Wamiliki wa vyombo usafiri, jihadhari na matapeli hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamiliki wa vyombo usafiri, jihadhari na matapeli hawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lambardi, Aug 3, 2011.

 1. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,217
  Likes Received: 4,111
  Trophy Points: 280
  Kwa wenye vyombo vya usafiri wa jumuia...dala dala na malori kuna utapeli mpya umeibuka hasa Dar,wanawafuata ma dereva na kuwaomba no ya wamiliki,wanakutafuta na kukuomba kukutana wanakupa "deal" kuwa kuna kampuni moja inatafuta usafiri wa wafanyakazi......wamependa bus/buses zako zitumike nao sasa wanaomba muongee nao waweke chao juu.....

  baada hapo watakupa docs kibao zote fake,watataka uwalipe fees za tender kama 500$.wanakupeleka nyumbani kwa mmoja wao ndio mtakapoongea hizo deal fake.

  kesho yake watakutafuta tena wanakuambia kuna mwenzao ambae company secretary anataka apoozwe kama 3-5m ili pesa zako zipite fasta (wanaambatana na mhasibu wao) ambae ataku piga sound kuwa yeye ndio ana process malipo,,.......ukiwaambia kwa nini alipwe kabla si asubiri deal likamilike?wanaanza kurudi nyuma na kuona kama umewastukia........

  wastukieni sana na waambie wengine hawa jamaa ni hatari sana.....mimi nimempeleka rafiki yangu tukastukiaa mchezo mzima....tuliwawekea mtego wa polisi wamestuka wakakimbia....wengi wanakaa maeneo ya mtoni,mtongani na tandika
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  DUh Bongo zaidi ya uijuavyo, daily mitego mipya inaibuka.
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,104
  Likes Received: 745
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli na nimeshakutana nao, namba zao za simu ni 0713 624046 ( huyu ndie anayeanzisha kwa kuwafuata madereva anajitambulisha kama alex au makello) likely anabadirisha jina kila mara.

  Kinara mkuu ni 0655 036016 ( ndio boss wao anajitambulisha kama Abbas) kuendana na mmiliki atakavyokuwa ni mweusi jiant kidogo na anasauti nziti hakawii kujifanya shekh.

  Mpambe wao anajitambulisha Doto 0718 586 919, kiukweli maelezo yao haya kamiliki, na wanataka ukaonane nao kwao, kuna nyumba iko Mtoni mtongani ndio ndio wanajitambulisha kwao lakini ni bosheni tu. Kampuni hewa wanataja na vyeo vyao feki.

  Yeyote atakaye kuja anasema anataka kukodisha gari please mkamate kwanza, maelezo akatoe polisi.
   
Loading...