Wamiliki wa viwanda vya nguo wanamshinikiza waziri wa fedha kuwafutia kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamiliki wa viwanda vya nguo wanamshinikiza waziri wa fedha kuwafutia kodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMA POROJO, Jun 22, 2012.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  WAMILIKI WA VIWANDA VYA NGUO WANAMSHINIKIZA WAZIRI WA FEDHA DR MGIMWA AFUTE VAT KWA BIDHAA ZAO KWA KISINGIZIO CHA KULINDA VIWANDA VYA NDANI. HILI LIKIFANIKIWA LITAPUNGUZA MAPATO YA SERIKALI, NA BAYA ZAIDI TANZANIA ITAINGIA MGOGORO MKUBWA NA NCHI ZINGINE ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI. SHINIKIZO NI KUBWA NA LINAONGOZWA NA MBUNGE WA SINGIDA MJINI, MOHAMED DEWJI AKIWATUMIA WABUNGE KADHAA KULE DODOMA.

  MY TAKE: kwa nini wafanyabiashara wakubwa hawataki kabisa kulipa kodi? nini maana yake? hata serikali ikipunguza kodi wao wanataka wasilipe kabisa.... huu ni uchumi wa dunia ipi?
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hawa ndio wahujumu uchumi hawa,si wa kuachwa hivi hivi.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama hawapati faida kiasi cha kutaka wasilipe kodi kabisa ni bora waachane na hiyo biashara huwezi kubaki kwenye biashara inayokuingizia hasara kiasi cha kulumbana na serikali kukufutia kodi yote......
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kodi ndio chanzo pekee cha mapato ambacho serikali inategemea,sasa hawa jamaa kumbe kazi yao wakienda dodoma sio kuwatetea wananchi bali ni kutaka kuneemesha biashara zao.mbaya zaidi wanapokea posho ambazo ni kodi za wananchi hawa hawa maskini.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  Mama Porojo sidhani kama uko sahihi.......
  unahitaji kujifunza sana kuhusu hii sekta...

  hii sekta ya nguo ikisimama itaweza kulipa kodi kuubwa sana na kuajiri watu weengi mno

  tatizo ni kuwa hii sekta iko chali....

  jiulize watanzania wangapi wanavaa nguo za ndani?

  kwa nini?

  Halafu Kigoda sio mbumbumbu aliwahi zungumzia sana hii sekta huko nyuma

  mwisho ni kuwa Vat sio kodi ya wenye viwanda
  VAT ni kodi ya mwananchi

  na VAT ya Tanzania ni kubwa kwa kila sekta..ilipaswa ipunguzwe kwa ujumla sio ya nguo

  tafuta threads za Mwanakijiji kuhusu VAT ya gharama za kuchapisha vitabu uone....

  hii sekta ni muhimu kwa uchumi na Kigoda ni mtu sahihi

  kama wakisema VAT ifutwe na ifutwe tu.......usiangalie kodi kubwa huku Watanzania wanavaa mitumba na nguo za nje

  bora kusiwe na VAT lakini tunavaa nguo za ndani asilimia kubwa na kutoa ajira na kodi zingine
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Dr mgimwa ameanza vizuri lakini asipokuwa makini watamuweka mfukoni na ataharibikiwa sasa hivi.kama kuna aliye naye karibu amfikishie ujumbe kuwa rais wa tano anamkanya na kumuonya vikali asijaribu na wala asiikurubie hiyo zinaa.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  waache ili tuvae mitumba na nguo za China
  huku mnalalamika ajira hakuna?
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mkuu hapo kwenye red hebu fafanua kidogo,unamaanisha gaguro au.samahani lakini.
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kodi ni muhimu,nadhani tusichangnye kati ya kodi na gharama za uendeshaji na uzalishaji mfano umeme
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mohamed dewji si ndio yule mtanzania mwenye asili ya asia???????
  naona ukoloni umeanza kurudi kwa kupitia mlango wa nyuma.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  kuondolewa VAT sio kuondolewa kodi zoote
  na VAT HAILIPWI NA WENYE VIWANDA
   
 12. broken ages

  broken ages Senior Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hili tukilitizama kwa mapana utapata jibu kirahisi sana leo hii nguo nyingi tunazovaa ni za kutoka nje ya Tanzania na hasa mataifa ya Asia lakini zaidi ni kutoka China ambayo haina kodi ya VAT ktk bidhaa zao zinazozalishwa ndani ya viwanda vyao kwa hiyo tukitaka kuingia ktk ushindani wa kweli kwenye bidhaa hii tungeondoa hiyo kodi ili kupunguza bei kubwa kwenye hii halafu tujipime ikiwa tutakuwa na viwanda vya kutosha sana tuongeze kodi kwenye hii bidha kwa ile inayoingia kutoka nje hii itatusaidia kuwapatia watanzania ajira tutapata kodi kutoka kwa wafanyakazi watakaokuwa wameajiriwa ktk viwanda vyetu wenyewe, tutapata bei nzuri na soko laa bidhaa yetu ya pamba hivyo tutakuwa tumeshamsaidia mkulima wa kitanzania
   
 13. broken ages

  broken ages Senior Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  WAAPI? Kwani hiyo kodi wao ndo wanaolipa? Ama ni wewe mlaji.Na kazi ya mbunge ni ipi kama siyo kuwasilisha serikalini kupitia bunge maoni ama kero za wananchi???
   
 14. broken ages

  broken ages Senior Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  WAAPI? Kwani hiyo kodi wao ndo wanaolipa? Ama ni wewe mlaji.Na kazi ya mbunge ni ipi kama siyo pamoja na kuwasilisha serikalini kwa kupitia bunge maoni ama kero za wananchi???
   
Loading...