Wamiliki watishia kufunga hoteli, gesti

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba za Kulala Wageni na Hoteli mkoani Iringa (Iloha) Adam Lameck amesema wafanyabiashara wa huduma hizo wamekataa kulipa tena ushuru wa hoteli hadi watakapoonana na uongozi wa mkoa.

Akizungumza leo katika mkutano wao alisema watalazimika kusitisha utoaji huduma kutokana na mlolongo wa kodi.

“Endapo hatutasikilizwa, tunafunga biashara zetu mpaka hapo tutakapopata muafaka,” alisema.

Mmiliki wa Nyumba ya Wageni, Zakaria Mdeka alisema tangu mwaka 2008 kodi hiyo ilifutwa lakini wao waliendelea kulipa kwa asilimia 10 bila kuzingatia mmiliki anaingiza shilingi ngapi.

Wafanyabiashara hao wamedai wamekuwa wakitozwa mlolongo mkubwa wa kodi zaidi ya 23 ambazo zote zinatakiwa kulipwa bila kuzingatia mmiliki anapata faida kiasi gani.

Chanzo:Mwananchi
 
Dah, isije uwa ile gesti yangu maarufu mitaa ya gangilonga nayo imefungwa.

Sijui nitaponea wapi wiki hii........
 
Kodi zaidi ya 23 kwa mtu mmoja halafu watu wanaondoka na shekeli kwenye mifuko ya sandarusi, jipu bivu kabisa hili lisipotumbuliwa litatumbuka lenyewe
 
Kodi zaidi ya 23 kwa mtu mmoja halafu watu wanaondoka na shekeli kwenye mifuko ya sandarusi, jipu bivu kabisa hili lisipotumbuliwa litatumbuka lenyewe
Wamebana matumizi hoteli na gesti hazipati wateja, halafu wanakamuiwa kodi 23.......wanaotumia bandari waliona huu ujinga wakahamia bandari ya Msumbiji
 
Wamebana matumizi hoteli na gesti hazipati wateja, halafu wanakamuiwa kodi 23.......wanaotumia bandari waliona huu ujinga wakahamia bandari ya Msumbiji
Mapato ya nchi yamepotea kwa ajili ya upuuzi wa wachache
 
Wanatakiwa wasikilizwe na ufumbuzi upatikane. ..
Biashara siku zote ni win win situation. ...
 
Sasa wakigoma tutapigia wapi mechi na kufungana magoli, hizi kodi zitasababisha mechi zianze kupigiwa kwenye vichochoro na kwenye vyoo vya kwenye bar, punguzeni hizo kodi bana
 
Haya beki tatu karibuni Mjiniiiii
Wakifunga waangalie pia Rate ya ongezeko la Ukimwi mkoani Iringa litakuwa limepungua,na wakifungua tu Graph inapanda tena.
Wangeainisha kwanza hizo Kodi.Maana hakuna Kitu hicho cha Kodi 23.
Hizi habari nyingine za juu juu hizi.
 
Isije kuwa zimewekwa ili kupunguza mechi za ugenini! Ni mtizamo tuh.
 
Back
Top Bottom