Wana CCM Arusha walisukuma gari la Lowassa Mzee wa maamuzi magumu kwa furaha ya kumuona.

Hahaa... inashangaza sana watu wana iman na katbu mpya kinana kupambana na rushwa ndani ya CCM wakati anazunguka na mtu ambaye chama chake kinamtuumu kwa rushwa na anaonekana ana mvuto kwa watu zaidi ya yule ambaye anaonekana ni tumaini kwa chama kupambana na rushwa............. hapo kuna jibya? nimeyakumbuka maneno ya zitto ili tanzania iwe salama ni lazima ccm iondolewe madarakani
 
Unapofunguka kidogo huwa unaeleweka,OK nakubaliana na wewe lakini kumbuka kila jambo na wakati wake nawexa kuamini na kushawishika kwamba huu ni wakati wa CHADEMA kufanya kila wanaloliona na likakubalika kwa jamii,kwa sababu tu ya pointi zako hizo sita,lakini wasiwasi wangu ni kama hali hii itakwends mpaka wakati wenyewe yani mwaka 2015,kwa sababu huko nako hawachelewi kuvurugana na kutimuana wanakosa uvumilivu na hasa kwenye mambo magumu!!!!!
That is the point.
Kwa vyovyote vile karata ya Maana kwa CCM kwa sasa nikujipanga internally ili kufanikisha mpango wa ''Divide and rule them''
kuimaliza CHADEMA.

Bahati mbaya sana kwa sasa ndani ya CCM hakuna siri wala nidhamu hivyo every tactic inavuja na kumfikia adui haraka sana.

Ninabashiri huenda hata JF ikafungiwa kwa amri ya ''wakubwa'' ndani ya miaka miwili ijayo.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,EL ni mtu anayekubalika,na hata zile kashfa za ufisadi wa Richmond yeye alikuwa ni mbuzi wa Kafara tu,nyie subiri muone kivumbi cha mwaka 2015 na tayari ameapa kulikomboa jimbo la Arusha mjini endapo rufaa ya Lema itatupiliwa mbali.

Acha utani mkuu!Lowassa alikomboe jimbo la Arusha mbele ya Lema na makamanda wengine?
 
Hakuna ccm Arusha wewe! Hao walugaluga waliletwa kutoka wapi sijui! Na hayo waliyofanya ni maigizo tu!

niliwaona wakiletwa na vidaldala vyenye vumbi, watu wakawa wanawaimbia ule wimbo wa siimbalii, nadhani wengi mshausikia.
 
ukaskini ni mtaji kwa ccm na kwa wanasiasa wa tanzania huu wote ni ubwawa ndio unawafikisha hapo vijana na akina mama kufanya kitendo ambacho hata shetani anawashangaa kusukuma gari la mwizi, fisadi, marehemu na mtu asiyejali utu wa watanzania
 
Tayari umesema anapendwa na wanaccm walio wengi sasa unataka nini ungesema anapendwa na watanzania wengi ningekuona chizi lakini kama anapendwa na wanaccm basi hayo ni mapenzi ya wanaccm siyo ya watanzania usirudi tena utanipeleka bani tena leo

wana ccm wanatosha kumpenda wala hatuna haja na wanamaandamano na migomo ya kijinga
 
3.+Pikipiki+zikiongoza+msafara+wa+Kinana,+kutoka+Uwanja+wa+Ndege+wa+Arusha.jpg

....kwa picha hii, basi itakuwa pikipiki zinavuta gari ya rais wa kufikirika !
 
Nguvu la Edward Lowassa kisiasa ilidhihirika katika ziara ya Katibu Mkuu mpya wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake mkoani Arusha. Kila walipofika, Lowassa alishangiliwa sana.

Kali ilikuwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid alikuwa wa mwisho kupanda jukwaani, pale jina lake lilipotajwa uwanja ulilipuka na mara baada ya hotuba yake ilibidi walinzi wake kufanya kazi ya ziada na kuzuia watu waliyotaka kumgusa na kumsahau mgeni rasmi.

Gari lake lilisukumwa hadi nje ya uwanja huku kina mama wakilifuta kwa kanga zao.
Huyo ndiyo Edward Lowassa

Kwa CCM ukiwa fisadi ndio ngazi ya juu kabisa ya mafanikio.

EL amefikia ngazi kuu ya ufisadi ambayo ndani ya CCM kila mtu anaitamani.

In CCM, this guy is a hero!
 
Back
Top Bottom