Wana-apolo wateka gari lenye mchanga wa tanzanite | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana-apolo wateka gari lenye mchanga wa tanzanite

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Dec 2, 2007.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,094
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wana-apolo wateka gari lenye mchanga wa tanzanite
  Na Neil Bwindiki, Simanjiro


  KUNDI la Wana-Apolo 200 walioko katika eneo la Mgodi wa Madini ya Tanzanite One wa Mererani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, wameliteka lori dogo lililokuwa likisafirisha mchanga wenye madini hayo mali ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani Arusha na kupora viroba vilivyosheheni mchanga huo.


  Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Luther Mbutu, amethibitisha tukio hilo lililotokea juzi saa 11 jioni katika eneo la kijiji cha Naisinyai kilichopo katika barabara kuu inayotoka eneo la mgodi huo kuelekea uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro (KIA).


  Alisema, lori hilo lenye mali ya Leonard Kavishe, mkazi wa Kaloleni, mkoani Arusha lilitumika kubeba mchanga huo kutoka kwa mwekezaji wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo baada ya kuomba ili aweze kupata fedha za kuendesha mradi wao.


  Kamanda Mbutu alisema baada ya kutoka katika eneo hilo la mgodini, lilipofika katika eneo hilo, dereva wa gari hilo, Davis Geoffrey (27) mkazi wa Arusha, aliwakuta baadhi ya wana-apolo wakiwa wamelala barabarani.


  Alisema aliposimama, alivamiwa na kujeruhiwa mkononi na gari lake kushambuliwa kwa mawe kupora viroba hivyo ambavyo thamani yake bado haijajulikana.


  Kamanda Mbutu alisema, baada ya kupora, wana-apolo hao walitoweka kusikojulikana na kuliacha gari hilo barabarani na kwamba, dereva huyo aliyejeruhiwa, alisaidiwa muda mchache baada ya askari polisi kufika eneo la tukio.


  Alisema baada ya kutekwa, lori hilo liliharibiwa na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh800,000 na limehifadhiwa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo Mererani.


  Kamanda Mbutu alisema polisi imefuatilia kujua mchanga huo ni mali ya nani baada ya kuwapo kwa uvumi kuwa ni mali ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na kubaini kuwa ni mali ya UV-CCM wilayani humo kutokana na kibali kilichotolewa na kuidhinishwa na Katibu wa Vijana Mkoa wa Arusha, Mfaume Kizigo.


  Naye Ole Sendeka akizungumza kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam, alithibitisha tukio hilo na kukanusha uvumi kuwa mchanga huo kuwa ni mali yake na kusema kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi hiyo kulichafua jina lake.


  mwananchi


  kazi hiyo sio ndogo hapa panahitaji utfiti wa kutosha haya mambo yanaendaje?
   
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Dec 2, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,346
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  swali kubwa hapa kwangu ni kuwa kunani hata kampuni hiyo iwape UVCCM mchanga wa Tanzanite? Siku UVCCM wanafanya biashara ya madini? Leaves a lot to be desired!
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kila mwanasiasa wa CCM anachukua pale anapoweza...nchi yetu inatia huruma.
   
 4. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2007
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii inadhihirisha kuwa "WADANGANYIKA" wamechoka na blabla za maisha bora kwa kila mtanzania huku "Watu wanachukua Chao Mapema" Watu wakiwasema viongozi, jibu linakuwa leteni ushahidi. Sasa nao wameamua kutumia staili hiyo kwa sababu "Mnyonge Siku zote hana cha kupoteza"

  Tanzania inaendelea kubadilika siku hadi siku; kuanzia kumrushia mawe Mkuu wa Wilaya , Zomea zomea na sasa kuchukua kile wanachokikosa kwa nguvu. Hii ni dalili mbaya kwa future ya nchi. Tusiendelee kujidanganya kuwa tuna AMANI wakati tumekalia BOMU kubwa ambalo ni suala la wakati tu. JK salam hizo zinatosha kuwafanya muangalie nyuma kabla hamjaiangamiza nchi.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,595
  Likes Received: 20,008
  Trophy Points: 280
  Jamani hivi ni utaratibu gani unaotumika ili kuweza kupata huo mchanga wa Tanzanite/dhahabu? Nauliza ili Watanzania wengine wazijue taratibu hizo na wao waombe kama ni kupewa au kununua mchanga huo. Juzi juzi tulisikia baadhi ya mawaziri wana migodi yao, sasa tunasikia kwamba UVCCM walikuwa na machanga wa Tanzanet wakati huo huo Watanzania tulio wengi hatujui ni taratibu zipi zinazotumika kumiliki mgodi au mchanga.

  *~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  Wanaapolo wapora madini ya mamilioni CCM

  na Mwandishi Wetu, Simanjiro
  Tanzania daima

  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni wachimbaji wadogo wa madini, juzi walivamia gari lililobeba mchanga wenye madini mali ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Simanjiro na kuiba kiasi kikubwa cha madini ya tanzanite yenye thamani ya mamilioni ya shilingi.
  Imeelezwa kwamba, waporaji walifanikisha wizi huo kwa kutumia silaha za jadi.

  Habari zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili kutoka Mirerani, wilayani Simanjiro zinasema kwamba, madini hayo yaliporwa juzi, majira ya saa tisa alasiri katika Kijiji cha Naisinyai na kundi la watu wanaosadikiwa kuwa wachimbaji wadogo wa madini, maarufu kwa jina la Wanaapolo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Luther Mbutu, jana alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa waporaji walioonekana kuzinasa mapema habari kuhusu mchanga wa madini hayo, walilivizia gari lililobeba mchanga na lilipokaribia mahali walipokuwa, walitanda haraka katikati ya barabara.

  Kwamba, baada ya kuona gari hilo linakuja bila kupunguza mwendo, waliamua kulala chini katikati ya barabara, jambo lililomlazimu dereva kusimama, pengine bila kutambua kwamba huo ulikuwa sawa na ushindi kwa waporaji hao.

  Taarifa za awali za kipolisi zilieleza kuwa, kundi hilo la watu, wakiwa na silaha mbalimbali za jadi waliliteka gari aina Isuzu Canter, lenye namba za usajili T 443 AAR, mali ya mtu binafsi lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa jina la Davis Japhet (27).

  Watekaji hao wakiwa wamelala chini, walilishambulia kwa mawe gari hilo na kupasua kioo chake cha mbele na baada ya kumteka dereva, walimjeruhi kwa sime, kisha wakaanza kuyasaka madini hayo kwenye mchanga.

  Taarifa hizo za kipolisi zilieleza zaidi kuwa, mchanga huo ambao ndani yake kulikuwa na madini ya tanzanite, ulitolewa na Kampuni ya Tanzanite One kwa UVCCM, Wilaya ya Simanjiro.

  "Inashangaza kweli, watu wameteka gari, wamemjeruhi dereva kwa sime, wameiba madini yenye thamani kubwa! Dereva huyu amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, anakopatiwa matibabu zaidi.

  "Madini hayo ya tanzanite yalikuwa yamechanganyika kwenye mchanga ambao imegundulika kuwa ulitolewa na Kampuni ya kuchimba madini ya Tanzanite One kwa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Simanjiro.

  "Kinachoshangaza hapa, ni hawa watu kuamua kusafirisha mchanga wenye mchanganyiko wa madini yenye thamani kubwa bila ya kuomba msaada wa ulinzi wa Jeshi la Polisi, msaada ambao unatolewa bure, haulipiwi!" alisema kwa mshangao Kamanda Mbutu.

  Alisema pamoja na masako mkali unaofanywa na jeshi hilo, bado halijafanikiwa kuwanasa waporaji hao na kwamba, dalili za awali zinaonyesha kuwa hawatakuwa tena eneo hilo.

  Hata hivyo, alieleza kuwa jitihada za polisi kuwasaka zinaendelea na watakapopatikana watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

  Alisema katika tukio hilo la kupora madini hayo, hakuna uharibifu mkubwa wa mali uliosababishwa na waporaji, lakini taarifa za awali zinadai kuwa, madini hayo yanaweza kuwa na thamani ya mamilioni ya shilingi.
   
Loading...