Wamisri wa kale walikuwa weusi(Africans)

Wanaweza tena sana tu. Huwaoni zeruzeru?

Binadam wote asili yao si weusi wala weupe, ni brown. Ukipungukiwa "melanin" unakuwa mweupe, "melanin" zikizidi unakooza na kuelekea kwenye weusi.
Sasa itabidi nikubali tu pia mke wangu mwarabu akipata mtoto mweusi maana melanin itakua imepungua
 
Makaburu hawana hata miaka 1000 sauzi.wajuzi juzi tu.kitendo cha kufukuza watu hakifanyiki kama unavofukuza mbwa mwizi.ni gradual process.

Mfano mwingine ni Red Indians wa Marekani walivyomezwa. Pia namna Wachina wanavyoingia katika nchi mbalimbali na kuanzisha China Cities. Wasipodhibitiwa watazijaza nchi hizo. Kisha wataandika historia kadri watakavyo.
 
Uarabu ni lugha na Kiarabu ni lugha namba moja Afrika. Fikiri.
Imekua hvo sababu ya Ottoman empire,kwa utawala wao wa Afrika kaskazini kwa zaidi ya miaka 400 na hii imetokea in common era(AD) au after Christ. miaka maelfu na maelfu baada ya utawala wa Misri kuanguka.Wagiriki walipita,wakapita Warumi ndio wakaja Waarabu.
 
Nilimuambia bukoba boy kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba sisi Wabantu tukawa ndiyo wale Wasraeli halisi kwa maana ya wana wa Yakobo...

Kwasababu hiyo,ukiangalia maandiko Wayahudi [Waisraeli walioishi kusini mwa Israeli baada ya mgawanyiko wa mwaka 670 b.c] na pia Waisraeli wa kaskazini mwa Israeli walimkataa masihi,na siyo hilo tu bali walikaidi maagizo ya Mungu....

Kwenye Kumbukumbu 28 kuna baraka na laana kama watafuata maagizo yake na kama watayakaidi.Sasa ukisoma hizo laana kwakuwa walikwenda kinyume na maagizo ya Mungu utaona kabisa utadhani mwandishi alikuwa anatuangalia sisi kwa yale yanayotupata....

Ndiyo nikasema kwamba hii inatuhusu kama nitakuwa sahihi kuhusu Wabantu kuwa Waisraeli halisi....
Wabantu ni wa kaskazini walikataa,hao wa Kusini waliokubali ni akina nani?
 
Sasa itabidi nikubali tu pia mke wangu mwarabu akipata mtoto mweusi maana melanin itakua imepungua
Haiwezi kua imepungua akawa mweusi.upungufu wa melanin ndio unaoleta rangi ningine apart from weusi.so wewe mwarabu una uoungufu wa melanin.
 
Naona baadhi ya wachangiaji wanasema Israel ilikuwa ya watu weusi jambo ambalo sio kweli pia Yesu kuwa mweusi. Yote haya ni kutokana na fikra finyu, kukosa vitu vya kujivunia hususan maendeleo ya dunia kwa hivyo watafiti wanajaribu na wameweza kwa kiasi fulani naweza sema kuaminisha watu kwamba historia iliyopo ni ya uongo.
Kwa kipindi kirefu sasa duniani katika uvumbuzi au ugunduzi watu weusi wamekuwa nyuma au wachache katika maswala mbalimbali ya sayansi na maendeleo kwa ujumla. Na moja ya sababu kubwa ya kuwa hivyo "wamekuwa" wakidai ni kutokana na ukoloni na kwa namna moja au nyingine waweza kubaliana nao lakini ukweli ni kwamba historia ya Israel,Egypt sio ya mtu mweusi. Uwepo wao (weusi) sio kigezo cha kudai na kusema wao ndio walikuwa watawala na kwamba wameporwa historia yao.
Ngoja nikuulize swali fikirisi sababu umejaa white supremacy doctrine
Wazungu wanasema wao ndio wamewafunxisha waafrika kusoma na kuandika na maelezo na mafundisho yalipitishwa kizazi kimoja mpaka kingine kwa njia ya mdomo.

Sasa inakuaje lugha karibia zote za wabantu wanayo maneno yao ya asili yanayatafsiriwa kama "soma" na "andika" ambayo hayajatoholewa toka lugha zingine ngeni,inakuaje wawe na msamiati wa jambo ambalo walikua hawalijui?
 
Uarabu ni lugha na Kiarabu ni lugha namba moja Afrika. Fikiri.
Wamisri wa kale hawakuongea kiarabu,waliongea lugha ambayo haina uhusiano wowote na "endo european" languages kama Hebrew au Arabic..Hjj imekaaje?
 
Ngoja nikuulize swali fikirisi sababu umejaa white supremacy doctrine
Wazungu wanasema wao ndio wamewafunxisha waafrika kusoma na kuandika na maelezo na mafundisho yalipitishwa kizazi kimoja mpaka kingine kwa njia ya mdomo.

Sasa inakuaje lugha karibia zote za wabantu wanayo maneno yao ya asili yanayatafsiriwa kama "soma" na "andika" ambayo hayajatoholewa toka lugha zingine ngeni,inakuaje wawe na msamiati wa jambo ambalo walikua hawalijui?

Wazungu walipokuja pwani yetu ya Zenj walikuta watu wanajuwa kusoma na kuandika.

Walikuta Kilwa nyumba za Ghorofa wakati kwao hawaijuwi. Walikuta Kilwa watu wanatumia hariri kutoka China wakati wao hata njia ya kwenda India tu walikuwa hawaijuwi. Walikuta kuna ilm na mfumo wa ilm wa hali ya juu. Roho ikawauma.

Waliporudi, wakapiga piga mizinga yao, wenyeji waka "take cover" msituni. Wao wakaingia, kitu cha kwanza wakaanza kusomba vitabu vyote walivyoweza kubeba walivyoshindwa kuvibeba wakavitia moto.

Soma kitabu cha empires of the monsoon.
 
Wamisri wa kale hawakuongea kiarabu,waliongea lugha ambayo haina uhusiano wowote na "endo european" languages kama Hebrew au Arabic..Hjj imekaaje?

Mara kwa mara humuhumu JF nimekuwa nikielezea maana ya Kiarabu na Uarabu ni nini, pitia pitia posts zangu utanielewa.
 
Rangi ya n'nya.
Nimekupata vyema,kuna udongo fulani hivi wanatengenezea majiko yale ya udongo au ule udongo maarufu wa Kigoma wanaotengenezea pemba,nadhani ni rangi ile ile....

Sasa basi,ulisema kuwa kuna kinachofanya mtu anakuwa mweupe sana au mweusi sana kama kikipungua.Je ni nini kinafanya huyo huyo aliyepungukiwa na hicho kinachofanya ngozi kuwa nyeusi awe na nywele za namna fulani hapo hapo?

Pia,watu wa rangi uisemayo ya brown mara nyingi ni wale wanaokuwa na nywele za kipilipili,kama wale wanaoishi kwenye misitu ya Botwana kama sikosei ambako alitokea yule Bush Man maarufu kwenye filam ya "gods must be crazy" hili linakuwaje?

Inaonekana ni kama "makosa" yalifanyika kupatikana race nyingine maana uliposema tu kitu fulani kikipungua au kuongezeka basi haya mabadiliko ndiyo yanatokea na hii inaonesha ni kama "makosa" hivi na siyo kwamba Mungu alifanya kwa makusudi kabisa kuwa na tofauti hizi,yaani haikutokea bahati mbaya.....

Hebu nieleze hapo....
 
Nimekupata vyema,kuna udongo fulani hivi wanatengenezea majiko yale ya udongo au ule udongo maarufu wa Kigoma wanaotengenezea pemba,nadhani ni rangi ile ile....

Sasa basi,ulisema kuwa kuna kinachofanya mtu anakuwa mweupe sana au mweusi sana kama kikipungua.Je ni nini kinafanya huyo huyo aliyepungukiwa na hicho kinachofanya ngozi kuwa nyeusi awe na nywele za namna fulani hapo hapo?

Pia,watu wa rangi uisemayo ya brown mara nyingi ni wale wanaokuwa na nywele za kipilipili,kama wale wanaoishi kwenye misitu ya Botwana kama sikosei ambako alitokea yule Bush Man maarufu kwenye filam ya "gods must be crazy" hili linakuwaje?

Inaonekana ni kama "makosa" yalifanyika kupatikana race nyingine maana uliposema tu kitu fulani kikipungua au kuongezeka basi haya mabadiliko ndiyo yanatokea na hii inaonesha ni kama "makosa" hivi na siyo kwamba Mungu alifanya kwa makusudi kabisa kuwa na tofauti hizi,yaani haikutokea bahati mbaya.....

Hebu nieleze hapo....

Soma kuhusu melanin.


Soma kuhusu origin of human kind, utakuta kuwa duniani watu wa mwanzo ni hawa wa hapa kwetu ambao leo tunawaita Wambulu na Kabila zinazozunguka huko Mbulu.
 
Wabantu ni wa kaskazini walikataa,hao wa Kusini waliokubali ni akina nani?
Kwa namna nijuavyo ni kwamba baada ya uvamizi wa Waashuru [Assyrian] kule Israeli ya kaskazini na kuwachukua mateka Waisraeli ambao walikuwa ni makabila 10 walizaana na Waashuru na kuanza kuabudu miungu wengine na kuiacha njia ya Bwana na baadaye walianza kuuawa ndipo wakakimbilia west Africa na kuanzisha empire huko...

Nikija kwenye nchi ya Judea [nchi ya Yuda au Israeli ya kusini],wakati wa uvamizi wa Rumi mwaka 70 A.D,majeshi ya Rumi yakiongozwa na jemedari Titus walivamia na kuanza kuvunja hekalu lililojengwa na Suleiman na kuua Wayahudi wengi sana....

Historia niliyoisoma inaniambia kwamba asilimia 90 ya askari waliokuwa chini ya Rumi ambao walivamia Israeli ya kusini mwaka huo wa 70 A.D walitokea kwenye makambi ya askari wa jeshi la Rumi ambao walikuwa ni raia au wakaazi wa mashariki ya kati na pia mfalme wa Arabia aliwapa jeshi na nyongoza ya farasi katika uvamizi huo,kwa maana hii askari wengi sana waliovamia Israel ya kusini na kuvunja hekalu la Jerusalem ni askari kutoka Assyria,Arabia na nchi zingine za mashariki ya kati....

Baada ya tukio hili,sehemu pekee waliyoweza kuona ni salama ni kule ambako wenzao walikuwa na siyo Ulaya au kwa majirani zao wa huko mashariki ya kati ambao ndiyo walioshiriki kuvamia nchi yao.Waliamua kuwafuata wenzao huku west Africa na kuendeleza maisha kama kawaida....

Waliendelea na maisha yao na ndipo walipopatikana Wabantu ambao walianza kutapakaa maeneo ya kusini mwa jangwa la Sahara hadi kusini mwa Africa.Baada ya miaka mingi wale wale watesi wao [Wazungu] walikuja tena kuwakuta huku Africa na kuwapeleka utumwani kwa meli [kama Kumbu 28 inavyosema] na kuwatesa na kuwaua kama walivyofanya zamani....

Walikwenda maeneo yote ambayo walikuwepo Wabantu [magharibi mwa Afrika na kusini mwa jangwa la sahara] Waliwapeleka utumwani kwa kuwatesa sana na kuendelea kuwaua kinyama.Pia,majirani zao wale wa mashariki ya kati [Waarabu] walikuja kuendeleza waliyoyafanya zamani kwa watu hawa kwa kuwauza kwa wazungu kama watumwa....

Kwa maana hii,kujibu swali lako ni kwamba wale wa kusini mwa Israeli nao walikuja huku Afrika pia lakini baadaye na waliwakuta wenzao tayari wameshaishi huku zamani tu.Hili utaliona kwenye kitabu cha matendo ya mitume ambapo kuna mahali mitume walikutana na towashi akitokea huku Afrika [Kush] akiwa na chuo cha nabii Isaya akielekea Jerusalem kuhiji,hii ilikuwa ni kabla ya tukio la mwaka 70 A.D.....

Kwa maana hiyo,kama historia ninayokuleza iko sahihi 100% basi huo ndiyo ukweli wenyewe....
 
Soma kuhusu melanin.


Soma kuhusu origin of human kind, utakuta kuwa duniani watu wa mwanzo ni hawa wa hapa kwetu ambao leo tunawaita Wambulu na Kabila zinazozunguka huko Mbulu.
Ni nini kinafanya mtu aliyepungukiwa melanin awe na nywele za tofauti pia?

Nauliza hivi maana mfano wale walemavu wa ngozi [zeruzeru na kwa msingi wa hoja yako hata wazungu nao ni walemavu wa ngozi] wanakuwa na nywele zile zile za kipilipili japokuwa zinakuwa na rangi tofauti tu,sasa inakuwaje kwa hawa wengine? Kwanini hadi nywele zinabadilika?

Unakubali kuwa hizi tofauti ni kutokana na "kupungua" kwa melanin au Mungu alidhamiria kufanya tofauti hii?
 
"Misri ilikua ni Afrika kwa maandishi yake,utamaduni wake na namna yake ya kufikiri" .Hivi ndivyo anavyohitimisha mtaalamu wa masuala ya kale ya Misri(Egyptologist) raia wa Ufaransa Jean Vercoutter na mpinzani wa Cheikh Anta Diop katika mkutano wa Cairo juu ya utambulisho wa Wamisri wa kale.

Mkutano wa Cairo ulifanyika Mwaka 1974,UNESCO taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuamua masuala kama hayo,ilikubali kua Cheikh Anta Diop na Theopile Obenga wako sahihi kua Misri ya kale ilikua ni ustaarabu(Civilazation) wa kiafrika katika nyanja zote,hii ilitokea baada ya malumbano makali kati ya Egyptologist wawili wa Kiafrika na wenzao wawili.

USHAHIDI

Tofauti na mtu atakavyoelekezwa kuamini,Misri ilikaliwa na watu waliokua wanahamia kutoka Kusini kwenda Kaskazini na watu weusi walioitwa Anu. Hawa ni watu waliotokea Kusini mwa Afrika na maeneo ya maziwa makuu ambao walilowea kwanza ilipo kwa sasa Sudan na Kusini mwa Misri.Ni Watu jamii ya Anu polepole ndio waliofuata bonde la mto Nile na kuitia Kaskazini yote mpaka Delta katika himaya yao.
Ustaarabu wa Misri una mizizi yake kutokea Kusini mwa Afrika na eneo la maziwa makuu sababu eneo hili ndio binadamu wa kwanza walizaliwa na ndio bakibaki(traces) za ustaarabu wote wa binadamu unaweza kuonekana( rejea mambo ya Oldupai Gorge) na hii ndio sababu kwa nini eneo hili Wamisri wa kale waliliita Ta Ntjer maana yake ardhi takatifu au ardhi ya Mungu.

Na kwa urithi huu uliopatikana katikati mwa Afrika kwa miaka 170,000 uliowezesha Anu kuijenga Misri kutokea kusini kwenda kaskazini.Hisabati, Kuandika, Kilimo, Usanifu Majengo, dini nakadhalika vyote vilianzia Afrika na Sudan na vilikuzwa zaidi na Wamisri.

Mafarao wa kwanza walitawala upande wa kusini kwa maelfu ya miaka,ilikua ni Msudani alieitwa Nare Mari ndie aliyemaliza kuiteka Delta ya mto Nile na Kuunda Falme ya Misri(Dynasty) iliyoungana mnamo mwaka 3300 BC.

Jina la Misri na Wamisri

Jina walilojipa na jina walilolipa bara lao pasi na shaka linaonyesha waziwazi asili(race) yao. walitumia jina(mzizi) Kam/Kem ikiwa na maana iliyopakwa makaa(coal coated) kwahiyo walikua ni weusi.Ambao ni sawa na Kemi/Kembou/Kheum/Kala ikimaanisha coal(makaa), iliyounguzwa , nyeusi katika Lugha nyingi za Kiafrika.

Michoro na Sanamu zote za Farao zinaonyesha waziwazi hawa ni watu weusi,kuanzia utawala wa kwanza(first dynasty) mpaka uvamizi wa Wagiriki.
Narmer-1st-Dynasty.jpg

Ingawa wamejaribu kuziharibu pua zao ila tazama walivyo na midomo mipana.
images


-Ushahidi mwingine ni kipimo cha vina saba na majaribio katika ngozi kwa kuangalia uwingi wa melanin.
-Familia sawa ya Lugha ,tamaduni sawa na dini sawa na waafrika wengine kwingineko.
Egyptologist wote wa Ulaya walishindwa kuonyesha uwiano kati ya Kimisri na lugha za Endo European ambazo ni ''semitic'' kama Arabic na Hebrew,Ni Cheikh Anta Diop katika miaka ya 50 aliyegundua usawa kati ya Wolof(Lugha yake) na Kimisri
-Mfumo wa familia ulioegemea upande wa mama(matriachy),jinsi mazishi yanavyofanywa na mpangilio wa ufalme,kila kitu katika tamaduni za Misri kinafanana na tamaduni za kusini mwa jangwa la Sahara. Dini ya Misri ambayo imeandikwa sana na inaendelea kuandikwa ni sawa na ile inayofanywa na watu weusi. Misri haikuamini katika Mungu zaidi ya mmoja(polytheistic) na wana sayansi wote wanajua hii na wakapandikiza propaganda kua Misri iliamini katika Miungu ili wainyime Afrika heshima yao kua wao ndio wa kwanza kuabudu katika Mungu mmoja.

Ushahidi mwingine ni kutoka kwa Wasomi wa Ulaya wenyewe mfano Wagiriki wa kale kabisa wanaoheshimika kuja Afrika wanasema Wamisri waliokutana nao ni weusi

Herodotus,anajulikana kama baba wa historia anaandika hakika kabisa Colchians(watu walioishi kando ya Black Sea) wana asili ya Misri(are of Egyptian race) kwa sababu walikua na ngozi nyeusi na nywele frizzy.

Aristotle,penginepo mwenye ushawishi mkuu katika ufikiri wa Kimagharibi anasema wale weusi sana ni waoga,hii ni kwa Wamisri na Waethiopia.

Aeschylus,mwana mashahiri akielezea meli ya Wamisri ikiondoka, i notice the crew with its black members bringing out the white tunics.

hata wakati wa utawwala wa Rumi,miaka 250 kabla ya uvamizi wa waarabu bila kujalisha uwepo wa ngozi nyeupe Misri kwa miaka 600 Ammian Marcellin, rafiki wa mtawala wa Rumi Julius anasema watu wa Misri kwa wingi wao ni wekundu(brown) au weusi.


Kama Wamisri walikua weusi,watu weupe wanatoka wapi?

Ustaarabu wa Misri ulianza miaka 27,000 iliyopita,miaka 19,000 kabla ya kuonekana kwa mtu mweupe.Uvamizi wa kwanza mkubwa wa weupe ulikua ni ule wa mwaka 663 BC wa Assyrians
Baada ya hapa Misri ikaanza kuyumba.ikavamiwa tena na Persia na Wagiriki waliomaliza tawala zote za Misri wakaja Warumi na Mwisho kabisa Waarabu walioingia Misri kama sehemu ya Uvamizi wa Kiislam karibia miaka 1000 baada ya utawala wa mwisho wa wazawa.
Waarabu walivyoingia Misri wazawa walikua wamekimbilia pande nyingine za Afrika kati yao wapo Sonike wa Mali,Akan wa Ghana,Yoruba wa Nigeria, Bassa wa Cameroon na hata Zulu na Xhosa wa Afrika Kusini. Weusi waliobakia Misri walizaliana na wavamizi ambao hiki kizazi kinaitwa Copt.
hii inaelezea kwa nini hawa Copts ni weupe lakini wanaongea BLACK TONGUE .Waarabu hawana lolote kuhusu ustaarabu wa Misri na wako makini kutosema ili wakusanye pesa ya utalii Misri.

Kama Misri ilikua ya weusi,kwa nini weusi hawana akili?

Hili ni swali maarufu sana linaloulizwa na Waafrika waliomeza propaganda ya kua mtu mweusi ni inferior.Lazima ufahamu kua baada ya uvamizi wa wageni Misri iliyumba sana, ila kutoa Misri,Afrika kwingineko ustaarabu ulizaliwa.
Mpaka mwanzo wa biashara ya utumwa ya wazungu,Afrika ilikua imetapakaa Falme nyingi maridadi na ilikua bara tajiri kuliko yote. Hujawahi kujiuliza kwa nini Mansa Musa ambae aliishi karne ya 14 ndie mtu tajiri kuliko wote kuwahi kutokea?(Meet Mansa Musa I of Mali – the richest human being in all history)Ni utumwa na ukoloni ndio umewafanya waafrika wajione wako nyuma. Na haieleweki kwanini tunaambiwa udhaifu wetu ni wa asili tumeweza kujenga ustaarabu ambao ulikuja kuambukiza dunia nzima.
Hii habari ni ngumu kumwingia mtu mweusi sababu haijasemwa na maneno takatifu ya wazungu.

Nimejaribu kutafsiri kutoka
The ancient Egyptians were Black

Mkuu, anaongea ukweli kabisa, watu walikuwa wanakuja Africa kusoma na kujifunza kila kitu kwa sababu Africa ilikuwa imeendelea kupita eneo lolote Duniani. Wagiriki wote maarufu walikuza africa kujifunza elimu ya juu, Hata Musa alieandika vitabu vitano vya kwanza vya biblia elimu yake yote aliipata kutoka Misri. Wale Wamisri wazamani walitokea ndani ya Africa, nchi zote zilizokuwa karibu na river Nile. Nchi Kama Tanzania, Sudan, Ethiopia, Uganda, etc. Civilization ilikuja kutoka nchi hizi na kwenda chini.

Pia Africa ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanzisha (Monotheist religion) Mungu Mmoja ambayo baadaye Judaism, Christianity and Islam will copy. Na kuirudisha tena kwa waafrica na kuwaambia angalia dini nzuri mpya. Leo apya Africa we are tunapigana kwa ajiri ya dini, kwa sababu hatujui historia yetu na tumedanganywa kwa muda mrefu sana.

Unaweza kusoma mwenyewe habari za Osiris, Isis na Horus. Unaweza kusoma zaidi kwenye vitabu vya Dr Cheick Anta Diop (The African origin of Civilization: Myth or Reality?) na Theopile Obenga. (Ancient Egypt and Black Africa: A student's Handbook for the Study of Ancient Egypt in Philosophy, Linguistics and Gender Relations).

Tatizo leo hatusomi historia yetu ya ukweli iliyoandikwa na Waafrica. Pia tv, newspapers, kubwa zinazomilikiwa na wazungu mara nyingi sana hazisemi ukweli kuhusu historia kwa sababu hawapendi ukweli ufahamike.
 
Back
Top Bottom