]
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Alichotimiza ni kuwapa wanawake nafasi ila kwa upendeleo maalum na kwa manufaa maalum na kwa malengo maalumu na mtizamo maalumu na faida maalumu kwa Rais.
   
 12. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,642
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  Jk na sisiyemu yake walikuwa wanafanya utani tu haikuwa siriazi kama anavofanya MKAPA kule arumeru
   
 13. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  nadhan bado anafanyia upembuzi yakinifu ahad zake.
   
 14. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mengi sana!
   
 15. T

  Tewe JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  For sure it was a joke
   
 16. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Utekelezaji mwisho 2015. Hivyo hajashindwa bado.
   
 17. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  alikuwa anatania wakuu
   
Loading...