Wana CCM 1,000, Wenyeviti wa Vitongoji Arumeru Wahamia Chadema

FF UPO!?

Utabiri wako ulioachiwa Urithi na Marehemu Mchawi Mkuu wa Magomeni Mikumi naona unaendelea kuumbuka.
 
Bye bye magamba!we ll meet u in heaven!mmmh lakini sidhani kama mtakwenda peponi!ila tutawakumbuka kwa ufisadi,uongo,maisha magumu,umaskini wa kupindukia,ujinga kuongezeka,ukosefu wa ajira na mengine mengi!Mungu awalaani sana!
 
Mtoa maada utueleze ni Arumeru ipi? mashariki au magaribi isije kuwa ni wale 960 tuliosoma wiki iliyopita, ila kama ni hili jimbo lililowazi kwa sasa CCM itakuwa na wakati mgumu jinsi siku zinavyosonga mbele, nahisi CDM itaendelea kuchanua kama itaendelea kuwa wachapakazi, waadilifu.
 
Ni habari njema kwa CDM, vijana wa CDM kazi kwenu kuhakikisha elimu ya Uraia inawafikia wananchi kila sehemu hasa vijijini.
 
Haina tatizo Ng'wana Sweke "Mhola ahene". Mbona kwenye harusi moja kuna sherehe tatu? Yaani Kitchen Party, Send off na Receiption. Wewe twanga tu sherehe hata kama zitafika kumi kwa tukio lilelile moja.

"Mhola duhu" na nimeupenda ushauri wako kiongozi,nitakuwepo Malaika Beach Resort kuanzia saa 11 jioni kama kuna mwana jf hapa Mwanza atapenda kujumuika namimi anakaribishwa ila asiwe wa magamba side
 
Hilo ndilo tatizo kubwa katika siasa za tanzania, nikuanzia raisi, wateule wake pale tume ya uchaguzi, vyombo vyote vya usalama, na punguani wengine kama wewe

Sasa la ajabu nini, wahamie tu lakini kwenye sanduku la kura CCM lazima ishinde.
 

na Grace Macha, Arusha

KITENDO cha baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji cha Ng’iresi wilayani Arumeru wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kukiuka makubaliano katika utekelezaji wa mradi wa maji uliogharimu zaidi ya sh milioni 40 kimewafanya wananchi 1,000 wa kijiji hicho kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Uamuzi wa kuhamia upinzani ulichukuliwa na wananchi wa vitongiji viwili kati ya vinne wa kijiji hicho wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na viongozi kwa lengo la kujadili changamoto zilizojitokeza katika awamu ya kwanza na ya pili ya utekelezaji wa mradi huo uliolenga kunufaisha wananchi zaidi ya 5,000.
Wananchi waliohamia CHADEMA wanatoka katika vitongoji vya Kimelok na Ngoikaa ambao licha ya kuhamia upinzani pia wamefikia uamuzi wa kuyang’oa mabomba ya maji yaliyotandazwa katika maeneo tofauti na makubaliano na kuyapeleka walikokubaliana katika kikao cha serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kimelok, Jonas Semeitei (CCM), na mwenzake wa kitongoji cha Ngoikaa, Elias Kirengai, wote kutoka CCM waliunga mkono uamuzi wa wananchi wanaowaongoza kuhamia upinzani huku nao wakiahidi kufanya hivyo kipindi muafaka.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Ngoikaa, Elias Kirengai, awali wananchi walikubaliana na kutekeleza mradi huo katika awamu tatu tofauti ambapo ile ya kwanza ulilenga kusambaza huduma ya maji kwenye taasisi za umma ikiwemo shule ya msingi na sekondari Ng’iresi kabla ya huduma kusambazwa kwa wananchi wote.
“Ajabu ni kwamba mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wake waliamua kufanya tofauti na makubaliano katika awamu ya pili kwa kuelekeza maji sehemu tofauti, jambo lililowachukiza wananchi ambao kwa pamoja bila kujali itikadi zao waliamua kung’oa mabomba yote na kutandaza katika njia waliyokubaliana awali,” alisema Kirengai.
Alisema baada ya uamuzi huo wa wananchi, uongozi wa kijiji ulifikisha suala hilo ngazi ya halmasahuri ya wilaya na jeshi la polisi ambao baada ya kufika kijijini hapo na kushuhudia ramani ya awali ya mradi huo walikubaliana na hatua iliyochukuliwa na wananchi.
Baada ya kupitisha uamuzi wa kuhamia CHADEMA, wananchi hao waliamua kumwalika katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, kuwapokea wanachama hao wapya na kuzindua rasmi awamu ya tatu na ya mwisho ya mradi huo ambapo aliahidi kuchangia sh 700,000 kati ya milioni 2.1 zinazohitajika kuufanikisha.

h.sep3.gif


 
...jiachiee/jipe raha kwa tan yako mkuu,acha kujibana-bana kumbuka sherehe moja huanzisha nyingine..."unatumia kinywaji gani?",mwambie muudum akuongeze one for the road!...

Nimekusoma mkuu,natumia Tusker bariiiidi
 
Makamanda ,

ile dhana ya kizamani kuwa wapinzani hawawezi kuongoza nchi imepitwa na wakati.tusipoteze tena msimu huu..ikizingatiwa kuwa rasilimali zetu zinaliwa na wachache,kitendo kilichofanywa na wananchi ni cha kijasiri kinapaswa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi na uzalendo wa nchi hii inayochumwa na wachache,huku wengine wakibaki watupu.tuwe wajasiri jamani,tuliweza na tutashinda.
 
wamefanya maamuzi wakiwa na hasira,wakitulia watarudi kundini kwao walikotoka,si watu wa kuwafurahia haraka haraka.
 
Back
Top Bottom