kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,307
- 12,602
Kila nikiwaona watu wa dini wananikumbusha namna ukoloni ulivyofika Afrika ikiwemo Tanzania.
Hawa ni watu ambao walikuja Kwanza kabla ya wakoloni (wanyonyaji) kufika na kuua machifu wetu waliokataa kunyonywa na kutawaliwa. Jambo la kushangaa na kutisha hawa watu wa dini ( missionaries) walikaa, waliishi na kushirikiana vizuri sana na wakoloni wetu waliohamisha rasilimali na watu wetu kwenda kwao. Hawakuonyesha kukerwa na vitendo vya wakoloni hata kidogo, wakoloni walikuwa wanakwenda kusali kwenye makanisa na misikiti yao bila kukemewa vitendo vyao vya kupora mali za wanyonge kwenda ulaya na uarabuni.
Hii ilimaanisha kuwa kupora mali za wanyonge ilikuwa sawa na halali kwa watu wa dini. Hii inanifanya hadi leo niamini kuwa makanisa na misikiti ni lango kuu la uporaji wa mali za wanyonge hata leo, maana quran na Bible waliyokuwa wanaitumia wakati wa ukoloni ni hii hii wanayoitumia leo.
Kama tusiposhituka dini zitatufanya Afrika tuendee kuwatumikia wazungu na waarabu milele Kwa kufahamu au bila kufahamu. Sera zao hazichukii unyonyaji wa aina yoyote hata ikibidi utumwa. Sioni kama kuna tofauti ya mahubiri, vision na mission kati ya wamissionari wale na hawa wa leo. Sikumbuki ni wapi wamionaries walipowahi kuukemea, ukoloni na vitendo vyao vya kibaguzi na kinyonyaji Kwa watanzania.
Kama Rais Magufuli akitaka kuleta ukombozi wa kweli wa taifa hili atupie macho mara tano tano misikiti na makanisa, huu ndio mkono, macho na masikio wa mkoloni uliobakia Afrika, ukisaidiwa na World Bank, IMF na World Trade Organisation.
Kitulacho kiko nguoni mwetu, akili Yao yote iko ulaya, Marekani na Uarabuni. Ukiunganisha ardhi yooote wanayoikalia Afrika, vitagauchumi vyoote wanavyovimiliki Afrika na Kodi wanayotulipa waafrika utagundua kuwa kazi bado tunayo waafrika, ukoloni bado upo na ndyo maana aAfrika yote kusini mwa jangwa la Sahara Kwa pamoja haipigi hatua.