BM Pesambili
Senior Member
- Jul 10, 2016
- 102
- 624
" Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au wengi. Chama kinachopenda ukweli na hakina budi kiwape wanachama wake Uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kutumia Uhuru huo na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia Uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli" Haya ni maneno ya busara ya Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere.
Hivi karibuni tumeshuhudia na bado tunaendelea kuhushudia Wana CCM wakinyukana wao kwa wao kisa kukabidhiwa uwenyekiti wa Chama Rais Magufuli. Sio kitu cha kushangaza wanachama kutofautiana ndani ya chama kila mwanachama ana mawazo yake huru. Tatizo linakuja huyu mwanachama au kiongozi wa chama ana dhamira gani na chama kwa mawazo yake?
Mfano kulikuwa na shutuma Kali humu ndani ya Jukwaa mmoja akishutumu na mwingine ikipanguwa shutuma hizo:
LIZABONI: "Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajabu Luhwavi NKM CCM Bara"
EGNECIOUS: Majibu kwa LIZABONI, kuhusu upotoshaji wa makusudi wenye dhamira mbaya dhidi ya Rajabu Luhwavi na CCM" wengi walipitia nyuzi hizi na kutoa mawazo yao wengine wakiwa kwa LIZABONI na wengine upande wa EGNECIOUS na kundi lingine lilikuwa kazi yao kuchochea kuni ili moto uendelee kuwaka.
Lengo langu sio kujadili hoja hizi na wala siko hapa kumshutum yoyote kati ya hawa wawili LIZABONI & EGNEOUS. Lakini baada ya kuzipitia nyuzi hizi mbili kwa makini kuna vitu nilivibaini vya kipuuzi sana na ndio lengo la mada yangu.
Kwa ufupi kabisa ambacho nimekibaini Biashara ya siasa imewanufaisha watu wengi mno. Siasa ndicho kiwanda kisichohitaji maarifa au ujuzi wowote, isipokuwa mtu ajue uongo, unafiki na kujipendekeza pendekeza. Wengine wameamua kufanya kazi na Camera ili waonekane na bwana mkubwa, kwamba wako nae katika kauli mbiu ya "Hapa kazi tu". Uroho wa madaraka na Mali zimewapumbaza sana vijana kwamba ukitaka utajiri wa haraka na umaarufu unachotakiwa kufanya ni kuingia katika siasa.
Ni kitu gani hasa kinachosabisha makundi kujitokeza ndani ya chama? Viongozi wenye makoromeo yenye uchu wa vyote Mali nyingi na madaraka ndio tatizo ndani ya Chama hiki, wameotesha mirija yao kunyonya watanzania sasa hawataki mirija yao ikatwe. Wamebaki kama shomoro katika kutangatanga kwake, na kama mbayumbayu katika kuruka kwake. Wengine wanasikitisha sana kutwa nzima wanahaha kwa waganga, wengine kuchafuana kwenye mitandao na hata kuua wanaowaona ni washindani wao.
Muda wa kukabidhiwa Chama Mh Rais ndio huo unawadia. Ushauri wangu kwa mwenyekiti mtarajiwa. Waache waendelee kuwa wanafiki, waache waendelee kuita wema ubaya na ubaya wema, waache waendelee na dhamira zao zilizo tiwa ngazi, waache waendelee kuchagua giza badala ya nuru, waache waendelee kukutoa dosari na kukusemea uongo ili wapate kujijenga wao.
Waache waendelee kukoroga sumu ikisha kuwa tayari wanyweshe wao kwanza kisha uvunje udhalimu na kiburi chao, uwafukuze toka mwangani hadi gizani. Hakikisha unawatupa nje wote wanafiki, wenye kiburi, dharau, uchoyo, wakafedheheshwe kwa ujinga na maradhi yao, hapo ndipo fitina zao zitakapokoma na kukumbukumbu lao kusaulika.
Aliyejiushisha na historia yako anakujua mpaka moyoni mwako atakulinda na wabaya wako wote, endelea kuwatumikia watanzania kwa akili zako zote, kwa moyo wako wote na kwa mapenzi yako yote. Busara itakulinda, ufahamu utakuhifadhi na hekima itakuokoa.