Wamtaka mwekezaji wa RITES aondoke na injini zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamtaka mwekezaji wa RITES aondoke na injini zake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Oct 5, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  4th October 2009


  [​IMG]


  [​IMG]
  Injini ya treni.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wamemtaka mwekezaji wa kampuni ya RITES kuondoka yeye na injini zake 10 nchini India alizozisimamisha kwa kuwa ameshindwa kuiendesha kampuni hiyo na kwamba wao wataendelea kufufua injini za hapa nchini vinginevyo amani itatoweka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wafanyakzi hao walisema hayo wakati wa kikao cha pamoja cha wafanyakazi hao na Mkurugenzi Mtendaji wa RITES Hundul Chondry kilichodumu kwa muda wa masaa matano mfululizo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, kikao hicho hakikufikia muafaka kutokana na wafanyakazi hao waliotaka kupata muafaka juu mwekezaji huyo kuondoka na kuwaachia wawekezaji wengine wenye uwezo waje wawekeze ili kuwakomboa Watanzania.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]" Tunataka mwekezaji ambaye atatusaidia, wewe huna pesa na unategemea misaada, hii inatuonyesha wazi kuwa huna uwezo wa kuendesha TRL, Jing'atue," alisema mmoja wa wafanyakazi Moses Mwembelezi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wafanyakazi hao walimwambia mwekezaji huyo kuwa gharama za kukodisha injini na mabehewa hayo yaliyotoka nchini India ni sh. 600,000 kwa siku ambapo ni hasara kubwa kwa Serikali ukilinganisha na injini na mabehewa ya hapa nchini yaliokuwepo tangu enzi ya TRC hayana gharama.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Walisema kuwa injini za hapa ambapo awali mwekezaji huyo alipoingia alisema hazifai na kuamua kwenda kukodisha India kumbe hizo ndio hazifai kabisa na kuongeza kuwa walichoamua ni kuzifanyia matengenezo na kuzitumia.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wafanyakazi hao ambao hadi mwisho wa kikao walionekana kutopata muafaka walisema hawatakubali tena kumsikiliza mwekezaji huyo na kuongeza kuwa ili amani iendele kudumu mahali hapo ni vema mwekezaji huyo akaondoa wazo la kurudisha injini zake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wake mwekekezaji huyo Chodray alisema kuwa yeye hawezi kutoa maamuzi kwamba ataondoka kwa shinikizo la wafanyakazi na kudai kuwa ataondoka baada ya makubaliano na yeye na serikali ambao ndiye mbia mwenzake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kikao hicho ambacho kilikuwa na mvutano mkali kutokana na majibu yaliokuwa yakitolewa na mwekezaji huyo kutowaridhisha wafanyakazi hao hakikupata muafaka na mwekezaji huyo kuamua kuondoka na kutoa ahadi ya kurudi tena huku wafanyakazi hao wakipinga vikali kuongea tena na mwekezaji huyo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wafanyakazi hao waliwaambia waandishi wa habari hawakutaka kuongea na mwekezaji huyo kwa madai kuwa anakuja kuwasanifu tu na si kuwapa ongera kwa kufufua mashine hizo ambazo kwa sasa zimeongeza uzalishaji mkubwa kutoka tani 5,000 hadi kufikia tani 13,000 kwa siku kwa kutumia injini za hapa nchini.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  http://www.ippmedia.com/
   
  Last edited: Oct 5, 2009
 2. N

  Nanu JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Is it true bei kukodisha ni laki sita kwa siku? Can you verify if you have any reliable sources?
   
Loading...