Uchaguzi 2020 Wana Arusha tumrudishieni Dkt. John Magufuli asante ya kufikisha usafiri wa treni Arusha, kwa kuifuta CHADEMA hapa mjini

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,070
3,705
Hapo vipi!

Ni kwa muda mrefu Arusha imezorota kimaendeleo,mpaka vimikoa vidogo vinakua kasi ukilinganisha na Arusha yenye fursa nyingi za kiuchumi.

WanaArusha nyie ni mashaidi juu ya kupwaya na kulala kwa fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Arusha.

Arusha kama miaka kumia imegeuzwa na wapinzani kama ndio kitovu cha harakati na sehemu ya kuanza kumwaga damu eti kwa lengo la ukombozi.Arusha imekuawa na historia mbaya ya machafuko ya kisiasa, maana yake, wapinzani wamebadilisha image ya kutoka mji wa kistaarabu na tulivu na kuwa kitovu cha machafuko ya kisiasa.

Tunakumbuka Arusha kwa miaka ya nyumba ilikuwa ni mji ambao serikali ilipendekeza kufanyia mikutano yake ya kimataifa kwasababu ni mji ambao una hali ya hewa nzuri na hotel za kutosha za zenye hadhi ya kimataifa.

Ila baada ya machafuko haya ya kisiasa, imefuta kabisa mambo kama haya ambayo pia ilikuwa inasababishs mzunguko wa pesa hapa mjini.

Pia sekta ya utalii imepwaya sana,watalii ambao ni wazungu wanaogopa sana kufanya utalii maeneo ambayo yanamachafuko ya kisiasa,hivyo hali hii imesababisha watalii kupungua sana katika mkoa wa Arusha, mikutano ya East Afrika mara nyingi huwa inafanyia Dar..badala ya Arusha ambayo ndio ilikuwa makao makuu ya East Afrika. Hizi nilizotaja ni fursa chache tu kati ya fursa nyingi zilizopotea katika mkoa wa Arusha.

Kitendo cha Rais Magufuli kufufua Reli na kufikisha Arusha,tafsiri yake ana imani na fursa zilizopo katika mkao huu,Hivyo tukiifuta hichi chama chenye kuleta machafuko hapa mjini itakuwa tumemrudishia asante Rais Maghufuli na serikali yake itaanza kuipa Arusha hadhi yake kama jiji la kiamataifa Tanzania.

Hawa wapinzani hawajawahi kuleta maendeleo yeyote hapa Arusha, zaidi ya kusababisha mkoa huu udumae kama Kilimanjaro. Kwa anayebisha ataje maendeleo yaliyoletwa na Lema na chama chake.

Hizo barabara zilizojengwa ndani ya mji wa Arusha ambayo chadema inatumia kama ngao,ya kuwadanganyia hao wafuasi wake ni project ya World Bank iliyoanza kipindi cha Kikwete.

Ni YEYE Magufuli2020#
 
Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi..watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei...chadema kweli inawanachama wenye akili ndogo kweli.
Hizo ni propaganda za kitoto sana!! Hiyo mikoa ambayo ndiko kuna CCM kila sehemu kuna maendeleo gani? Pamoja na kuimalisha reli ya kati kuna bidhaa gani imepungua bei hasa kanda ya ziwa, nenda bukoba /mwanza/shinyanga /katavi kaulizie bei ya cement, nondo.

Ukishaharibu uchumi mdogo mdogo kila sehemu kuna haribika, kila leo gharama za uzalishaji, kodi zinapanda eti utegemee bei ya bidhaa ishuke kisa reli?!! Kingine hizo ni siasa za kishamba eti mahali fulani sikupata kura hivyo sipeleki maendeleo wakati kodi zao unazichukua!!!
 
Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi, watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei. Chadema kweli ina wanachama wenye akili ndogo kweli.
Inamaana hiyo miaka 30 mara ya mwisho kufika ulikuwa unawalisha wewe? Twaweza hawakukosea walivyosema CCM inapendwa na wasio soma ,masikini ,wazee ,warugaruga etc unahakisi 100% takwimu za twaweza.
 
Chadema wajenge treni wamewai kuongoza nchi na kupanga matumizi ya bajeti ya nchi?

Una elimu gani kwani Ndugu? Naweza kuwa naelezana jambo na mtoto wa form three hapa!!
Kizingizio kukamata dola..hata maendeleo yanayopimika kwa kiganja cha mkono katika majimbo yenj imewazhinda..haya maendeleo makubwa mtayaweza?
 
Ongeza viwango a kufikiri we sijui nikuite kitu gani Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi, watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei. Chadema kweli ina wanachama wenye akili ndogo kweli.
Waulize wa Shinyanga na Mwanza reli ipo jee sasa hivi kuna mabehewa yanaenda huko?
Hizo zinaitwa danganya wajinga (kama wewe) ili kuwaaminisha
 
Hiyo Chadema katika majimbo yake imejenga treni ya kisasa?kama imeahajenga huko basi ndio utoe kauli kama hizi.
Huna ufahamu wa mambo! Serikali iliyopo madaraka inapanga budget yote, mapato na matumizi. Serikali hiyo iliyopo madarakani inawajibika kujenga miundombinu, kwenye majimbo na mikoa yote, bila kujali ina wawakilishi wa chama tawala ama upinzani. Kujenga barabara, kuleta treni Arusha, siyo kitendo cha hisani, ni jukumu lao, na tunawalipa kwa pesa zetu za nyanya, na misaada kutoka kwa ‘mabeberu’ (Mungu atusamehe kwa ubaguzi) Tunawalipa kufanya hizo kazi, na hiki kipindi wanaomba ajira kwetu Watanzania.
 
Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi, watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei. Chadema kweli ina wanachama wenye akili ndogo kweli.
Siku wakikupakia kukupeleka Kisutu kwa money laundering ndiyo utajua hujui.Endelea kufurahia unyonge wako!
 
Back
Top Bottom