Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Ni kweli mkuu inafikirisha sana tena sana tu.....
Lakini kikubwa na kibaya zaidi ni kwamba kuna watu weusi hasa kutoka mashariki mwa Afrika walipelekwa utumwani kule India na kuna kijiji kukubwa sana eneo moja kule Inadia wanaishi huko na wanajua kuwa walitoka huku mashariki mwa afrika,nimesahau eneo husika nikikumbuka nitalitaja hapa....
Watu wale walitoka hasa Kenya na sehemu za pwani ya Afrika ya mashariki.Ni masikini wa hatari kabisa kule na serikali ya India ni kama imewatupa hivi.Mkuu,sisi huku tunaishi maisha ya kishenzi lakini wale ni kama wapo shimoni,inasikitisha sana aisee....
Kwanini historia hizi zinafichwa?
Suala la mtu mweusi na uwepo wake duniani imekuwa kama ni laana.Haya ndiyo maana ninasema yana sababu maalum kabisa na siku siyo nyingi tutafutwa machozi haya ya damu siku itakayoutisha ulimwengu kwa namna ya kutisha kabisa.....
Acha tu waendelee kudanganya....
Hao weusi walioko India, hawakuenda huko kama Watumwa,