Wana CCM Kigamboni wapata shaka mwenendo wa mbunge wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM Kigamboni wapata shaka mwenendo wa mbunge wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]IJUMAA, JULAI 20, 2012 06:13 NA EVANS MAGEGE, DAR ES SALAAM

  WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kigamboni, wamesema wanapata shaka kutokana na mwenendo wa mbunge wao, Dk. Faustine Ndugulile, kwa kuwa na tabia ya kuchukua hatua mbalimbali zinazokuwa kinyume na Ilani ya chama hicho.

  Wasiwasi huo uliibuka Dar es Salaam juzi, katika majadiliano ya mkutano uliojumuisha wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Kata Kigamboni, ambapo baadhi walisema wanatilia shaka uamuzi unaofanywa na mbunge wao kwamba si maagizo halali ya wapiga kura wa Kigamboni.

  Mwenyekiti ya Halmashauri hiyo, Ramadhani Waziri, alisema ameshangazwa na uamuzi wa mbunge huyo wa kuandaa mkutano wa hadhara katika Kata hiyo, bila kushirikisha Kamati ya Siasa au Halmashauri Kuu ya Chama hicho Kata ya Kigamboni.

  Alisema pamoja na mkutano huo kuota mbawa kwa kushindwa kufanyika, kumeibuka mijadala mingi kwa wananchi wa kata hiyo juu ya jambo hilo hali inayotishia mustakabali wa chama hicho katika kata na jimbo hilo kwa ujumla.

  “Sisi sote ni wanachama wa CCM, kuna mambo ya msingi ya kukaa na kuelezana kwa ajili ya kuweka usawa wa pamoja katika utekelezaji wa Ilani ya chama chetu, hivi juzi tu tumeona mbunge wetu anaandaa mkutano bila kutushirikisha wanachama wenyeji, sielewi kwanini aliamua hivyo,” alisema Waziri.

  Naye, Diwani wa Kata hiyo, Dotto Msawa, alisema anasikitishwa na kauli ya mbunge huyo kwa kumtuhumu kuwa ni miongoni mwa diwani aliyepewa rushwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa ajili ya mchakato wa mji mpya Kigamboni.

  Alisema kauli hiyo ilimkera ambapo yeye na madiwani wenzake watatu wa jimbo hilo walilazimika kumuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda juu ya kuchafuliwa na mbunge wao.

  “Sina ugomvi na mbunge wangu, lakini nashangaa kumuona akienda kinyume na Ilani yetu ya CCM, mchakato wa mji mpya ni jambo ambalo lipo katika Ilani yetu ya uchaguzi, sasa iweje leo hii atutuhumu sisi kuwa tumehongwa katika mchakato huu na kama vile haitoshi wizara hiyo imetupeleka bungeni.

  “Kwanini tugombanie fito na wakati tunajenga nyumba moja, kuna mambo ya kukaa chini tunakosoana kwa nia njema ya kujenga na sio kutoa kauli za ajabu ajabu ambazo zinatumiwa na wapinzani kama mtaji wa kisiasa.

  “Kigamboni ni yetu kwa hiyo ni muhimu tusimamie Ilani ya chama ambayo wananchi wetu waliipenda na wakaamua kumpigia kura mbunge wetu pamoja na sisi madiwani, kwa hiyo tusianze kuwachanganya wapiga kura wetu,” alisema Msawa.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hawa watu wa Kigamboni wana Mbunge Mzuri wa CCM anatetea Haki zao Madiwani wao wanawaangusha

  Kukimbilia CCM ambayo haiwaambii matokeo ya huo MJI MPYA.

  Wananchi Wa Tanzania kweli Hawajui Demokrasia, Tunadhani Demokrasia ni kusema NDIO, NDIO kwa chama chako

  kila kitu kinachosema; Lakini ni la ni kusema pia hapana na kurekebisha...
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwa hali ilivyo Kigamboni jimbo ni la Anna Komu 2015 CHADEMA.
   
 4. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Mimi Sio Mwana-CCM na wala sina Elimu kama ya huyu Mbunge lakin naishi hukuhuku Kigamboni. Huyu Jamaa ni dhaifu sana na amejiona yeye ana madaraka kama Rais cha pili watu wanaomshaur wanampoteza kwa kiasi flani. 2015 akatafute Jimbo mahali pengine
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo huyo, sasa kupitia CDM, Tetesi. Ila afanye spidi.
   
 6. m

  maingu z Senior Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hey, watch out your statements , kigomboni si ya ccm, ni ya watanzania wote waishio kigamboni na wasio wana ccm, na mbunge si wa ccm pekee, anawakilisha watu wenye kada tofauti, msimlazimishe tu akafuata yenu tu, wakati maslani ya wengi yanaachwa, hapo hatutokubaliana navyi bali tutamsikiliza mbunge pale tunapoona anatetea maslahi ya wengi na sio chama,wakati wa kuwa na viongozi wa kutetea chama badala ya maslahi ya nchi umepitwa na wakati mwacheni mbunge afanye kazi ili mradi maslahi ya wengi yanafuatwa.......poleni kwa mawazo mgando....mbunge chapa kazi hata wakikutoa vyama vipo unapata tu....cha msingi tetea maslahi ya wengi na wengi ndo watakuchagua
   
 7. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180

  Huwezi ukamfananisha na mpambanaji A.Komu, kosa walilifanya wanakigamboni kumchagua huyo bwana(na kumuacha Komu) wameshaanza kuliona na 2015 ni wakati muafaka wa kutubu makosa yao.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Dr Ndungulile ameibuka baada ya kutokuwekwa kwenye baraza la mawaziri huyu mbunge asiwaige wakina Mnyika ambao hawana serikali anchotakiwa ni kutekeleza ahadi zake na za rais wake huu sio muda wa malumbano na kutafuta umaarufu wa kijinga
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Fanyeni yote lakini hili ni la maisha ya watu, kama kweli hakuna kuelewana kwani nini wanatupiana maneno bungeni na kwenye vyombo vya habari..... warudi kwa wananchi waliowachagua kueleza tofauti zao zilizojitokeza kuhusu mradi wa mji mpya wa kigamboni...

  Wananchi ni wadau wa mradi kutokuwaeleza nini kilijitokeza bungeni huku wakisoma mambo kwenye vyombo vya habari ni kuwachanganya zaidi.
   
 10. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madiwani kujibanza kwenye kivuli cha ilani ya chama hakuna tofauti na mbunge kujibanza kwenye kivuli cha bunge.

  wakazi wa kigamboni si wote wanaCCM ni wa vyama vingi na wengine hawana chama, kulifanya jambo hilo la ndani ya chama ni kuleta mfarakano.

  Makazi hayana chama na ndivyo naamini kwamba Ndungulile hawatetei wanaCCM kigamboni bali wananchi ambao kwa namna moja au nyingine wataathirika na mradi huo...

  kwa nafasi ya mbunge sio mwendawazimu anajua nini anasema na ukifuatilia kauli zake anaongelea zaidi sheria zinazosimamia mradi wakati madiwani wanazungumzia halmashauri ya chama imesema nini!!!!!! ilani ya chama imesema nini!!!!!!!!

  Tukumbuke kwamba Ilani ya chama sio sheria inayosimamia mradi bali ni sera na sera inatamka tu kwamba kigamboni itafanywa mji mpya baada ya sera ndio sheria za kusimamia sera zinafuata.
   
 11. b

  beyanga Senior Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la ccm ni akili ndogo kuongoza akili kubwa doto ni darasa la saba mbunge ni dr of medicine doto anatumiwa kwa sababu uwezo wa kujua mambo ni mdogo saana poleni ccm kigamboni mmekalia kuti kavu
   
 12. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dotto Msawa na genge lake wakumbuke kuwa kuichagua CCM hakuna maana kwamba wakazi wengine wa itikadi zingine hawaongozwi na viongozi wa CCM na ndio sababu kakimbilia kwa mwandishi wa habari uchwara kueleza mgogoro wao na mbunge badala ya wananchi.

  mbunge ni mjanja ndio maana baada ya kuona mmetofautiana bungeni akaomba mkutano na wananchi, kigamboni yote wanajua kuwa madiwani mlikula njama mkazuia mkutano huku wananchi wamekusanyika uwanjani.

  Kikubwa ni kwamba, mbunge anapigana peke yake na hilo wananchi wanalitambua.
   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hivi mbunge amechaguliwa na CCM au wananchi wa Kigamboni? Yani mbunge anapotaka kuonana na wananchi wake lazima aombe ruhusa kwa chama? Huu ni utaratibu wa wapi?
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kabla mbunge hajakwenda Dodoma aliwaita wananchi wa kata zote za kigamboni na kuzungumza nao na swali lake kubwa lilikuwa mnataka nikawasemee nini mbungeni???

  lakini madiwani na wenyeviti wa serikali za mtaa mnaotuhumiwa kwenda dodoma kwa rushwa ya Waziri wa Ardhi hamkufanya hivyo mliwatoroka wananchi hadi pale walipomsikia mbunge akilalamika mbungeni.

  Doto msawa diwani wa kata ya kigamboni anajua hasira ya wananchi juu yao hivyo anatumia njia hii kujisafisha.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Ni utaratibu wa diwani wa kata ya kigamboni (CCM) Doto msawa na genge lake.

  Kasahau pia kwamba kwenye uchaguzi wowote ule baadhi ya wananchi bila kujali chama anaweza kumuunga mkono mgombea wa chama ambacho sio chake kama ana sifa kuliko wa chama chake na ndio jambo lililomsaidia sana Ndungulile kigamboni hadi kumwangusha Anna Komu wa chadema. Wakazi wengi walimkubali DR Ndungulile kama Ndungulile sio chama chake.
   
 16. b

  bashemere Senior Member

  #16
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​yuko hapo kwa pesa za waarbu akina abdala wa scaba sasa na wao wawe makini maan chadema ikiingia waanze kurudi zanzibar wameiba maeneo mengi ya wazi kwa kifadhiri ccm
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Doto anatembea kwenye historia yake.

  Dotto ni mhuni wa kijiweni na hilo litawapa tabu sana wakazi wa kigambini ni vijana waliokuwa wamezoea kucheza kamali na kufanya matukio ya kihalifu jambo ambalo haliwezi kumshangaza yeyote.

  Ndungulile ni msomi Dk wa tiba ya binadamu na kafanya kazi kwenye hosp. kuu ya nchi hii Muhimbili na Afrika kusini. Linganisha na darasa la saba.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kumbe unajua heee hao magenge ya Scaba ndio wanaompa tabu ndungulile sio CCM, akina Scaba walimweka Dotto kwa maslahi yao na kumpa jeuri lakini Dotto anadhani wakazi wa kigamboni ni wajinga hawamjui kwa kujificha kwenye kivuli ya CCM.

  CCM haiwezi kumtuma mtu (Dotto) asikutane na wananchi wake lakini akakutane na vyombo vya habari (gazeti), Dotto anacheza na akili za watu.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kama kweli Dotto anajiamini ana nguvu kigamboni na alichaguliwa kwa sababu anapendwa aitishe mkutano sasa.

  Dotto anajua jinsi alivyotumia njia za panya kupata udiwani wengi walikuwa na mashaka naye alipokuwa anapita kuomba kura na kuna wengine walikuwa wanasema jambazi sugu kapewa udiwani?

  Ile kesi yake ya kuiba magari ya watu akakamatwa morogoro na gari iliyoibiwa nchini kenya sijui zilikwisha vipi????

  Hawa ndio aina ya watu tunaotaka wawatetee wananchi.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  hapa hatujadili vyama tunajadili maisha na hatima ya wakazi wa kigamboni kuelekea mji mpya.
   
Loading...