Wamiliki wa Manchester United kwenye hati hati ya kupoteza miliki ya klabu hiyo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamiliki wa Manchester United kwenye hati hati ya kupoteza miliki ya klabu hiyo...

Discussion in 'Sports' started by Rutashubanyuma, Oct 22, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Sababu alizozitoa mshambuliaji wa hatari Wayne Rooney kuwa timu hiyo ya Manchester United haina uchu wa kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kwa kutonunua wachezaji wenye vipaji unaashiria ya kuwa kuporomoka kwa hadhi ya klabu hiyo kutaongeza mashinikizo ya wamiliki wa klabu hiyo - the Glaziers family - kuiuza klabu hiyo.

  Lipo kundi la wafanya biashara na wapenzi wa klabu hiyo nchini uingereza ambao wamekuwa kwenye jitihada za kutaka kuwalazimisha wamiliki hao kuiuza klabu hiyo bila ya mafanikio.

  Tatizo kwa the Glaziers ni kuwa hawakutumia fedha zao pekee katika kuinunua klabu hii na matokeo yake uraro wa madeni ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa kiwango cha klabu hiyo. Hawawezi kununua wachezaji bora duniani na hawawezi kuwashawishi wachezaji wao bora kubaki na klabu hiyo...Kuondoka kwa Christiano Ronaldo aliyeelekea Real Madrid na Tevez aliyetua Manchester City ulikuwa mwanzo wa dalili ya shughuli pevu ndani ya klabu hiyo.

  Tofauti na mwaka 2008 na 2009 ambapo klabu hiyo iliweza kuingia fainali za ubingwa wa ulaya mara mbili mfululizo na hivyo kutunisha mapato yao lakini msimu uliopita walishindwa hata kufikia nusu fainali na walitolewa na Bayern Munich katika robo fainali. Kushindwa kufika fainali kwenye mashindano hayo kumechangia sana kupoteza mapato......Vile vile timu hii kwenye ligi ya uingereza ilipokonywa taji lake na Chelsea......Maendeleo yake msimu huu kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya na ligi ya uingereza ni wa kusuasua tu.........

  Katika mazingira haya ni dhahiri kauli ya Rooney ya kuitema klabu hiyo kwa madai haina msukumo wa kufanya vizuri itaharakisha kwa wamiliki hao kujikuta wanapata wakati mgumu wa kulipa madeni ya klabu hiyo na hivyo kujikuta kwa amri ya mahakama wanatupwa nje ya miliki hiyo kama ilivyowatokea wamiliki wa Liverpool akina Gillet na Hicks ambao walijikuta hawana hela ya kulipa riba ya mikopo wanayodaiwa na mabenki ya huko ulaya na kutupiwa virago vyao na mahakama tena kwa hasara kubwa kwao.............
   
 2. g

  gutierez JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hata Roy Keane aliongea maneno hayo kusema wachezaji wa man utd kipindi kile hawana sifa za kuchezea man utd,na kuondoka yeye tu,man utd ikakaa msimu 1 tu,wakabeba premier league baada ya kulikosa takriban misimu 3 mfululizo.
   
Loading...