VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Rais Magufuli leo amezungumza na Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya. Lengo hasa lilikuwa ni kuwashukuru vigogo hao kwa kufanikisha ushindi wa Rais Magufuli na CCM kwa ujumla.
Alipokuwa akizungumza Rais Magufuli,hasa kuhusu kutumbua majipu na namna ya utumbuaji huo,vigogo wa chama walikuwa wakiripuka mara kwa mara kumshangilia Rais. Hadhira ilionekana kuendana vyema na scripts za kikao cha leo.
Rais Magufuli anakaribia kutwaa Uenyekiti wa CCM Taifa. Atakapokuwa Mwenyekiti,utumbuaji utahamia chamani kutoka kwa watumishi wa umma. Ingawa chama kimeshaanza kubana matumizi na kuleta maumivu yasiyo na ganzi,utumbuaji wa nafasi hauko mbali kuanza. Leo viongozi wamejichora kama walio pamoja na Rais. Je,wanachama na viongozi wa CCM tutashangilia hadi mwisho?
Isije ikawa mkuki kwa nguruwe..!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam