Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani, kwanini mnatutesa na kutukomoa Abiria wenu katika dakika 20 za huduma mnazotupa mkisimama njiani?

Mabasi yote ya safari ndefu yawe na vyoo vya ndani, pia kisheria baada ya masaa manne matano kupumzika iwe lazima. Hiyo itamsaidia dereva kupumzika kidogo na kupunguza ajali zinazosababishwa na uchovu.
Kila baada ya masaa manne upumzike Dar Bukoba utafika baada ya siku ngapi?
 
Ndio maana bado tuna safari ndefu,tuache siasa uchwara na tufanye maamuzi yanayoshirikisha ubongo,Dar to Mwanza ni kama 1200km huu ni mwendo wa masaa 15 kwa bus,ila kutokana na ubovu wa barabara,huduma za kijamii njiani hamna ni vurugu tupu,ile stendi ya pale Morogoro(nje kidogo ya msamvu)kuna kipindi zinakusanyika bus zaidi ya10 kwa wakati mmoja na kinachotokea pale ni vurugu tupu.

Wenzetu vitu vituo vizuri kila baada ya 100km nchi nzima. Kuna huduma zote unakuta, kuna Migahawa misafi na fast food chain kama McDonald, KFC, Starbuck, vyoo kama 30 visafi kabisa.

Hata sisi tunaweza ni uamuzi tu.
 
Kisayansi ni masaa 3 ndo kibofu cha6binadamu kinakuwa kimejaa. So waliweka baada ya masaa 4 siyo mbaya anagalau abiria achimbe dawa na hata anyooshe mwili hata kwa dk hizo 10 inatosha sana kwa afya.

Sasa basi siku moja nimepanda basi la ABC high class. Nilipanda saa 1.00 kutoka Mafinga. Kuchimba dawa ni Morogoro cate hotel. Umbali wa masaa 7 hadi nane wanatutesa sana aise

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app

Hili sipandi kabisa kuna siku niliwaambia waniache waende wakanisubiri maana nilikuwa nawaharibia wangeondoka
 
Yaan dk 20 unaona ndogo?alafu ww kama ni wa kiume unatia aibu futa hii post, watu wanaolalamika kwa mambo ya kijinga kama haya huwa ni wanawake..

Mwiso niseme kuna haja ya serikali kufanya iwe lazima kwa kila mtu mwenye miaka 17 kwenye JKT ili kuwa wakakamavu... taifa hili linapaswa kuwa na watu wakakamavu sio hawa wanaolilia kupewa dk 45 kwenda choon.. yaan ww ktk safari unawaza kunya na kula tu?

Unatia aibu mkuu
 
Dakika 30 unaziona nyingi eeeh, hizo ni dakika chache sana ukiwa na tatizo la tumbo, kama dakika 10 zinaisha hujamaliza haja ya kawaida, jiulize sasa ikiwa umeshikwa na tumbo zitakuwa ngapi. Omba sana usishikwe na tumbo unasafiri , safari utaiona chungu.
Kamwone Daktari mkuu yaan dakika kumi! i mean ten minutes haja ya kawaida(ukiacha la tumbo la kuhara) unakua hujamaliza???
 
Nilipanda basi moja nikiwa naenda kusini. Safari ya masaa zaidi ya kumi. baada ya masaa manne dereva akasimama porini. Akatangaza Muda wa kuchimba dawa, dakika tano wanawake kulia, wanaume kushoto. Watu wakashuka wa wakatembea kama mita kumi, naona wanawake wanachuchumaa, wanaume wanafungua zipu.

Umbali kati ya wanawake na wanaume ni kama mita tatu. Konda anawahimiza wamalize shughuli chapchap, yuko nervous anasema polisi wanaweza kutokea muda wowote. Dah nilichoka.

Hivi Simba, chui, chatu au mnyama yoyote mfano angetokea, si angeondoka na mtu.
We ni wale wanao ogopa hadi mende makabatini mkuu?
 
We ni wale wanao ogopa hadi mende makabatini mkuu?

Haha, standards, viwango, ustaarabu.

Mama, dada, bibi yako anachuchumaa hapa wewe uko pembeni unakojoa.

Kulinda utu, heshima ni muhimu kwa binadamu wote.

Usiwe mbinafsi, siku zote unajifikiria wewe. Look at big picture.Watu wote, wazee, walemavu, watoto, wanawake,wagonjwa.
 
Yaani inawezekana vipi dakika hizi hizi 20 mnazotupa tukiwa tumesimama Mombo au Msamvu au Singida Sisi Abiria wenu tuweze kuzigawa Kiustadi kwa Kula, Kukojoa na Kunya wakati tukifika tu haya maeneo tunakuwa Abiria wengi na waliotutangulia pia Kihuduma?

Kwani mkisema tu kuwa muda wa Kula na Kujisaidia Huduma zingine Muhimu za Kibinadamu (kama za Kukojoa na Kunya njiani Safarini) uwe ni dakika 30 au 45 mtapungukiwa nini?

Matokeo yake kwa hii Roho Mbaya yenu ya kutupa hizi dakika 20 njiani na Kutuwahishia Abiria kurudi katika Mabasi tuendelee na Safari wengine tunajikuta tunakula ndani ya Mabasi kwa Presha huku tunakunya na Kujinyea vile vile ila Siti zenu tu huwa zinatusaidia Kutusitiri mpaka tufikapo mwisho wa Kituo.

Na hakuna Kitendo ambacho KEROZENE nakichukia kama unakuta Abiria umemuomba Kondakta na Dereva unataka Kukojoa halafu unashuka na unaanza Kufungua Zipu ili uuchomoe 'Mkurudungu' wako ukojoe unasikia Dereva anakupigia Honi matokeo yake kwa Kitete ( Presha ) unajikuta unakojoa kidogo tu au unaacha na kujikuta ukianza Kukimbia kuwahi ndani ya Basi huku Ukijamba hovyo Porini hadi unawashtua Vicheche waliojipumzisha. Suruali umeishikilia ikiwa Magotini na kuja kuvalia vizuri ndani ya Gari mlangoni huku Abiria Wenzako wakikukodolea tu Mubashara.

SUMATRA tafadhalini ongeeni na TABOA kuwa Abiria tunateseka na hizi dakika zao 20 tu wanazotupa tukiwa njiani na sasa tunataka tupewe ama dakika 30 au 45 ili tuweze Kujinafasi vizuri kwa Huduma zote Tatu muhimu za Kula, Kukojoa na Kunya ndipo tuwe tunaendelea na Safari zetu.

Hizi dakika zao 20 Kimahesabu tu hata kama ukiwa ni 'Mathematician' utazigawa vipi kwa Foleni ya Chakula unayoikuta? Kwa Foleni ya Watu Kukojoa katika Vyoo vichache achilia mbali wale ambao unawakuta nao wanataka Kunya ila wamekuta wameshawahiwa na wanaojua Kunya wakiwa Wanaguna tu Vyooni, kutoka haraka hawatoki na hata wakitoka utaambulia Msonyo na Bonge la Kimba linakukaribisha ili Kwanza ulione ndipo 'Uliflashi' likuage halafu nawe uanze Kushughulikia na lako lililoko Tumboni na linataka kutoka?
Ila mabasi mengi hutoa dakika kumi tu kwa abiria kupata chakula na pia kwenda maliwato kujisaidia. Huu ni ukatili usiomithilika.
 
Nchi imejaa misukule mioga, inapelekeshwa kama nyumbu! Hivi hili nalo ni jambo la kulalamika? Kwa nini abiria kwa umoja wao wasiseme kuwa muda hautoshi? Hii nchi yetu ina laana gani watu wanapelekeshwa kila kona na kuhoji hawahoji?
 
Back
Top Bottom