Wana CCM Arusha walisukuma gari la Lowassa Mzee wa maamuzi magumu kwa furaha ya kumuona.

Jul 27, 2012
19
7
Nguvu ya Edward Lowassa kisiasa ilidhihirika katika ziara ya Katibu Mkuu mpya wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake mkoani Arusha. Kila walipofika, Lowassa alishangiliwa sana.

Kali ilikuwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid alikuwa wa mwisho kupanda jukwaani, pale jina lake lilipotajwa uwanja ulilipuka na mara baada ya hotuba yake ilibidi walinzi wake kufanya kazi ya ziada na kuzuia watu waliyotaka kumgusa na kumsahau mgeni rasmi.

Gari lake lilisukumwa hadi nje ya uwanja huku kina mama wakilifuta kwa kanga zao.
Huyo ndiyo Edward Lowassa
 
Kusukumizwa hata Mrema alisukumizwa...kiko wapi??? vionjo tu vya dunia hivyo.....imepita hiyo.
 
Mwenye namba ya lowasa anaeweza kuniunganisha na lowasa aniinbox. I hate all except Lws. He is a pragmaticand visionary leader
 
mwamkata muhamad kwani hukusikia ya kwamba aliwalipa wale waliokawa wanafanya kazi ile??

Maisha yenyewe pale arachuga ni magumu
50elfu kwa ajili tuh ya dk 5 za kusukuma gari lake sasa kwanin vijana wasichangamkie deal??
 
Last edited by a moderator:
Wakuu tuache wivu Fisadi Lowassa anapendwa sana na wanaCCM walio wengi.
Huu ni ukweli mchungu sana kwa baadhi ya watu.
 
Nguvu la Edward Lowassa kisiasa ilidhihirika katika ziara ya Katibu Mkuu mpya wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake mkoani Arusha.Kila walipofika, Lowassa alishangiliwa sana. Kali ilikuwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid alikuwa wa mwisho kupanda jukwaani, pale jina lake lilipotajwa uwanja ulilipuka na mara baada ya hotuba yake ilibidi walinzi wake kufanya kazi ya ziada na kuzuia watu waliyotaka kumgusa na kumsahau mgeni rasmi. Gari lake lilisukumwa hadi nje ya uwanja huku kina mama wakilifuta kwa kanga zao.
Huyo ndiyo Edward Lowassa

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,EL ni mtu anayekubalika,na hata zile kashfa za ufisadi wa Richmond yeye alikuwa ni mbuzi wa Kafara tu,nyie subiri muone kivumbi cha mwaka 2015 na tayari ameapa kulikomboa jimbo la Arusha mjini endapo rufaa ya Lema itatupiliwa mbali.
 
Wakuu tuache wivu Fisadi Lowassa anapendwa sana na wanaCCM walio wengi.
Huu ni ukweli mchungu sana kwa baadhi ya watu.

Katika hilo hakuna ubishi hata kidogo mkuu,tatizo ni moja tu kwamba watu mara zote hawataki kuukubali ukweli,lakini huyu jamaa anakubaika kuanzia kwa viongozi wa chama,pamoja na wananchama wale wa kawaida katika nchi hii,isipokuwa tu wale ambao wana chuki zao binafsi.
 
Wakuu tuache wivu Fisadi Lowassa anapendwa sana na wanaCCM walio wengi.
Huu ni ukweli mchungu sana kwa baadhi ya watu.

Tayari umesema anapendwa na wanaccm walio wengi sasa unataka nini ungesema anapendwa na watanzania wengi ningekuona chizi lakini kama anapendwa na wanaccm basi hayo ni mapenzi ya wanaccm siyo ya watanzania usirudi tena utanipeleka bani tena leo
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,EL ni mtu anayekubalika,na hata zile kashfa za ufisadi wa Richmond yeye alikuwa ni mbuzi wa Kafara tu,nyie subiri muone kivumbi cha mwaka 2015 na tayari ameapa kulikomboa jimbo la Arusha mjini endapo rufaa ya Lema itatupiliwa mbali.
Mkuu hapo umepitiliza sana.
Arusha mjini kurudi CCM ni sawa na ndoto za kichaa.

Ni yeye Lowassa alihusika sana jimbo hili kwenda CHADEMA baada ya kumuunga mkono Dr.Batrida Buriani 2005.

Mkuu Lowassa anapendwa sana na WanaCCM wengi ambapo kwa Arusha mjini ni kama hakuna wanaCCM.

Infact hata Lowassa 2015 akigombea ubunge wa Arusha mjini nina uhakika hata robo ya kura hata pata.
 
Back
Top Bottom